Uchaguzi 2020 Mwana wa kulitafuta Lijualikali kalipata, baada ya kuangukia pua Ubunge ajaribu udiwani na kuambulia kura 5. Adaiwa kutamani kurudi CHADEMA

Anaomba kurudi wapi? Akae hapohapo labda anaweza kupewa ukatibu tarafa vijijini huko ndanindani
Mteuaji anaweza akakomesha maneno yenu.
Nafasi kumi za kuteua wabunge, akamteua na kumpa ukatibu wa wizara fulani.
Si mnamjua kwa visasi na kupenda sifa?
 
Kwa kuwa alisema yuko tayari kufanya kazi yoyote pale Lumumba bila shaka alijiandaa kisaikolojia

Watakaoteseka wanaodhani atateseka
 
Kumbe ana digrii ya kufuta na kupanga vitabu kabatini?
 
Agombee ubalozi wa nyumba sasa mamaaaeeee na huko atakutana na wajumbe piA!
 
Si awe mwanachama wa kawaida tu
Mbona kuna majamaa zangu wengi tu na mimi nikiwepo tupo tu
Kwani ni lazima uwe mbunge au diwani??
Hawa watu wana shida fulani sio bure
 
Hii ni kweli? Mbona amejipa demotion mwenyewe? Kama kuna mtu kamshauri amemshauri fyongo. Yaani kutoka ubunge, kufightia ubunge kisha kufightia udiwani.

Ila hao wajumbe ni hatari
Mkuu siyo mbaya, biashara ya jumla ikigoma unahamia biashara reja reja.
 
Angojee teuzi, anaweza kupewa hata ukatibu mtendaji.
 
MALIPO NI HAPA HAPA SI ALISEMA BADO ANA NGUVU ATAENDESHA HATA BODABODA AENDE AKAENDESHE SASA, ALIDHANI ANAWAFURAHISHA NZI WA KIJANI KUMBE ANAJIPOTEZA KISIASA. HILI NI FUNDISHO TOSHA KWA WASALITI UNATEMA BIG G KWA KARANGA ZA KUONJESHWA NDICHO KILICHOMKUTA SASA.
 
Alisema bora akalime na kufuga ng'ombe huko Kilombero, nadhani ni muda muafaka wa yeye kuishi katika maneno yake mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…