Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na kama nimekusoma vizuri wewe si "Mswahili" mwenzetu.
Sikulaumu, tamaduni zinatofautiana, kwa siye "Waswahili" huwa tunajua legacy ya marehemu tunapoomboleza na kupiga soga hapa na pale. Hatuulizi "legacy" ya marehemu katikati ya waombolezaji, ni adabu mbaya.
Nafikiri hata wewe ukifa regardless of any legacy utayoiacha tutakuandikia tu RIP upumzike kwa amani simply because ulikuwa MwanaJF mwenzetu
Sijui kabisa Siri za Mungu, lakini Kwa mujibu wa maandiko ya Mungu, mtu akifa huhukumiwa papo hapo kulingana na matendo yake.Mungu amtendee haki!
Nenda msibani utaikuta legacy huko.Mimi sio Mswahili mwenzenu, mwenzenu wewe na nani? Jiongelee mwenyewe! Usibane wigo wa msiba kwamba ni wako wewe Mswahili tu!
Halafu wewe huwezi kutathmini ufasaha wa Kiswahili ninachoandika mimi na kunipa sifa, kwa sababu wewe mwenyewe chako kimepinda! Lakini hiyo si mada ya leo.
Unasema msibani watu hujua legacy ya marehemu kwa kupiga soga hapa na pale, kwa hiyo kumbe "legacy ya marehemu" kitu hicho kipo na hujulikana, hata misiba ya Kiswahili.
Sasa hapa kuna kurasa zaenda hamsini tumejaza marudio ya RIP Dena Amsi, Inna Lillahi wa Inna, Bwana amempenda zaidi kamuua, pole sana tunakukumbaka... tunakukumbuka kwa lipi? Hakuna anaejua!
Halafu kwenye misiba, iwe ya Kiswahili au ya Ki-Spanish, kuna mtu anasimama rasmi anamuongelea marehemu kirefu, na wengine husoma eulogy kujaribu kueleza legacy ya marehemu. Usinambie ni kukutana kupiga soga, kupia mayowe ya vilio, kuzika, kurudi kula ubwabwa, kuondoka! Mswahili wa wapi wewe?
Dunia imebadilika siku hizi, huyu Dena Amsi ambae kurasa zaenda hamsini za pole na R.I.P. hakuna anaemkumbukia kwa lolote tusije kuwa mithili ya waombolezaji wa kukodishwa.
Hapana ahsante, mimi nikifa msijaze kurasa ndeeefu za R.I.P na kariri za Inna Lillahi wa Inna na Bwana ametoa Bwana ametwaa kwa kumpiga bisu la mdomo kwenye bifu na wafugaji.... no, spare me with the horse dang please kama hakutakuwa na cha mno nilichokiachia legacy zaidi ya "alikuwa mwanajamii mwenzetu..."
Hapana, hiyo sio picha yake nahisi.Sidhani Mkuu, ila sina uhakika wa 100% Mkuu, kuna mwenzetu alibahatika kukutana naye anaweza kuthibitisha kama hii ni picha yake au la.
CC: Prishaz
Nenda msibani utaikuta legacy huko.
Maneno mingi ya nini.
Niende msibani nitazikuta legacy, na nyinyi hizo pole si mkatoe msibani, makurasa mengi hapa ya nini?
Wewe kinyamkera ulitumwa kuingia kwenye huu Uzi mbona hasira zako huko unahamishia humu , uliitwa kwani .Watu wapo kwenye majonzi unataka kuleta ubunuwasi wako humu.Niende msibani nitazikuta legacy, na nyinyi hizo pole si mkatoe msibani, makurasa mengi hapa ya nini?
Unatafuta umaarufu kwa falsafa za kijinga sio?nimeandika posti mbili ndefu nikianisha swali langu, kama hujanielewa sidhani kama kuna jinsi ya kuiweka vingine.
Legacy ningeiweka kwa muktadha wa nyinyi Waswahili ningeeleweka?
Kwa hiyo huu msiba wawahusu Waswahili tu? Nitaiwekaje legacy kwenye muktadha wa legacy za Kiswahili kama labda mimi sio Mswahili?
Waswahili kuhuzunika msibani ni jambo la kawaida na kama sijahuzunika msiba haunihusu. Kwa hiyo huu ni msiba wa Kiswahili mimi siwezi kuulewa, sio?
Msiba wa Kiswahili ni kwamba hauna mambo ya kueleza kuhusu legacy za marehemu, tunamkumbukia nini marehemu, ni tunalia weee, tunazika, tunakula ubwabwa, tunajaza ma pages ya R.I.P, tuna move forward!
Sawa ndugu, labda sintakaa nikaelewa misiba ya Kiswahili!
Very sadDena Amsi is dead!
Thanks kwa picha mkuuHii ndio picha yake aliekuwa Member mwenzetu....
AMENMungu ampe pumziko LA milele