Mwamposa: Mimi siyo Freemasons na sijui kwanini naandamwa na kusingiziwa vingi

Mwamposa: Mimi siyo Freemasons na sijui kwanini naandamwa na kusingiziwa vingi

Mambo ya watumishi wa Mungu iwe masheikh au makaasisi waachie wenyewe maana wanajua nani wanamtumikia
Wanapoingilia yale yasiyo kwenye uwezo wao, lazima tuwajulishe. Mimi siyo Mwislamu, lakini niseme ukweli, sijasikia au kuona Sheikh au Mhubiri wa Kiislamu akidai kuponya, kuleta au kuongeza utajiri, wala hawana vitabu vya utajirisho. Lakini dini ya Kikristo umeingiliwa na kujaa matapeli wengi mno. Kazi yao kudanganya watu kwa kutumia jina la Mungu kujitajirisha. Hii ndiyo sababu utaona ugomvi mwingi kwenye hayo makanisa. Wengine hutumiaa umaarufu wao wa kidini kujiingiza panono zaidi, kama vile kwenye siasa (Rwakatare/Gwajima). Wote hao siyo wacha Mungu bali matapeli. Ndiyo maana nyumba zao za igada hata kama zimejengwa na waumini lakini ni mali binafsi za hao manabii wa uongo.
 
Ila maaskofu wa katoliki kuvaa micheni mikubwa ya msalaba na Pete ya dhahabu ya Ki Askofu ni sawa tu? Shida ni Kwa Mwamposa tu?

Padre wa parokia tu wa kanisa katoliki gari ya thamani ya chini anayotumia ni Prado.
Kuna makanisa au madhehebu kazi zao za kiroho na kibinadamu zinaonekana. Makanisa katoliki yana huduma nyingi za jamii zinazojulikana. Unamlinganisha nabii wako ambaye pesa yote anayokusanya anakula na mke wake na watoto wake. Mali zote za madhahabu ni mali yake, pesa anaweka account ya binafi. Hao maaskofu Katoliki unaowasema wana mahospitali, kliniki, nchi nzima. Hivi unajuwa hospitali ya Bugando imejengwa na inaendeshwa na Kanisa katoliki. Na ile ile ya Moshi (KCMC) pia ni kanisa la Kianglikana au Kilutheri. Wewe kaa na matapeli wako wanaokudanganya wanawaponyama wasiyotembea kumbe uongo.
 
Wanapoingilia yale yasiyo kwenye uwezo wao, lazima tuwajulishe. Mimi siyo Mwislamu, lakini niseme ukweli, sijasikia au kuona Sheikh au Mhubiri wa Kiislamu akidai kuponya, kuleta au kuongeza utajiri, wala hawana vitabu vya utajirisho. Lakini dini ya Kikristo umeingiliwa na kujaa matapeli wengi mno. Kazi yao kudanganya watu kwa kutumia jina la Mungu kujitajirisha. Hii ndiyo sababu utaona ugomvi mwingi kwenye hayo makanisa. Wengine hutumiaa umaarufu wao wa kidini kujiingiza panono zaidi, kama vile kwenye siasa (Rwakatare/Gwajima). Wote hao siyo wacha Mungu bali matapeli. Ndiyo maana nyumba zao za igada hata kama zimejengwa na waumini lakini ni mali binafsi za hao manabii wa uongo.
Yesu ambaye ndiye Neno la Mungu alishasema walio wake watatambua kazi zao wanaoijiita watimishi wake....
 
Jumapili iliyopita nilikuwa naangalia ibada ya kanisa la WRM lipo kivule matembele ya pili. Hili kanisa lilikuwa limefungwa takribani miezi miwili na serikali. Sasa wiki iliyopita ndo likawa limefunguliwa. Yule mchingaji wake akawa anaelezea chanzo cha kufungiwa hilo kanisa. Aisee kumbe ni fitna kutoka kwa makanisa menzake hayo hayo. Siyo siri nilijisikia vibaya nikaona haya makanisa yote ni utapeli na biashara tu. Watu wa Mungu naowaamini ukiacha dhehebu langu la RC ni mwakasege na mchungaji FJ Katunzi(huyu mchungaji ntamheshimu mpaka kesho kwa sababu aliniponya pumu mwaka 2004)
Mungu alikuponya na siyo padri. Padri hana uwezo huo. Alikuombea na Mungu akasikiliza sala zake na zako. Hata hivyo, pumu huwa inafikia mahali inapona yenyewe. Mimi watoto wangu wawili wamekuwa na pumu tena kali saana mpaka katika umri wa miaka 18 ikawa imeisha. Sasa hawa watoto wako kwenye 40s na hawajawi kupata attack ya pumu.
 
