Uhai mwingine umetutoka.. Ni wa mwana JF mwenzetu...
Mpauko! Apumzike kwa amani... Nimepitia mada ya tangazo la kifo chake na mada zake nyingine nyingi... Nimeona sononi na majuto katikati ya maandishi ya wengi
Majuto ya kukejeli
Majuto ya kutochukua hatua kwa wakati sahihi
Majuto ya kuchukulia mizaha
Majuto ya kuupuuzia...
Nina hakika hata viongozi wa JF nao wanajuta kwa namna moja au nyingine.. Pengine kwa kutojali na kuweka barrier kubwa kati yao na wateja wao (wanachama) labda wakiwa busy zaidi na kusajili wanachama wapya, kurekebisha nyuzi, kuzifungia, kuzihamisha kuziondoa na kutoa adhabu
Kuna moja lilipaswa kuwepo na pengine limepuuziwa MAWASILIANO kati ya viongozi na wanachama na sio hivi ilivyo sasa.. Uhafifu mkubwa wa mawasiliano
Kuna sababu kubwa na muhimu sana kwanini watu wanakimbilia JF kama sehemu sahihi ya kusaidika kiroho na kimwili.. Slogans za HOME OF GREAT THINKERS.. where we dare to talk openly, zimewavutia wengi wakubwa kwa wadogo na watu wa kaliba zote kwenye jamii
Mpauko ameondoka.. Hatuishi milele! Lakini je pale alipodhani ni kimbilio sahihi hakujutia kwa aliyokutana nayo? Je wewe u mmoja wao waliomkebehi na kumkejeli au ni mmojawapo uliyempa faraja, tumaini na kumtia moyo?
Tuna ombwe kubwa sana kwenye jamii yetu.. Tumekuwa busy na ya kimwili kuliko ya kiroho... Ya kiroho tumewaachia watu wa dini tukidhani kuwa ni watu sahihi.. Lakini tunasahau kuwa ya kiroho ni zaidi ya mahubiri na mawaidha kwenye masinagogi.. Kule kuna vigezo masharti, mipaka na taratibu... Sio sehemu za kuongea kwa uwazi
Jamii haina muda na wanajamii... Habari mbaya ndio huwa habari kubwa kuliko habari njema! Kushindwa kwa wengine ndio mashangilio na furaha ya wengine..
Wazazi hawana muda na watoto
Mke hana muda na mume
Mume hana muda na mke
Ndugu hawana muda na ndugu
Hakuna mawasiliano ya kifamilia, hakuna mawasiliano ya kikaya hakuna mawasiliano ya kijamii ni kila mmoja na lwake.. Yanafanyika yale ya kimwili tuu tena kwa mipaka na yanayoonekana ni muhimu
Watu hawana pa kukimbilia.. Huko mitandaoni ni ujinga mtupu... Misaada na ushauri unaoombwa ni vituko tupu.. Mtu anaomba ushauri uliojaa mizaha na porojo... Watu wakikimbilia nyumba za imani huko nako kuna yake.. Hakuna cha bure
JF imeonekana kama sehemu sahihi... Je tunalitambua hili? Maombi yameshatolewa mara kadhaa kuwa kwenye maboresho walau liwepo jukwaa la misaada ushauri na kutiana moyo! Misaada si lazima iwe pesa la hasha.. Lakini liwepo jukwaa maalumu kwa mambo hayo...
Natambua mtanziko uliopo kati yetu kwakuwa ni vigumu kumjua nani mkweli nani muongo.. Nani mhitaji wa kweli na nani mzugaji... Tumeshatapeliwa sana hapa kwa kudhani tunasaidia penye tatizo la kweli kumbe hamna kitu... Lakini hii yote imetokana na sisi kudili na mwili zaidi kuliko roho...
Tunahitaji kuwa na jukwaa la kiroho lenye dhima ya kutoa misaada na ushauri wa mambo magumu wanayokutana nayo watu.. Tusiwe busy tu na majukwaa mengine.. Sasa hivi kejeli ni nyingi kwakuwa hakuna jukwaa maalumu la haya mambo... Hatujachelewa bado tunaweza kufanya hata sasa
Mwisho nilikuwa na mawasiliano ya karibu na marehemu
Mpauko mwalimu aliyekuwa na tatizo la uziwi... Kwenye kujitambulisha kwangu aliwataja wana JF wawili kama reference
Avriel na @manengelo
Kuepuka majuto mengine tusiwadharau na kuwakejeli tena wale wote wanaokuja na shida mbalimbali hapa.. Kama hutoweza kutoa hata neno la faraja basi at least usikejeli... HUJAFA HUJAUMBIKA... Na ya kesho huyajui
Hii barua yake ya kuomba msaada nadhani wengi mnaikumbuka
Sent using
Jamii Forums mobile app