Mwana J.F..Unakula Tsh.ngapi kwa siku?

Buku 5 kwa familia ya watu wa 4! Hatari sana
 
Ndio napanga ratiba hivyo!


Haha umenikumbusha zamani wakati tupo wadogo nyumbani tulikuwa na ratiba ya msosi aisee..

Nakumbuka tu jumapili ilikuwa Pilau...au mom's special meal!! atakachojisikia mama kupika...good old days za ratiba.

Ila siku za makande usiombe uwe nyumbani...maana hakuna kutoka, saa tisa uwashe mkaa na kubandika makande yako kila saa kuongeza maji hata kucheza huwezi kwenda!!!
 
Hahaaaaa!! Nilivyokuwa napenda kucheza makande na maharage niliunguza sana.

Akina mama sijui kwanini huwa wanapika vyakula wanavyopenda wao,ukiona mtoto hali/hapendi chakula fulani jua home kilikuwa hakipikwi.
 
Hahaaaaa!! Nilivyokuwa napenda kucheza makande na maharage niliunguza sana.

Akina mama sijui kwanini huwa wanapika vyakula wanavyopenda wao,ukiona mtoto hali/hapendi chakula fulani jua home kilikuwa hakipikwi.


Kibongobongo unaanzaje kukataa chakula..labda kama ulizaliwa Masaki...au kwa wale wa Moshi Shanty town!

Nakumbuka siku moja nilienda kwa rafiki yangu huko Shanty town. Sasa siku hiyo mama yake lunch kapika wali samaki halafu ka bake queen cakes.

Kwanza dogo anakula kwa pozi maana yule samaki alimla utadhani anaumwa.

Haya kimbembe kikaja kwenye cake, kumbe dogo hapendi (am sure sio alergy!) mayai. Kaonja cake moja akaitema kwenye carpet halafu akaanza kumgombeza mama yake, "Mum don't you know I hate eggs!!! I am alergic to eggs..."

Nilirudi home nikajaribu kufanya hivyo maana mi sipendi ndizi...aisee kipigo nilichokipata niligundua kuna magonjwa mengine sisi wa hali ya kawaida hatustahili kuwa nayo.
 
Asubuhi supu 500 + chapati 400 = 900
Mchana ugali 1000 + maji kandoro 200 = 1200
Jioni ugali 1000 + miguu ya kuku 500= 1500
Viroba 1000 + sigara 500

Jumla 5100.

Hiyo red hapo umetoka nje ya mada...

Mada ni kula siyo kunywa wala kuvuta...

Ndio maana mnafeli mitihani afu mnamsingizia mama Ndalichako wa watu ...
 
Mi niko interested kujua, alivyombwerambwera kula samaki na keki, wewe kama wewe ulichukua hatua gani kuhakikisha chakula hakitupwi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…