Hahaha weekend ni shida kwa kweli..hapo ndo unapotamani uwe umeoa maana kupika unaona uvivu na njaa unasikia, unaishia kwenda kula chakula hata hushibi ila ghali!
Yani mimi huwa napanga kabisa..asubuhi nikiamka nitachemsha samaki ninywe supu na chapati, baada ya hapo samaki wawili nitawaunga vizuri nitengeneze mchuzi wa kutosha lunch na jioni.
Labda najisemea leo nitapika wali kwenye rice cooker wa kutosha mchana na jioni. Nikitoka gharama ni vinywaji tu tena mimi hata vilevi situmii so kichwani bajeti ni ndogo mno.
Subiri uamke sasa...mara
RRONDO amekupitia mnaenda kunywa mtori Liquid kule Kigamboni...ukirudi hapo umechoka na uvivu juu wala samaki huwakumbuki..unaishia kwenda kula nje the rest of the day!!! Tena usiombe hiyo siku kuwe na games jioni ndo kabisaaa jiko litakusikia tu kwa jirani...weekends ni mbaya sana aisee kwa mifuko ya bachelors wengi!!!