Mwamposa: Mimi siyo Freemasons na sijui kwanini naandamwa na kusingiziwa vingi

Humu Wanaomlaumu mwamposa unakuta na wao ni chenga tuu , wazinzi , mafisadi , watoaji wa makafara, wezi , wadanganyifu nk ... Kiufupi hakuna wa kumcheka mwenzake ..mwamposa kawazid ujanja ndo mana wanamwandama Sana
Na wasi wasi huenda hata maana ya ujanja hujui.
 
Jamaa anawapiga pumbazo waumini kisha anawaseti 🤣🤣🤣 kila mtu akitoka anamuona jamaa ana superpowers.
 
Ha ha ha...mi mwnyw Huwa nawaza TU,
Siku maisha yakinipiga naenda Nigeria nachukua uchawi, naanzisha kanisa[emoji4]
Katibu nipo hapa usiniache 🤣🤣🤣 inahitajika dawa ya kupumbaza umati tu.😀😀😀
 
Hii ya viwete kupona mimi mwenyew inanishangaza viwete wanaofahamika huwa hawaponi ila wale ambao huwajui ndo unakuta maelfu wamepona
Sasa sio viwete tu magumashi, hata hayo mengine ni magumashi hivo hivo, sema tu kuna wengine wankua wepes kugundua kama ww, ila wengine ni wagumu sana vichwa vigumu hata uwadhihirishie laiv bado watamuamini tu. Na si ajabu. Na wala sio mageni.
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Kuhani wa. Mchongo
 
Naona unatangaza kabiashara kintindo kintindo kintindo!!!!! Hahahaha
 
Kikubwa analipa kodi🤝🤝🤝🤝
Ni wivu tuu sababu anamake money , Mimi kwenye hzi dini ni mzoefu Sana , asikwambie mtu wachungaji wa madhehebu yote Wana njaa Kali Sana na wana uchu wa pesa Acha kabisa , ni kweli mwamba ana mauza uza kibao Ila hata hao wanaomponda hawana unafuu wwte ni wasanii tuu kama yeye sema Ile popularity ya jamaa na kumake mkwanja ndo inawaumiza kichwa wameamua kumsagia kunguni ..... Ndo mana wale wahuni walipotaka kumpiga mawe mariamu kisa wamemfumania Yesu aliwaambia asiye na dhambi awe wa Kwanza kumpiga jiwe , watu ni wepesi wa kuhukumu ya wengine Ila Yao yakifunuliwa mbna tunakimbiana , Yesu aliandika dhambi za kila mmoja wao pale chini , ndani ya nusu saa wakachora wote

Tunapomhukumu mwamposa inabd na sie tujitafakari njia zetu....!! Na ni ukweli mtupu madhehebu ni biashara za watu
 
Mwamposa yeye anafanya biashara ya mafuta , nguvu anayoutumia Siri anaijua mwenyewe , Ila anachoamini shida yyte uliyo nayo itatatuliwa na mafuta, yeye hatambui shida za watu ingekuwa hvyo asingekwambia uandike means anakubali Hana uwezo wa kujua shida za watu , Ila yeye anachojua ni kuwa mafuta yake yatakuponya na kukusaidia shida zako ... Nguvu ya hayo mafuta kwamba ni ya Shetani au ya Mungu yeye ndo anajua...
 
Huyu tapeli Mwamposa anaona watu mambwiga kweli. Anaibia watu mchana kweupe na hawamshtukii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…