Mshana Jr,
Mimi niliwahi kuandika huu uzi.....
Wengi wao humu JF inakuwa porojo tu kuchangamsha baraza. Si kweli ya kuwa wanataka kujifupisha Maisha yao
www.jamiiforums.com
Nimeandika thread hii baada ya kuona ongezeko la thread za members wa JF wakitishia au wakitoa thread zenye mawazo ya muelekeo wa kujiua/ kukata tamaa ya maisha.
Pia, naelewa kuwa hiki nitakachosema kinaweza kisiwe kilifikiriwa mwanzoni na waanzishaji wa JF. Lakini ni kitu kizuri kama watafiikiria kukifanya.
Kwa social medias za nchi za wenzetu, kwa mfano Facebook, wana njia ambazo mtumiaji wa Facebook anaweza kuripoti post ambayo imekaa kiuelekeo wa mtu kuwa na suicidal thoughts, then kuna taratibu wanafanya nadhani kupitia 'hot lines' kwa wataalamu wa saikolojia kuweza kuwasiliana na mhusika na kumpa msaada wa counselling (sifahamu the exact procedure wanafanyeje, lakini najua kuna kitu wanafanya kwa watu wanaopost post za aina hiyo).
Sasa challenge kwa waanzilishi wa JF, je, hawaoni kama kuna umuhimu pia wa kuweza kuweka mechanism ya aina hiyo? Watu ambao wanapost thread za kutaka kujiua au kukata tamaa ya maisha, post zao zinakua identified, na ID zao, then wanakua contacted (na wanasaikolojia) kwa maongezi kupitia PM... kama wakiafiki na wakawa tayari kutoa mawasiliano yao ya simu, wanaweza kufikiwa pia kwa njia ya simu kwa kupigiwa kupitia a 'hot line' ambayo itakua imekua established.
Hii inaweza kusaidia sana pia hata wale wenye msongo wa mawazo tu na matatizo ya kisaikolojia (wako wengi sana humu, kwa kuangalia tu post watu wengi wametingwa sana, vichwa vyao vimejaa misongo).
JF inaweza ikawa link ya muhimu kati ya hawa watu na wanasaikolojia kupitia utaratibu maalum ambao utaruhusu anonymity ya mtu kuwa preserved if they wish so.
Kama waanzilishi wa JF mtakuwa tayari, mimi niko tayari kuandika a write-up ya kuombea fund hii idea BURE KABISA, ambayo mnaweza kuipeleka kwa potential NGOs ambazo ziko interested na mental and social health they might be interested.
Au, mnaweza kufanya hata kama ni kwa scope kidogo kwanza kwa kadri ya uwezo wenu bila kuhitaji a lot of funds.
What do you think guys?
Maxence Melo Moderator Invisible
Ila wadau wengi hawakunielewa kabisa, na wengine walinituhumu nina multiple IDs, natafuta kiki.
Nadhani ni muda wa kufanya kitu sasa.
Mshana Jr