Mkuu
johnthebaptist, japo kwa sasa mimi ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, lakini ni mwana CCM wa siasa safi na sio siasa za majitaka!. Huyo dogo ni msaka fursa tu, ili kuonyeshea Chadema ni chama cha wauwaji!. Matukio yote matatu aliyoyataja, kwanza yametokea kwa bahati mbaya, na yote walifyatua risasi ni polisi wetu!
Anataka kujenga hoja kuwa, vifo vile vilipangwa na Chadema na zile risasi zimefyatuliwa na Chadema!. Next step atazungumzia mipango ya Wangwe, na shambulio la Lissu!.
Nakiomba sana kwa dhati chama changu kisiwape airtime vichaa hawa!. CCM itashinda uchaguzi huu majimbo yote na kata zote, kwa track record ya kazi nzuri iliyofanywa na JPM na awamu ya tano, CCM hatuhitaji kutumia siasa za majitaka ili kushinda uchaguzi ili hali uchaguzi huu tumeishashinda siku nyingi, ile tarehe 28, ni kwenda tu kukamilishwa kwa taratibu na kuthibitisha ushindi mnono wa kishindo.
Hawa vichaa wa Chadema wapokelewe yes, lakini wasipewe air time. Na kama hayo aliyoyasema ni kweli, then sehemu stahiki alikopaswa kuwa ni Keko, Ukonga au Segerea na sio kwenye mkutano wa kampeni!.
P