TANZIA Mwana JamiiForums mkongwe, Dena Amsi afariki dunia



Mimi sio Mswahili mwenzenu, mwenzenu wewe na nani? Jiongelee mwenyewe! Usibane wigo wa msiba kwamba ni wako wewe Mswahili tu!

Halafu wewe huwezi kutathmini ufasaha wa Kiswahili ninachoandika mimi na kunipa sifa, kwa sababu wewe mwenyewe chako kimepinda! Lakini hiyo si mada ya leo.

Unasema msibani watu hujua legacy ya marehemu kwa kupiga soga hapa na pale, kwa hiyo kumbe "legacy ya marehemu" kitu hicho kipo na hujulikana, hata misiba ya Kiswahili.

Sasa hapa kuna kurasa zaenda hamsini tumejaza marudio ya RIP Dena Amsi, Inna Lillahi wa Inna, Bwana amempenda zaidi kamuua, pole sana tunakukumbaka... tunakukumbuka kwa lipi? Hakuna anaejua!

Halafu kwenye misiba, iwe ya Kiswahili au ya Ki-Spanish, kuna mtu anasimama rasmi anamuongelea marehemu kirefu, na wengine husoma eulogy kujaribu kueleza legacy ya marehemu. Usinambie ni kukutana kupiga soga, kupiga mayowe ya vilio, kuzika, kurudi kula ubwabwa, kuondoka! Mswahili wa wapi wewe?

Dunia imebadilika siku hizi, huyu Dena ambae kurasa hamsini hakuna anaemkumbukia kwa lolote tusije kuwa mithili ya waombolezaji wa kukodishwa.

Nafikiri hata wewe ukifa regardless of any legacy utayoiacha tutakuandikia tu RIP upumzike kwa amani simply because ulikuwa MwanaJF mwenzetu


Hapana ahsante, mimi nikifa msijaze kurasa ndeeefu za R.I.P na kariri za Inna Lillahi wa Inna na Bwana ametoa Bwana ametwaa kwa kumpiga limkuki la mdomo kwenye bifu na wafugaji.... no, spare me with the superstitious horse dang please kama hakutakuwa na cha mno nilichokiachia legacy zaidi ya "alikuwa mwanajamii mwenzetu..."
 
Mungu amtendee haki!
Sijui kabisa Siri za Mungu, lakini Kwa mujibu wa maandiko ya Mungu, mtu akifa huhukumiwa papo hapo kulingana na matendo yake.
Neema ya kuiona pepo ipo duniani kabla hatujafa, Kwa maana ya kutengeneza matendo yetu yampendezeshe Mungu.
 
Nenda msibani utaikuta legacy huko.
Maneno mingi ya nini.
 
Mkuu kwanini ukereke kwa kitu ambacho hakikupunguzii chochote kwenye maisha yako ya kila siku!? Haya "makurasa mengi" hapa yanakupunguzia nini wewe!?

Acha hizo Mkuu kama huna la maana la kuandika kufuatia kifo cha huyu mwenzetu pita kimya kimya.

Niende msibani nitazikuta legacy, na nyinyi hizo pole si mkatoe msibani, makurasa mengi hapa ya nini?
 
Tindikali

Imenibidi nicheke tu..!!

Huu mjadala unaweza kwenda na kujirudia rudia yaleyale. Niliyoandika yamejitosheleza mumo kwa humo.
Wewe member wa JF kama Mimi na marehemu japo tuna tofauti ya "Uswahili" wetu. Kama hujatambua
legacy ya marehemu toka kurasa ya kwanza wakati nawe memba pia inawezekana msiba haukuhusu kama nilivyosema
awali.

Hakuna Mtu akafariki na hajaacha legacy. Kwa muktadha wa Dena Amsi ni wale waliomfahamu kupitia mabandiko na mijadala baina yao iwe mizuri au mibaya, ikiwa pia na wale waliokutana ana kwa ana japo mwanzo ni JF.

Utamaliza nguvu zako kutaka legacy unayoweza kuipata humuhumu kupitia mahusiano yake na members tena kupitia pen names na mtiririko wa kurasa kwenye uzi huu wa msiba wake, lah kama unataka kitabu cha legacy yake sina hakika kama kitaandikwa.
 
Unatafuta umaarufu kwa falsafa za kijinga sio?
 
Dah!
Inauma jamani!
Natamani nione picha enzi za uhai wake,nilianza kuona post na comment zake 2011 kama sikosei,nilikuwa msomaji tu kabla sijajiunga humu.
Mungu ampuzishe kwa amani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…