Mimi kuna siku nilienda nilipofika nikaambiwa niandike majina yangu, historia yangu na sababu iliyonipeleka, basi nikaamua kuandika majina halafu sababu iliyonipeleka nikaongopa kuna mahali nadai pesa nyingi ila silipwi ndio maana nimekuja niombewe. Ilipofika muda wa maombi nikashangaa kuhania anauliza Skayla ndio yupi, nikasimama, akaniambia unadai pesa mahahali na ninaona kabisa wanataka kukudhulumu kwa sababu kuna roho za wachawi zimeshikilia uchumi wako, nikabaki natoa macho, akasema inabifi unione kabla hujatoka hapa nitakupa mafuta . Na ninaona roho wa Mungu akiniambia wiki hii haitaisha hujapokea pesa yako, na ukipokra unapaswa kuikumbuka mafhabahu hii kwa sadaka

Ibada iliposiha sikukanyaga tena kwenye hilo kanisa maana nilidanganya kwamba nimeenda pale ili niombewe niwlipwe deni, kumbe kuhani huwa anadanganya watu kwamba ana maono wakati anasoma taarifa za watu walizoandika, nilijikuta nashangaa maana sikua namdai mtu sasa hapo aliponiambia kwamba anaona wachawi wameshika uchumi wangu ndio nilibaki hooi
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Mwamposa tapeli TU,
1. Kwañn viwete anaoponyesha kwny mikutano yake wote wageni eneo la mkutano, hamna hata mwenyeji mmoja[emoji2]
2. Viwete wanaoponyeshwa ulemavu,
wote magongo yao Huwa Ni mapya kabisa brand new. Huwa wanapata wapi muda wa kuyaosha yatakate yawe mapya ndo waende kwny mkutano wake[emoji1787]

3. Sijawahi kuskia mwamposa akamwangusha pepo tajiri yoyote yule,
Kwake waanguka mapepo wote Ni maskini TU[emoji38]
😂😂😂 izi imani hizi
 
Jumapili iliyopita nilikuwa naangalia ibada ya kanisa la WRM lipo kivule matembele ya pili. Hili kanisa lilikuwa limefungwa takribani miezi miwili na serikali. Sasa wiki iliyopita ndo likawa limefunguliwa. Yule mchingaji wake akawa anaelezea chanzo cha kufungiwa hilo kanisa. Aisee kumbe ni fitna kutoka kwa makanisa menzake hayo hayo. Siyo siri nilijisikia vibaya nikaona haya makanisa yote ni utapeli na biashara tu. Watu wa Mungu naowaamini ukiacha dhehebu langu la RC ni mwakasege na mchungaji FJ Katunzi(huyu mchungaji ntamheshimu mpaka kesho kwa sababu aliniponya pumu mwaka 2004)
Kupona pumu tu kwan kina mwamposa hawajawai kuwaponya watu magonjwa mengine acheni wivu na husda ,,mwamposa chapa Kaz watu elfu 20 kwa ibada moja lazma utapigwa majungu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mwamposa tapeli TU,
1. Kwañn viwete anaoponyesha kwny mikutano yake wote wageni eneo la mkutano, hamna hata mwenyeji mmoja[emoji2]
2. Viwete wanaoponyeshwa ulemavu,
wote magongo yao Huwa Ni mapya kabisa brand new. Huwa wanapata wapi muda wa kuyaosha yatakate yawe mapya ndo waende kwny mkutano wake[emoji1787]

3. Sijawahi kuskia mwamposa akamwangusha pepo tajiri yoyote yule,
Kwake waanguka mapepo wote Ni maskini TU[emoji38]
Maswali ya msingi sana haya.

Sijawahi kufuatilia kumbe ndivyo inavyokuwa?
 
Watu wa Mungu naowaamini ukiacha dhehebu langu la RC ni mwakasege na mchungaji FJ Katunzi(huyu mchungaji ntamheshimu mpaka kesho kwa sababu aliniponya pumu mwaka 2004)
Mungu ndiye mponyaji siku zote zingatia hili..............huyo mchungaji alitumika tu na Mungu kupitisha uponyaji wako.
 
"Juzi nilikuwa Bungeni na tulikuwa Watumishi wengi tu ila nashangaa Picha zangu tu ndizo zinasambazwa kwa Mabaya. Nikibadilisha Viatu hapa Madhabahuni, nikijifuta Jasho na Kitambaa na Nikivaa Cheni naambiwa Mimi ni Freemasons kwanini?" Amehoji Mtume Wenu Mwamposa.

Chanzo: Tv Channel yake muda huu

Kazi ipo.....!!!!!!

=============

Akizungumza na waumini wake, leo Jumapili Februari 12, 2023, Mwamposa amesema: "Yaani mimi nianze kujibizana na watu kwenye mitandao wanavyosema Mwamposa Freemason, nami niingine kwenye mitandao kuanza kuwajibu kuwa mimi si Freemason, sina muda huo hata kidogo.

"Kila kitu nikifanya inakuwa gumzo, juzi nilikuwa Bungeni, nilifanya ibada kwa Wabunge, nilipotoka pale nashangaa picha zinazagaa kuhusu mimi licha ya kuwa watumishi tulikuwa wengi.

"Hata nikiwa hapa (Kanisani) huwa wanashangaa ninavyobadilisha viatu, nabadilisha kwa kuwa mafuta ninayotembea nayo yakimwagikia kwenye kiatu yanakiharibu, hivyo nafaa viatu ambavyo nakuwa comfortable kuzunguka nacho.

"Hata wakiona nimevaa cheni inakuwa gumzo, hata nikivaa kitambaa inakuwa gumzo."

Chanzo: Mwamposa Live
Mganga wa kienyeji.
 
Back
Top Bottom