TANZIA Mwana JamiiForums mkongwe, Dena Amsi afariki dunia

TANZIA Mwana JamiiForums mkongwe, Dena Amsi afariki dunia

Pole sana Afrodenzi na ahsante sana kunitaarifu na kufuatilia kuhusu habari hii. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mwenzetu mahali pema peponi. Mimi kama wewe bado siamini kama Dena Amsi hayuko hai bado niko kwenye mstuko mkubwa.

Nimepigwa na butwaa tangu nipoke hii taarifa.

Dena Amsi, King Mungu igaslaa ne iga amorosiatet. Aten king i-islawan ar muru hho tatlehhit bara-slafing-woge. Umu Mungu i-khirfuti.
(Dena Amsi, wewe Mungu amekupenda na amekuita kwake. Sisi tutakumbuka kwa mazuri uliyoyafanya wakati wa uhai wako, Jina la Mungu litukuzwe)

Kila nikiongea na Dena tunajaribu kuongea Ki nyumbani japokuwa hatukijui kivile.
Ni vema nikimuaga kwa lugha ambayo huwa tunajaribu kuitumia. Kwa kweli sitaki kabisa kuamini hili bado.
 
RIP Dena Amsi, pole familia

Miaka 6 pamoja JF ni mingi sana, tangulia ndugu sisi nyuma yako. Kweli kizuri hakidumu
 
Ni habari za kusikitisha kwa familia ya JamiiForums kwa ujumla wake.

Inadaiwa marehemu Dena Amsi amefariki jana baada ya kuugua kwa siku kadhaa.

Taarifa za kina juu ya nini kilitokea na msiba upo wapi zitafuatia.

Mwenyezi Mungu amsamehe dhambi zake na kumjalia pumziko la milele.

R.I.P Dena Amsi
Poleni sana na Mola ampokee katika mikono yake
"R.I.P Dena"
 
Back
Top Bottom