Pole sana Mbumbumbu wa karne hii na ambaye huwezi thibitisha juu ya mambo ya Imani na unaanza kutunga stori zako. Hivi huwa Uoni zile Imani zingine zinafunga kabisa barabara na kuweka matent barabarani mpaka Wiki njoo hapo Ilala,Magomeni Tandika mbona hujawahi jadili jambo hilo au Huyu Mchungaji amekukera kwa Watu kufurika kwake .Kama unajua zilipo dawa anazogawa basi usipate tabu najua hata wewe pesa unazihitaji kachukue hizo dawa anzisha ibada nao watakuja .
Mtu mwenye wafuasi wengi vile wenye elimu na nguvu za kiuchumi tena wengine wenye Mamlaka makubwa ndani na nje ya hii nchi wanakwenda kumsikiliza yeye jua wazi pale kuna jambo si kawaida ukipata fursa nenda kachunguze vizuri ili usiropoke na kuonekana huna akili.
Ebu fikiri kampuni ya Abood bus service inapeleka magari 10+ yanapark pale kutokea huko mikoani inasubiria abiria iliowaleta kutokea mikoani ,Hotel za maeneo ya Kawe,Mbezi,Tegeta,Kunduchi zimejaa waamini wake ili wahudhurie ibada,Tax,Boda,Bajaji,Daladala wanapata fursa ya kupata abiria,Television karibu tano zinapata Matangazo yake,Wafanyabiashara ndogondogo wanapata wateja,Watu walioajiriwa kwake ni wengi.Yaani wewe Mbumbumbu badala ya kuona utajiri na neema ya fursa anazoleta huyo Mchungaji wewe unaona kero tu.Roho ya kimaskini inakutafuna sana.Huu muda nilitegemea kuwa unazo Bajaji pale zinapiga hela,Unacho kigest pale Watu wanalala ,Unao mgahawa pale Watu wanakula, Eti umekuja hapa inalalamika Uzio ambao unajengeka Fasta tu wakati huo serikali imeshakusanya kodi kwenye Hotel,vyombo vya usafiri, na imesaidiwa kupunguza tatizo la ajira. Amka toka shimoni.
Ukiona Mtu anawafuasi wengi Mtazame kwa jicho la tatu Mtu wa kawaida hawezi kuwa na Ushawishi vile.