Mwamposa: Mimi siyo Freemasons na sijui kwanini naandamwa na kusingiziwa vingi

Mwamposa: Mimi siyo Freemasons na sijui kwanini naandamwa na kusingiziwa vingi

Mwamposa tapeli TU,
1. Kwañn viwete anaoponyesha kwny mikutano yake wote wageni eneo la mkutano, hamna hata mwenyeji mmoja[emoji2]
2. Viwete wanaoponyeshwa ulemavu,
wote magongo yao Huwa Ni mapya kabisa brand new. Huwa wanapata wapi muda wa kuyaosha yatakate yawe mapya ndo waende kwny mkutano wake[emoji1787]

3. Sijawahi kuskia mwamposa akamwangusha pepo tajiri yoyote yule,
Kwake waanguka mapepo wote Ni maskini TU[emoji38]

Point zako zakitoto sana,hujawahi kubwa na matatizo utawatafuta hao akina mwamposa.
 
"Juzi nilikuwa Bungeni na tulikuwa Watumishi wengi tu ila nashangaa Picha zangu tu ndizo zinasambazwa kwa Mabaya. Nikibadilisha Viatu hapa Madhabahuni, nikijifuta Jasho na Kitambaa na Nikivaa Cheni naambiwa Mimi ni Freemasons kwanini?" Amehoji Mtume Wenu Mwamposa.

Chanzo: Tv Channel yake muda huu

Kazi ipo.....!!!!!!

=============

Akizungumza na waumini wake, leo Jumapili Februari 12, 2023, Mwamposa amesema: "Yaani mimi nianze kujibizana na watu kwenye mitandao wanavyosema Mwamposa Freemason, nami niingine kwenye mitandao kuanza kuwajibu kuwa mimi si Freemason, sina muda huo hata kidogo.

"Kila kitu nikifanya inakuwa gumzo, juzi nilikuwa Bungeni, nilifanya ibada kwa Wabunge, nilipotoka pale nashangaa picha zinazagaa kuhusu mimi licha ya kuwa watumishi tulikuwa wengi.

"Hata nikiwa hapa (Kanisani) huwa wanashangaa ninavyobadilisha viatu, nabadilisha kwa kuwa mafuta ninayotembea nayo yakimwagikia kwenye kiatu yanakiharibu, hivyo nafaa viatu ambavyo nakuwa comfortable kuzunguka nacho.

"Hata wakiona nimevaa cheni inakuwa gumzo, hata nikivaa kitambaa inakuwa gumzo."

Chanzo: Mwamposa Live
Ohooo
 
Huyu jamaa akienda mkoa fulani wanaopona wanatoka wilayani tu yani vijijini akienda vijijini wanaopona wale wanaotoka mjini
Hii ya viwete kupona mimi mwenyew inanishangaza viwete wanaofahamika huwa hawaponi ila wale ambao huwajui ndo unakuta maelfu wamepona
 
Mwamposa tapeli TU,
1. Kwañn viwete anaoponyesha kwny mikutano yake wote wageni eneo la mkutano, hamna hata mwenyeji mmoja[emoji2]
2. Viwete wanaoponyeshwa ulemavu,
wote magongo yao Huwa Ni mapya kabisa brand new. Huwa wanapata wapi muda wa kuyaosha yatakate yawe mapya ndo waende kwny mkutano wake[emoji1787]

3. Sijawahi kuskia mwamposa akamwangusha pepo tajiri yoyote yule,
Kwake waanguka mapepo wote Ni maskini TU[emoji38]

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
"Juzi nilikuwa Bungeni na tulikuwa Watumishi wengi tu ila nashangaa Picha zangu tu ndizo zinasambazwa kwa Mabaya. Nikibadilisha Viatu hapa Madhabahuni, nikijifuta Jasho na Kitambaa na Nikivaa Cheni naambiwa Mimi ni Freemasons kwanini?" Amehoji Mtume Wenu Mwamposa.

Chanzo: Tv Channel yake muda huu

Kazi ipo.....!!!!!!

=============

Akizungumza na waumini wake, leo Jumapili Februari 12, 2023, Mwamposa amesema: "Yaani mimi nianze kujibizana na watu kwenye mitandao wanavyosema Mwamposa Freemason, nami niingine kwenye mitandao kuanza kuwajibu kuwa mimi si Freemason, sina muda huo hata kidogo.

"Kila kitu nikifanya inakuwa gumzo, juzi nilikuwa Bungeni, nilifanya ibada kwa Wabunge, nilipotoka pale nashangaa picha zinazagaa kuhusu mimi licha ya kuwa watumishi tulikuwa wengi.

"Hata nikiwa hapa (Kanisani) huwa wanashangaa ninavyobadilisha viatu, nabadilisha kwa kuwa mafuta ninayotembea nayo yakimwagikia kwenye kiatu yanakiharibu, hivyo nafaa viatu ambavyo nakuwa comfortable kuzunguka nacho.

"Hata wakiona nimevaa cheni inakuwa gumzo, hata nikivaa kitambaa inakuwa gumzo."

Chanzo: Mwamposa Live
Kwani Freemasons Wana baya Gani? Hawajui Freemasons.
 
Humu Wanaomlaumu mwamposa unakuta na wao ni chenga tuu , wazinzi , mafisadi , watoaji wa makafara, wezi , wadanganyifu nk ... Kiufupi hakuna wa kumcheka mwenzake ..mwamposa kawazid ujanja ndo mana wanamwandama Sana
 
Sasa mchungaji na cheni wapi kwa wapi?
Hataki kujibizana na watu kivipi sindio ameshawajibu? Hayo mafuta yake nikama maji ya betri mpaka yaharibu viatu? Sasa inakuaje mafuta yakimwagika kwenye kiatu kinaharibika kisha mtu anapewa mafuta hayo alambe?
Hivi TBS wamewahi kuangalia bidhaa za huyo mtumishi?

Mbona anajichanganya
 
Hakuna kitu kina nguvu ya kujibu hoja kama kukaa kimya. Angekaa kimya tu!!
Hata ujumbe huu umeletwa sivyo. Nilimsikiliza.
Alitolea mfano jinsi Mungu akikuweka level flani ukawa juu basi watu watakuangalia wewe, watakusema wewe kwa lolote ufanyalo.
Alijitolea mfano yeye mwenyewe kuwa Mungu kamuweka level ya juu ndio mana gumzo jingi mtaani na yeye alisema hana muda wa kujibu hoja za mitaani mana sio level (kiwango) chake, akifanya hivyo atakuwa amejishusha sana. Cha ajabu mleta mada kaigeuza hoja kaileta hapa kama amewajibu hao wamsemao mtaani.
 
Ila jamani wale wajenzi huru kujiunga umoja wao sio kitu rahisi kama tunavyoropakaga mitaani.
Semeni labda kama yuko kwenye kundi lingine ila sio lile la WAJENZI HURU.
 
Back
Top Bottom