Wale wenzetu wanaokujaga huku kuomba msaada wa ada mfano @najanaja tukiwa nacho tuwasaidie kama hatuna tusiwaseme vibaya (wamekuwa wakitolewa maneno makali wengine wanadiriki kusema wasiombe watafumuliwa marinda).
Hauwezi kujua huo msaada wako anauhitaji kiasi gani na pengine ungemuokoa na maamuzi ya kujiua au hayo maneno yako ya kejeli yangempelekea ajione si kitu aamue kujiua.
Watu wengi wanaojiua ni mapenzi au hali ngumu za maisha. Tujifunze kumsaidia mtu akiwa hai. Sio hadi afe ndio tuanze kusema "hata mimi alinifuata pm ningejua ningemsaidia, au hata Mimi niliona Uzi wake nikajua ni utani.".
Ni kweli wengine wanaomba misaada wakiwa wana nia mbaya na wengine ni kweli ana shida. Ukibarikiwa moyoni saidia na usipobarikiwa kumsaidia epuka kumtolea maneno ya kejeli.
Leo kuna watu wakisikia Najanaja kajinyonga kwa sababu alishindwa kuendelea na masomo na hata biashara alizotamani kufanya alikosa mtaji, watu wataishia kusema " ningejua ningemsaidia". Kama upo kwenye nafasi ya kumsaidia mtu msaidie usisubiri afe ujilaumu.
NB. Kuna watu pia watasema Mimi ni Naja naja.
Sent using
Jamii Forums mobile app