TANZIA Mwana JamiiForums Miguu ya Kuku/ Mpauko afariki dunia

Baada ya kuona msalaba sasa ndio nmeamini inasikitisha sana ulijitahidi kutukutanisha pamoja wenye tatizo kama lako ili tusijisikie wapweke na tusione tatizo ni letu pekee na tupo wengi kumbe wewe nia ya kujiua ulikuwa nayo bado daah tulikuwa hatuna kitu ila tulijitahidi kufalijiana umekuwa daraja kwetu mimi na mwenzangu maana wewe ndiye uliyetuunganisha tulikuwa hatuna kitu ila tulifarijiana kwia matatizo yetu na kukabiliana na changamoto zetu pumzika kwa amani
 
Nakumbuka alini pm akikuulizia kama nakufahamu, akadai yanatakiwa majina yako ili akamilishe muamala, na haupatikani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi nimemuelewa hoja yake, wewe utakua na shida sio bure.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Well said my dear, Mungu atusamehe na kutuhurumia
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekusoma sana,nimekuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilianza kumfahamu kupitia uzi ule na niliusoma a-z nikaelewa dhamira ya ndani ya mleta uzi na nilijua hatanii japo uwasilishaji wake ni kama masihara.

Nilimfuata PM straight, sasa ya huko PM tuyaache, ila huku ndani kuna watu wana roho zilizopungukiwa ubinadamu. Tupendane ndugu zangu, kejeli na ndugu yake madharau, nk sio fungu letu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni mhanga mkubwa wa hili... Nisingekuwa imara ningepata tabu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Jr we angalau una silaha. Si unaweza kuwaroga tu ukamaliza mchezo asubuhi na mapema?

Kuanzia sasa nategemea mods watakuwa proactive kidogo. Itakuwa poa sana na JF pataanza kuwa mahali salama. Kuna sababu akina Zuckerberg wanatumia mamilioni ya dola kupambana na bullying kwenye mitandao yao kwa sababu wanajua madhara yake ni makubwa; na wenyewe wanaweza kuwa liable.
 
Ni kweli. Na inavyoonekana marehemu alikuwa na mawasiliano na watu wengi sana huko PM na wengi wao walijaribu kumsaidia kwa kadri walivyoweza. Ni wazi alikuwa amedhamiria kweli kujitoa uhai; na msaada wa kitaalamu kisaikolojia pengine ndiyo ungeweza kusaidia.

Wote waliojaribu kumsaidia na wale ambao walipuuzia maombi yake najua sasa wanajisikia vibaya sana. Hii ni hali ya kawaida. Sense of guilty. Pengine ningefanya hiki au kile marehemu asingejiua. Ukweli hata hivyo ni kwamba mtu akishafikia hatua ya kukata tamaa na akaamua kabisa kabisa kujiua hata wangefanya nini angejiua tu. Labda tiba ya wataalamu wa magonjwa ya akili na watu wa saikolojia ndivyo vingeweza kumletea ahueni.

Wote hawa wanaojilaumu wakae wakijua kuwa siyo kosa lao kuwa marehemu aliamua kujiua pamoja na jitihada zao zote zilizofanya mpaka ada yake ikalipwa, vyeti vyake vikaachiliwa na ahadi ya kazi akapata. Wamshukuru Mungu kwa moyo wao mwema na wasonge mbele. Tukio hili basi liwaachie alama chanya katika mioyo yao kuhusu maisha, upendo, wema na ubinadamu. Mungu Ataponya majeraha yao. Marehemu Alale salama [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
@maxence melo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi mwenyewe nimehudhuria sana pale CCBRT Msasani lakini naona kama nimepoteza hela yangu tu.
Yaani kila ikifika leo, ya jana afadhali.
Tatizo kila siku linakuwa.
Udogoni nilikuwa nasikia fresh tu.
Ila navyozidi kukua ndio tatizo linapanuka.
Hakuna hata ndugu mmoja anayenipigia simu zaidi ya kuchati kupitia sms.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana. Hosp wanasema shida ni nini? Ulishajaribu tiba kwa njia ya mitishamba? Pole sana...nakutia moyo mkuu, usije ukakata tamaa. Mungu akuinue kwa upendo mkuu nawe uione asubuhi yako ikiwa njema na yenye kusikia kila jambo! Jipe moyo, tuko pamoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…