"Juzi nilikuwa Bungeni na tulikuwa Watumishi wengi tu ila nashangaa Picha zangu tu ndizo zinasambazwa kwa Mabaya. Nikibadilisha Viatu hapa Madhabahuni, nikijifuta Jasho na Kitambaa na Nikivaa Cheni naambiwa Mimi ni Freemasons kwanini?" Amehoji Mtume Wenu Mwamposa.
Chanzo: Tv Channel yake muda huu
Kazi ipo.....!!!!!!
=============
Akizungumza na waumini wake, leo Jumapili Februari 12, 2023, Mwamposa amesema: "Yaani mimi nianze kujibizana na watu kwenye mitandao wanavyosema Mwamposa Freemason, nami niingine kwenye mitandao kuanza kuwajibu kuwa mimi si Freemason, sina muda huo hata kidogo.
"Kila kitu nikifanya inakuwa gumzo, juzi nilikuwa Bungeni, nilifanya ibada kwa Wabunge, nilipotoka pale nashangaa picha zinazagaa kuhusu mimi licha ya kuwa watumishi tulikuwa wengi.
"Hata nikiwa hapa (Kanisani) huwa wanashangaa ninavyobadilisha viatu, nabadilisha kwa kuwa mafuta ninayotembea nayo yakimwagikia kwenye kiatu yanakiharibu, hivyo nafaa viatu ambavyo nakuwa comfortable kuzunguka nacho.
"Hata wakiona nimevaa cheni inakuwa gumzo, hata nikivaa kitambaa inakuwa gumzo."
Chanzo: Mwamposa Live