Tayari refa kafunguka na ametusaidia pakubwa sana pale anaposema there is always mistakes in football, hapo amekiri kuna makosa yalifanyika sasa tumepiga hatua moja kudai haki yetu ya mabilioni ya kuingia nusu fainali. Refa aseme ni mistake gani amemaanisha maana kuna mistakes za maksudi na bahati mbaya, refa akabwe zaidi koo akizidiwa atamwaga mboga na tupambane VAR room officials tuwapate majina tuwafuate kwenye pages zao tukawacharue na wao hadi ukweli ujulikane na Africa nzima wajue bongo hatukubali kuonewa!!
Yanga sasa tukomae na mwamuzi kutafuta jina la officer alietoa maamuzi VAR room ni nani na mpaka anakataa goli ataje alitumia vigezo gani na atuambie kwa nini VAR room hawakuchora mstari kwenye mpira au kuonesha watazamaji sababu ya kukataa goli , Manara amrudie tena mwamuzi ataje jina la alietoa maamuzi VAR kesi ianze upya!
Yaani hapa ndo kumekucha wanayanga hatutakiwi kukubali kurudishwa nyuma kisoka maisha ni vita na soka ni ajira na huleta utajiri na furaha kwa nchi, Yanga tukomae sasa na VAR room officials wa mechi hadi wafunguke, hii itasaidia kuhalalisha madai yetu ya match fixing pale na wao wakianza kujichanganya kama refa ambae hajasema ni goli au sio goli maana hata yeye hana jibu baada ya kuona ngoma imedundia ndani laivu na hakukuwa na sababu ya VAR kukataa goli!!
Nchi nyingi zinaonea wabongo this time tuwaoneshe our true colours kuwa hatuonewi na hatukimbii kesi. Tuwapuuze wanasimba wanaotubeza tunaposaka haki yetu hawa mbumbumbu mfupa wa robo fainali hawauwezi.
Dalili za ushindi ndio zimeanza kwa refa kufunguka sasa wanayanga tukomae na wengine VAR room nao wafunguke na kwakuwa wameanza kuweweseka tutaujua ukweli siku si nyingi. Refa atuambie vigezo VAR room walivyomwambia kuwa sio goli!!
Barua ya Yanga kwa CAF imesaidia sana mechi mbili za robo fainali zilizobaki jana niliziangalia na zilichezeshwa kwa haki na wenye msuli TP Mazembe na Waarabu kupita! Hongera sana uongozi wa Yanga, daima mbele, nyuma mwiko.
Ahsante Sana Bugatti