Mwana JF yupi unamkubali sana na kwanini unamkubali?

Msomee tu. Huyo kanigandisha mi nasubiri tiketi ya kwenda kuuza figo tiketi yangu anayo yeye.
Kwa taarifa nilizopewa figo yako haifai kutolewa, unatumia sana dry gin na una tamaa na MLF + BBW sasa ukitolewa sitaki kulaumiwa niliwahisha ratiba ya Izrael!.
 
Vyema Sana umemkogesha nayo mwili mzima.ungemwadhiri zaidi Kwa kumtaja na jina lake. Vidume vingine vimezidi kuwa na bifu za kishamba na watoto wa kike, online bullying kwa women lazma iishe.
Mimi ni mwanaume ila siiungi mkono uonevu wa wanawake mtandaoni. Period!
 
Sifa hizo za Max umezijuaje mkuu?
Una mfaham nje ya JF?

1. Kesi za Jamiiforums na jinsi alivyoandamwa kwa nguvu kubwa za serikali, kuanzia utawala wa Kikwete mpaka leo,na akapigania uhuru wa kujieleza na faragha za JF mpaka kushinda ni ushahidi kuhusu msimamo wake.

2. Mimi mwenyewe katika mode yangu ya ku criticize JF, nilishawahi kuwasiliana naye na jopo la Moderators wa JF, nikawapa maneno makali sana kuhusiana na JF ilipotoka, ilipo leo na inapoelekea, nikisisitiza kwamba wanaharibu kanuni za msingi za kutunza uhuru wa maoni wa watu hapa JF kwa mtindo wa baadhi ya Mods kufutafuta threads bila mpango na ku ban bila uchunguzi wa kutosha. Kwa kweli niliwasema kwa maneno makali sana ambayo kikawaida kwa wabongo wasio na busara na wenye hamaki, mtu akiwa anaongoza kitu kama JF, ni rahisi sana kukutukana, kukubishia na hata kuku ban kwamba umemvunjia heshima. Aghalabu mtu angeweza kuku ignore kuto acknowledge maoni kabisa.Lakini Max alionesha ukomavu mkubwa sio tu kunijibu, bali pia kukubali makosa na kuahidi kuyafanyia kazi maoni. This points to a mature humility.

3. Nimefanya kazi muhimu za kuetetea uhuru wa habari na maoni Tanzania, tangu misuko suko ya enzi ya Kikwete, katika ngazi za kimataifa, hususan na "Committee To Protect Journalists" ambayo ipo hapa hometown kwangu New York City, katika kumulika uonevu dhidi ya waandishi wa habari na wenye forums kama JF Tanzania. Katika kazi hizi, ili kuhamasisha Jumuiya ya Kimataifa kuingilia uonevu huu. Pamoja na wengine, tume organize media campaign iliyopelekea Rais Kikwete mwenyewe kuwaambia watu wa Usalama wache kuwaingilia viongozi wa JF, kwa sababu kuwaingilia hivyo kunaipa nchi jina baya. Kazi hizi zimenipa kujua mambo yanavyoenda kwa undani zaidi ya kumjua Max huyu wa hapa mtandaoni tu. Na hata hapa naona kama nimesema mengi zaidi kiasi ambacho mwenyewe kwa haiba yake ya ukimya wa kierevu anaweza kuwa hapendi yajulikane sana, kwa hivyo, naomba nisiseme sana, niishie kwa kumnukuu mshairi wangu mmoja wa Kimarekani kati ya ninaowapenda kabisa, Nas.

"There's some ghetto secrets I can't rhyme in this song
There's some missing pieces I had to leave out "

-Nas "Last Real Nigga Alive"
 
Asante kaka.
Kuna baadhi ya wanaume wanaona kila mwanamke mtandaoni yuko kibiashara zaidi.
Kumbe hajui wengine tuko kama chapati.
Unapika A na B.
Sawa hatujawakataza kuja Pm, karibuni sana, ila wekeni mipaka basi.

Afu niwamegee siri, humu Jf ni kama ngoma, mdundo ukianza, akicheza wa kwanza basi mpaka wa mwisho atacheza mdundo huohuo.
Humu tunajuana kitambo....humu kuna Pm zinatembea kama moto wa nyasi.
Kuna baadhi ya shost zangu hata iweje...lazima tutembezeane ushashambe.
Asa kuna nini tena.
Matokeo yake...mtu mzima unakuja kuaibika.

Kaka, ubarikiwe sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…