Tetesi: Mwamposa mbioni kuinunua E-FM, TV-E

Ni kweli aisee niliwahi kukaa nawafanyakazi wa RFA,Star TV na Kiss FM kipindi za moto.Ila walikuwa na njaa kali sana ila majina makubwaaa.
Hatari sana
 
  • Thanks
Reactions: EEX
Babu una mengi jamani? Hadi kuoa kabisa?
Loh!

Siwezi kukuacha peke yako na mkweo, huchelei kumpa mbinu za kijangili.
Yalikuwa ni mapito tu Mjukuu, na bahati mbaya ndiyo kipindi nilipokea pension yangu ya Mkupuo 😜

Huyo Mkwe siwezi kumpa mbinu za kufanya aongeze Mke, zaidi zaidi nitampa zitakazowafanya mdumu pamoja hadi mtakapofikia umri wetu Babu zenu 🤗
 
View attachment 3184579

Katika kilichoonekana kama kusogeza ‘huduma’ karibu kwa waumini wa kanisa lake, Askofu na Mtume Boniface Mwamposa yupo kwenye mchakato wa kuinunua EFM Company Limited.

EFM ni kampuni iliyosajiliwa kama chombo cha habari, ikiwa na umiliki wa Redio na Televisheni.

Mwamposa na Mkurugenzi wameshibana…
Mkurugenzi wa EFM Bwana Francis Ciza maarufu kama Majizzo (Mume wa muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’) wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu na Askofu Mwamposa katika kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mikutano na ibada zinazoendeshwa na Mwamposa kwa kipindi kirefu.

Baada ya kufanya kazi pamoja kwa kipindi kirefu, hivi sasa wapo kwenye mazungumzo ya kumuuzia media hiyo Mwamposa.

Nimetaarifiwa kwamba vikao vya mauziano hayo vinafanyika kwa siri nyumbani kwa Majizo, huku dau likiwa bado halifahamiki lakini ikielezwa Majizzo anataka dau kubwa linalokwamisha taratibu za mauziano kuanza.

EFM Radio imemshinda Majizzo!
Kwa kipindi kirefu kumekuwa na minong’ono ya wafanyakazi kushindwa kulipwa mishahara kwa wakati, ikisemekana wanaolipwa bila kusumbuliwa ni wale watangazaji wenye majina makubwa pekee, huku wale wachanga wakipitia wakati mgumu kimalipo.

Taarifa za uhakika ni kwamba redio hiyo imemshinda Majizzo, changamoto za uendeshaji zimemuelemea na inasemekana kama sababu kuu ya yeye kufikia uamuzi wa kumuuzia Mwamposa kampuni yote hiyo ya habari iliyokuja kuzipa chachu redio kongwe miaka ya mwanzoni mwa uzinduzi wake.

Majizzo siye mmiliki pekee…
Taarifa za usajili wa kampuni zinaonesha kumilikiwa na ndugu watatu, yeye Majizzo (Francis Ciza 40%) ndugu zake kwa upande wa baba yake mlezi Mzee Ciza… Jean Ciza 40% pamoja na Justine Ciza 20%

Wenu katika unyetishaji, mimi na chanzo changu,

Nifah.
Acha Injili iendelee
 
Na ushindani unazidi kua mkubwa sana, crown, wasafi, bongo fm na nyinginezo zote zina maudhui sawa na hao EFM.

Competition imekua kali upande huo, ukilegea umeliwa na watangazaji maarufu watakukimbia.
 
Leo Vishu umeacha utata, umetema facts.
Safi.
 
Yalikuwa ni mapito tu Mjukuu, na bahati mbaya ndiyo kipindi nilipokea pension yangu ya Mkupuo 😜

Huyo Mkwe siwezi kumpa mbinu za kufanya aongeze Mke, zaidi zaidi nitampa zitakazowafanya mdumu pamoja hadi mtakapofikia umri wetu Babu zenu 🤗
Amen, pole kwa mapito Babu.
 
Oooyeeeah ni Niffer tena...

Na chanzo chetu ni kile kile kama TBC ukweli na uhakika n swala la muda let's wait and see...
Chanzo makini, hakijawahi kuyumba!
 
UKiona mtu anakwenda kwa Mwamposa ujue kuwa anachangamoto zake,wewe ambae hauna changamoto yoyote ya kiafya wala kiuchumi utawaona wanaokwenda kuwa niwajinga na MUNGU akusimamie mkuu kwa hilo yasikukute!. By theway Nimeipenda T shirt ya mtume Mwamposa.
 
View attachment 3184579

Katika kilichoonekana kama kusogeza ‘huduma’ karibu kwa waumini wa kanisa lake, Askofu na Mtume Boniface Mwamposa yupo kwenye mchakato wa kuinunua EFM Company Limited.

EFM ni kampuni iliyosajiliwa kama chombo cha habari, ikiwa na umiliki wa Redio na Televisheni.

Mwamposa na Mkurugenzi wameshibana…
Mkurugenzi wa EFM Bwana Francis Ciza maarufu kama Majizzo (Mume wa muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’) wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu na Askofu Mwamposa katika kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mikutano na ibada zinazoendeshwa na Mwamposa kwa kipindi kirefu.

Baada ya kufanya kazi pamoja kwa kipindi kirefu, hivi sasa wapo kwenye mazungumzo ya kumuuzia media hiyo Mwamposa.

Nimetaarifiwa kwamba vikao vya mauziano hayo vinafanyika kwa siri nyumbani kwa Majizo, huku dau likiwa bado halifahamiki lakini ikielezwa Majizzo anataka dau kubwa linalokwamisha taratibu za mauziano kuanza.

EFM Radio imemshinda Majizzo!
Kwa kipindi kirefu kumekuwa na minong’ono ya wafanyakazi kushindwa kulipwa mishahara kwa wakati, ikisemekana wanaolipwa bila kusumbuliwa ni wale watangazaji wenye majina makubwa pekee, huku wale wachanga wakipitia wakati mgumu kimalipo.

Taarifa za uhakika ni kwamba redio hiyo imemshinda Majizzo, changamoto za uendeshaji zimemuelemea na inasemekana kama sababu kuu ya yeye kufikia uamuzi wa kumuuzia Mwamposa kampuni yote hiyo ya habari iliyokuja kuzipa chachu redio kongwe miaka ya mwanzoni mwa uzinduzi wake.

Majizzo siye mmiliki pekee…
Taarifa za usajili wa kampuni zinaonesha kumilikiwa na ndugu watatu, yeye Majizzo (Francis Ciza 40%) ndugu zake kwa upande wa baba yake mlezi Mzee Ciza… Jean Ciza 40% pamoja na Justine Ciza 20%

Wenu katika unyetishaji, mimi na chanzo changu,

Nifah.
Majizzo ameuza unga kakamata mahela akaamua ayatakatishe kwenye media business.
Sema alitumia akili kutojifanya yeye sio mmilike peke yake
 
Back
Top Bottom