Mwamposa: End of an Era au mwanzo wa michezo michafu?

Mwamposa: End of an Era au mwanzo wa michezo michafu?

Kwamba Yesu ndo huyo huyo Mungu kashuka kuwakomboa wanadamu?
Ukisema anawakomboa na maovu ya shetani kwa maana hiyo shetani anauwezo na nguvu kuliko yeye Yesu?
Au huyo shetani alikuwa anampokonya viumbe wake?
Wakati huo huo huyo shetani yeye katokea wapi?
Baasiiiiii umemaliza
Mi na wewe tuna mtazamo same same hapa tunajiuliza na kujijibu wenyewe ilifaa tupate mtu aliekinyume na sisi ili mjadala unoge
 
Hahaha kuna Mzee mkewe anapenda sana kumsikiliza huyo jamaa kwenye redio, sasa juzi nikakatisha hapo nikakuta huyo mkewe kafungulia redio sauti kubwa sana mwaposa huyo, sasa kwenye shuhuda kuna mama alisema alikua na uvimbe sijui nini nikasikia mzee amesonya kwanza halafu akaanza kuuliza maswali aliulizwa maswali mengi mengi kisha mwisho aka doubt kwamba huyu jamaa mboni km anatupanga mboni km anacheza na akili zetu hili jambo haliwezekani
Picha linaanza wafanya kazi wake wanao tangaza shuhuda pamoja na watoa shuhuda wote wana ongea kwa melody moja ile ile, Hdi najiuliza ina maana watu hawana akili kiasi hiki
 
Kwa Mwamposa, yeye na vitu vyake vyote vina mwanzo na vitakuwa na mwisho. Hilo halina shaka; sio suala la mjadala.

Ila, hakuna mwanzo wala mwisho wa mwisho wa michezo michafu katika uwepo wa binadamu duniani (Mhubiri 1:9).

Kwa kadiri binadamu anavyoathiriwa sana na ujinga, hisia na imani za kishirikina, na hulka ya kuepuka uhalisia na uwajibikaji kwa maisha yake, ataendelea kuwa mhanga kwa walaghai wa kila aina: kisiasa, kidini na kijamii.

Watu aina ya Mwamposa wanaotegeneza "cult following" kwa ulaghai wa kutumia imani ya kidini walikuwepo tangu enzi za kale na hawataisha hadi mwisho wa binadamu. Vivyo hivyo kwenye fani zote kuna cults zake.
 
Ukishajifungamanisha na CCM tu ndiyo kwishaaa..Juzi alikuwa Katoro anafosi kuwaombea wachimbaji wa Dhahabu kwa nguvu
 
I like how these animations bring True Bible History to life:

The 10 Commandments


View: https://youtu.be/tgxws7YDk-c?si=pYtakdqNxZsR9QOR

What happened in Egypt is a shadow of what will soon happen over the whole earth.

The Great Tribulation is coming. Final attempt to bring the last generation to repentance.

JESUS IS LORD!

MAKE WAY FOR THE KING OF KINGS! 🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
 
Kitendo cha kuanza ujinga eti anakuombea unapokea hela kwenye simu bila kujua imetoka wapi hakika nakuunga mkono kabisa!!
Serikali inatakiwa imfukuze hapo kwenye eneo la Serikali, yule ni tapele hana ofisi wala mali zisizo hamishika Mali zake ni Udongo na Mafuta, anakusanya pesa ana zipeleka nje ya nchi ili siku libuma anasepa na Kibegi kidogo cha ngu hana chakupoteza.
 
Yote anayoyafanya Mwaposa sio mapya yalishawahi kufanywa na wahuni wengi tu kama Kakobe, Getruda Rwakatare ( marehemu), ni suala la muda tu naye atapita japo wajinga wengi watakuwa wamepigwa.
Mwamposa huu ni wakati wake na atapotea ni kama Walivyo wachezaji wa mpira au Wasanii huja nakupotea na kuja wengine.
 
