Mwamposa: End of an Era au mwanzo wa michezo michafu?

Nimeelewa kuwa Yesu nae ana Mungu kwahiyo yeye si Mungu.
Nimeelewa Yesu nae ana baba kama sisi,
Ndo maana sasa nikauliza huyo Yesu asie na Mungu alie na baba kama sisi ndo yule yule alieuliwa pale msalabani?
Marko 15;34

Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu,Eloi eloi lama sabakhtani,
Maana yake Mungu wangu,Mungu wangu,mbona unaniacha?

Jibu la swali lako,ndio huyo huyo.
 
Mwamposa ni tapeli na mhalifu anayetumiwa na Allah Samia.

Aliua watu 18, Moshi. Waliochanganyikiwa tu ndio wanamuona Mtume
 
Utaelewa tu hao huitwa wapakwa mafuta na wana kibali mbele za bwana
 
Mkuu Mungu angekuwa habagui basi kusingekuwa na waumini kisha kuwe na mitume mapdri masheikh nk.
Kusingekuwa na ubaguzi basi kusingekuwa na sehemu zingine takatifu ambazo wengine inatakiwa muende kuzitembelea...
Kungekuwa na usawa basi Afrika nako kungekuwa na sehemu takatifu kama ilivo maka madina na yerusalemu.
 
Marko 15;34

Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu,Eloi eloi lama sabakhtani,
Maana yake Mungu wangu,Mungu wangu,mbona unaniacha?

Jibu la swali lako,ndio huyo huyo.
Kama ni huyo huyo kwa maana ni binadamu kama sie
Sasa iweje yeye auliwe kwa lengo la kusamehewa madhambi wengine,
Yeye alikuwa na umaalum gani kwamba kifo chake kiwe misamaha ya wengine wakati nae ni binadamu kama wengine?
 
Mkuu Mungu angekuwa habagui basi kusingekuwa na waumini kisha kuwe na mitume mapdri masheikh nk.
Kwahiyo Serikali unaweza kusema inabagua coz kuna mawaziri,wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya....
Kungekuwa na usawa basi Afrika nako kungekuwa na sehemu takatifu kama ilivo maka madina na yerusalemu.
Unajua ni kwanini hizo sehemu zinaitwa takatifu? coz kuna matukio yaliyo tokea ambayo ndio panafanywa kua patakatifu,

Kwahiyo watu wa Kigoma,Tabora,Nzega..nao walalamike kwanini Dodoma ndio mji mkuu wa nchi? kwanini kusiwe mji mkuu huku kwetu Nanjilinji?
 
Wewe nae umekuja kivingine hakuna jambo lolote mimi nililofanya yesu kasema nisifanye kwa sababu mimi sijawahi zungumza na Yesu hata siku moja.
Au wewe una ushahidi yesu aliniambia nisifanye kitu fulani nikafanya??
Sasa ulikuwa unauliza kwanini Yesu anawaacha hao wahuni wa imani kwa misingi ipi? ?

Walikwambia Yesu kawaambia wasiwe wahuni wa imani ? ?
 
Kwamba Yesu ndo huyo huyo Mungu kashuka kuwakomboa wanadamu?
Ukisema anawakomboa na maovu ya shetani kwa maana hiyo shetani anauwezo na nguvu kuliko yeye Yesu?
Au huyo shetani alikuwa anampokonya viumbe wake?
Wakati huo huo huyo shetani yeye katokea wapi?
 
Kama ni huyo huyo kwa maana ni binadamu kama sie
Sasa iweje yeye auliwe kwa lengo la kusamehewa madhambi wengine,
Huu ni uzushi tu,
Yeye alikuwa na umaalum gani kwamba kifo chake kiwe misamaha ya wengine wakati nae ni binadamu kama wengine?
Kifo chake sio misamaha ya wengine,
''Kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe,siku hiyo itafika''
 
Watajuana wenyewe
 
Kuna vitu fulani fulani wanavifuata vinaitwa vifaa vya kiroho hua anawauzia hivyo kwa ajili ya shughuli fulani fulani, nilipotumia maji nikanywa na mafuta nimeacha kabisa kuharisha Mtume.. kweli umeacha kuharisha? Ndio mtume tumbo la kuhara limeacha kabisa.. Mwaposa anacheka.. hahaha Mpogie Yesu Makofi.. jina la Yesu linatumika vibaya sana kwa watu kujiingizia kipato
 
Sasa unafananishaje mji mkuu na sehemu takatifu!!
Mfano tumeona uhamisho ukitoka Dar kwenda Dodoma kwa maana hiyo hata mahali takatifu panaweza hamishwa?
Unafananishaje uongozi wa binadamu ambao hutenguliwa muda wowote je na uongozi wa Mumgu nao hutenguliwa?

Viongozi wa dini nao hitenguliwa kama wanavotemguliwaga mawaziri?
Mfano umi mwalimu alikuwa waziri wa afya alitenguliwa na kukosa cheo hicho hebu nitolee mfano nabii/mtume wa Mungu alietenguliwa na kukosa cheo hicho.
 
Sasa ulikuwa unauliza kwanini Yesu anawaacha hao wahuni wa imani kwa misingi ipi? ?

Walikwambia Yesu kawaambia wasiwe wahuni wa imani ? ?
Bila shaka wewe ni Kondoo
Hebu achia mijadala wanaoiweza nadhani wewe huu mjadala ni mzito kwako.
Nimekuuliza swali badala ujibu unaniuliza swali tena..
Au huoni wenzio wanavojibu ukajifunza!
 
Nimetumia hiyo mifano ili iwe rahisi kwako kuelewa coz nimeona kua uelewa wako bado upo mbali sana,
Viongozi wa dini nao hitenguliwa kama wanavotemguliwaga mawaziri?
Hiyo ni mifano tu,ili iwe rahisi kwako kuelewa,najua hata nikikupa majibu ya aina gani,ni lazima utakuja na maswali mengine tu coz inaonekana huelewi au unafanya makusudi,kuna kitu umekilenga zaidi kwenye maswali yako kuliko kutaka kuelewa, I've already noticed.
 
Halafu moja ya jambo linalonilashangaza ambalo kwangu linaongezea point Biblia ni wasioamini kuhangaika na Biblia! !

Kati ya vitu nisivyohangaika navyo ni
Quran,
Vedas,
Maandiko ya Wamisri wa Kale,
sijui maandiko ya Mayas,
maandiki ya wa Tao n.k,

kwasababu kichwani nimeshavi cancel!

Hata nguvu ya kuviongelea sina!

Hata huwa siviwazi! !

Mtu haamini Mungu lakini kutwa kumuongelea Mungu ambaye hayupo! ! !

Sijui nguvu ya kuongelea kitu usichokiamini kitu ambacho hakipo kila siku mnatoa wapi! ! !

Oohh ni kwasababu mnajaribu kupingana na KWELI! Hiyo kwakweli ni kazi mtafanya kila siku!

Ni kazi ya ule ufalme mwingine unaopingana na Ufalme wa MUNGU.

Na bado hamuamini YESU amekaribia kurudi! ! ! Uzao wa Esau na Yakobo Live ulingoni! Uzao wa mwanamke na wa nyoka!

"Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine. Hapa na pale patakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi."
Mathayo.24.7.BHN
 
Huu ni uzushi tu,

Kifo chake sio misamaha ya wengine,
''Kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe,siku hiyo itafika''
Mkuu yohana 3:16 hii ilikuwa na maana gani nifafanulie
''Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…