Mwana FA & AY acheni utapeli, hamna miziki yenye thamani ya Bilioni 2.1, Tigo gomeni

Heri mleta uzi ameonyesha roho yake ya kutu na kutoa la moyoni maana wachawi wengi sana sema wengine wanakuja na gia ya kupongeza huku moyoni wanawaza kama mleta uzi.

Ukiiba idea au kazi yoyote ya mtu ikakuingizia kipato mwenye mali ana haki ya kutamka chochote anachodhani ndo thamani ya kazi...je Tigo wameingiza kiasi gani mpaka sasa kutokana na wizi huo?
 

ni kweli kabisa wasanii hawa hawana mziki wa bil 2 ila naomba unambie tigo ina wateja wangapi hapa bongo? imepata kiasi gani baada ya kutumia nyimbo za wasanii hawa?na kwanini tigo watumie jasho la wasanii hawa kwa wizi?
 
Ndugu yangu duniani kuna watu wa ajabu sana....Tigo wasingetumia kama kungekuwa hakuna faida kwao!!...Jamaa ameumia sana, nimeshindwa hata kuelewa kinachomuuma ni nini, Tigo wanadaiwa, anakuja mtu kutoa povu huku JF sasa hii inaonyesha wabongo hatupendi maaendeleo ya wenzetu....
 
ni kweli kabisa wasanii hawa hawana mziki wa bil 2 ila naomba unambie tigo ina wateja wangapi hapa bongo? imepata kiasi gani baada ya kutumia nyimbo za wasanii hawa?na kwanini tigo watumie jasho la wasanii hawa kwa wizi?
Na wewe unatakiwa kujiuliza kwanini Tigo wamechukua kazi za wasanii hao bila idhini? au unadhani walistahili kulipwa ngapi?......huwezi kujiuliza kwanini mtu akivunja na kuiba hata kama ni kitasa cha 60,000 na kuiba radio ya 15,000 anachezea mvua za kutosha (je kifungo ni sawa na mali iliyoibiwa).......hiyo inaitwa hukumu waliopewa Tigo inaitwa "iwe mfano kwa wengine wanaoiba kazi za wasanii"
 
Kuna hali flani ya watu wasiokuwa na fedha kuwachukia wenye fedha yaani mtu anataka yeye apate ama ukipata wewe angalau na yeye pia awe ni miongoni mwa waliopata...jamaa wivu tu ndo unamsumbua
 
Mtoa mada una mahaba na tigo sio kwa kutokwa povu hili.. ivi unajua tigo wametengeneza sh ngapi kupitia izo nyimbo..?
 
Ndio kizungumkuti cha fidia hicho mtu anatamka tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Yaani unaangalia thamani ya muziki wao sokoni badala ya kuangali thamani ya muziki wao kwa Tigo, yaani kwamba hao Tigo wametengeneza faida kiasi gani kutokana na muziki huo!!

Kama hujui sheria inavofanya kazi kaa kimya...

Kwa maelezo yako unataka wadau hiyo hela so kwa kuangali faida iliyotengenezwa kupitia muziki wao bali wadau hiyo hela kwa kuangali muziki wao uliuza kiasi gani sokoni walipotoa wimbo wao kitu ambacho hakihusiani na Tigo!!!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuimba hujui lakini unajua kuthaminisha bei za nyimbo za wengine.
 

ni sawa kabisa,acha walipe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…