Yule na Gwajima wote ni waganga wavaa suti , ile mikesha yake anatumia nguvu uganga kupeleka watu .Hao wafuasi wake wamrogwa , hata aseme hii wanafurahi .

Kiufupi , kwa kutumia sayansi ya pwani yule kawafanya watu misekule yaani anachotaka wanafanya.
 
Habari,

Kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia ile video ya Mtume na Nabii Boniface Mwamposa akitoa ushuhuda na dokezo kuhusu kuingia chumba cha marubani na kumuuliza rubani kwanini ndege haitembei kwa speed.

Video ilienda viral kwa sababu y maelezo yake na mazingira yake ukiwa ndani ya ndege na jinsi ya kumfikia rubani wewe abiria kuwa ni kitu ambacho hakiwezekani kwa hali ya kawaida.

Kabla hili halijakaa sawa naona limeibuka lingine huko mwanza nadhani la kuponya viwete. Ukiangalia yale magongo ambayo anadai walikuwa wanatumia viwete ni almost yote ni mapya, hayajawahi kutumika au kama yametumika basi ni mara moja tu, hii inaleta ukakasi kwenye kuamini maneno yake na ushuhudu wake.

Je ni end of an era au watu wake wa karibu wameshamchoka na wameanza kumuumbua? Maisha ya imani huwa na ups and down, nadhani kama kuna kitu anafanya makosa kwa sasa basi ni kuamini ataendelea kuwalisha ujinga waumini wake kwa muda wote.

As kiongozi wa dini anapaswa sana kuchunga ndimi yake, kauli zake na vitendo vyake anvyofanya katika jamii, Mimbari ni sehemu patakatifu, si sahihi kutoa maneno yanayoacha dalili za uongo hata mara moja.

Na kwa sisi waamini, As a bible says "Mtafute sana elimu, usimwache aende zake" basi yatubidi kutafuta ukweli kwa yale yatupasayo, kuendelea kulishwa uongo ni kukosa hekima na maarifa, Mwenyezi Mungu ametuumba kuwa na uwezo wa kufikiri, kuhoji na kufanya tafakari ya yale tuyaonayo, tuyasikiayo na tuambiayo.

Kama lengo la kufanya ibada ni kumfikia mwenyezi Mungu basi kumbuka nabii mwongo hawezi kukufikisha kwenye hilo lengo lako, Kamwe kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzake.

Kwa sisi watafuta miujiza, tuaomini ulonzi na wafuta mafanikio, Je kwa Mtume Boniface Mwamposa, ni End of an era au aliteleza tu?

NB: Usihukumu, kwa maana usije kuhukumiwa, ila usiache kukemea uovu, kwakuwa muovu siku zote ni ibilisi.
Mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kutumia hata dk1 kumsikiliza mtu mhuni kama mwamposa.
Shida nchi hii ina mijinga mingi ngoja waipige
 
Ile number ya mwanza na katoro lazima kobazi muweweseke!
Injili lazima isonge mbele na watakaopeleka mbele ni Hawa Hawa unaobeza kwa bandiko reeeefu
 
As long as wajinga wajinga na wapumbavu bado wapo huyo mjasiriamali hashuki leo wala kesho!!

Mtasubiri sana!!!
20250326_121631.jpg
 
Haiwezi kuwa end of era
Suala la Kondoo kupigwa halikuanza leo
Kwani kina kakobe walichokuwa wanafanya ni tofauti na anachofanya mwamposa?
Ataondoka atakuja mwingine atafanya hivi hivi.
Jitahidi sana uelewe neno KONDOO kama biblia inavotambua waumini wake ni KONDOO WA BWANA.
Si unamjua kondoo sifa zake!
Kwamba kwakuwa kondoo ni mpole basi upole wetu ndio unasababisha tutaendelea kupigwa vizazi hadi vizazi?
 
Back
Top Bottom