Mwana J.F..Unakula Tsh.ngapi kwa siku?

Babu sio kosa langu nilifundishwa kula inajumuisha na kunywa pia
 
Unatumia au unauza mgahawa?
 
Kuna application nyingi sana za ''Expense/Finance Manager'' kwa Android na hata Ios.....Unaweza kutrace hata kwa asilimia ama mgawanyo wa matumizi yako....Binafsi hata ukitaka kujua tarehe 2 Januari mwaka huu nilitumia kiasi gani katika nini nafahamu..Mali bila daftari hupotea bila habari.
 
Asubuhi chai na mayai miwili=1000
Chakula mchana 3000
Chakula jioni=4000
Bia na mengineyo =10000
Total 9000
Hiyo total nimeioata kwa kutumia formula iliyo tumika kujumlisha michango ya kagera.
 


Nilikuwa na shida mbili kwenye hizo apps:

1. Consistency ya kujaza. Yaani kuna siku inafika jioni unaona uvivuuuu unasema nitajaza kesho. Ikifika asubuhi unasahau jana ulifanya nini.

**Hili nadhani ni rahisi kuliepuka nikiamua kuwa serious**

2. Kuna vitu unanunua ambavyo hutamani hata viingie kwenye kumbukumbu hizo ilhali zimekula hela yako. Yani unataka kujidanganya hadi wewe mwenyewe. Sometimes unajipa moyo kuwa nitafanya mishe midweek ili hiyo hela niirudishe isihesabike kama imetumika.

(Mfano wa ukweliukweli ingawa sio mzuri: Ijumaa jioni, umetoka kazini mara sms, "Mentor uko wapi nimekumiss", nyumbani kuna dogo, unaishia kwenda lodge 40,000/-, condoms 5000/- hizi gharama walai sidanganyi sikuwa naziandika ilhali ndizo zinazotumia hela. Au wacha hilo, hata akija ghetto kwako, akiondoka lazima umtoe 50k hivi..sasa nikikaa nikawaza hii hela nayo niiandike kwenye hii app pia unajionea aibu mwenyewe)

Labda hapa mkuu ungenipa ushauri unawezaje (na siongelei hilo tu, huenda wewe kuna jambo huwa unafanya ambalo hulipendi kulifanya lakini ndo hivo limeshatumia expenses...huwa unaliandikaje...au huwa unafanyaje)



Swali la nyongeza:

Mfano nataka kuanzia Mwezi December nianze upya huu utaratatibu. Kuna fedha unazoanza nazo mwezi kwa mfano mshahara (ambao ni fixed income inajulikana kiasi gani) lakini kuna vile visenti senti vilikuwa kwenye suruali, kwenye simu, kabatini, juu ya fridge..etc) hizi pesa nyingine unaanzaje kuziingiza kwenye baseline yako???!


Natanguliza shukrani.
 
upo vizuri [emoji2] [emoji2]
 
Nilikuwa na shida mbili kwenye hizo apps:
1. Consistency ya kujaza. Yaani kuna siku inafika jioni unaona uvivuuuu unasema nitajaza kesho. Ikifika asubuhi unasahau jana ulifanya nini.
**Hili nadhani ni rahisi kuliepuka nikiamua kuwa serious**
Jibu lipo hapo chini..cha msingi ni kutambua jambo hili lina manufaa mengi zaidi,ikiwepo kutambua mapato na matumizi yako,wapi pesa inatumika zaidi,wapi pa kutilia mkazo.Ni commitment na discipline,overtime,utaona umuhimu wake, ni kitu ambacho hutataka kumiss kukifanya kama sehemu ya utaratibu wako.

tena hivi usivyotamani viingie ndio vizuri hasa viwepo kwenye record maana katika evaluation yako huko mbeleni vitakusaidia kupanga mikakati madhubuti ya jinsi ya kudeal navyo..Chochote kinacho affect pato lako kwa wakati huo lazima urecord tu.Kuna vitu vingine ni kanuni za kihasibu/mahesabu na si tutakavyosisi.Kutambua kipi na wakati gani haya ni matumizi ama mapato ni kanuni za kihasibu.

Mfano wako ni mzuri hata mimi kwa namna moja ama nyingine nakuwa embarrased kurecord baadhi ya mambo....Hata hivyo hakuna namna I have to be true to myself na nifuate taratibu za kihasibu.Kwa kuwa hii ni personal Finance basi mimi ndio kama ''mkaguzi'' wa hayo matumizi na mapato yangu.Mwisho wa siku nafanya hivi kwa manufaa yangu..Kitu pekee nachoweza kufanya katika jambo naloliona ''embarrasing'' ni kulirecord kwa ''lugha ya kujifariji'' lakini bila kuharibu ama lengo la hela ilivyotumika..Mfano Wako unaweza ukadescibe gharama kama ''Night Out Expenses with XYZ''....

Labda hapa mkuu ungenipa ushauri unawezaje (na siongelei hilo tu, huenda wewe kuna jambo huwa unafanya ambalo hulipendi kulifanya lakini ndo hivo limeshatumia expenses...huwa unaliandikaje...au huwa unafanyaje)
nadhani nimejibu hapo juu..Kiukweli the moment nilipoamua kutumia hii app nilikuwa nimeshakubaliana kufuata kanuni na taratibu za kutambua mapato na matumizi yangu....Kitu pekee kwa sasa ambacho si hakiingii kwenye record ni pale ninaposahau.Unajua kama binadamu si kila kitu utakikumbuka hasa unaporecord siku inapoisha ama zimepita sku kadhaa.Kuna zile petty expenses kama upo njiani umeombwa TZS 100,Au umenunua pipi ya TZS 50,Unaweza ukajisahau kabisa hata usiikumbuke.

Haijalishi unaanza lini,Kwa kuwa kuna vyanzo mbalimbali vya mapato,bado huna budi kukeep track ya record zote..Kumbuka hela unayopata kwa namna yoyote bado itapelekwa kama si kwenye savings basi ni matumizi.Uzuri hizi apps zinatambua vyanzo vya mbalimbali vya mapato,ni suala la kucategorize tu...Kiukweli unaweza kuona inachosha na haina maana,lakini ipe muda utaona kumbe ni jambo zuri na linakujengea discipline ya pesa yako..
 
Hahaaaaaa!!! Yaani nimecheka kwa nguvu.
We uliwahi kuona wapi mtoto wa mwenzangu na mie ana aleji na chakula fulani!!!

Niliwahi kujifanya sili dagaa(nilikuwa sizipendi) mama alifululiza kuzipika akiniambia nione kama utakufa, aisee mpaka nikazipenda.
 
Nimepata somo, shukrani mkuu.
 
Sijuw huwa sifany hesabu mana nikitoka kazini nakuwa namkoba wapesa matumizi yangu mabaya sanaa ;kuanzia laki kwa siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…