Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,434
- 27,177
KATIKA UISLAMU mtoto wa nje ya ndoa (mtoto wa zinaa) hana haki ya kurithi mali ya baba yake kibiolojia kwa sababu hakuna uhusiano wa kisheria wa kifamilia kati yao.
Hata hivyo, mtoto huyo anayo haki kamili ya kurithi kwa mama yake mzazi na ukoo wa upande wa mama.
Ingawa hana urithi wa moja kwa moja kwa baba, mtoto huyo anaweza kufaidika na mali ya baba yake kupitia njia zifuatazo kama njia ya wema na usaidizi:-
Soma Pia: Watoto wa ndani ya Ndoa wapewe urithi zaidi ya watoto wa nje ya ndoa
1. Mtoto wa Zinaa, mlipeana mimba hata kama ina wiki mbili ndio mkaoana, huyo mtoto ni wa zinaa, je anapata urithi?

- Zawadi na Hiba: Baba anaruhusiwa kumpa mtoto huyu zawadi (Hiba) wakati wa uhai wake kama ambavyo anaweza kuwapa watu wengine.
- Wosia / Thelutthi: Baba anaweza kumuandikia mtoto huyo wosia akampatia sehemu ya mali yake. Katika Uislamu, wosia hutolewa kwa kuzingatia isizidi theluthi ya mali yote ya marehemu, huku theluthi mbili (2/3) zikibaki kwa ajili ya warithi halali ambo si zao la zinaa.
- Wakfu: Baba anaweza kumwekea mtoto wakfu, kama vile nyumba au shamba, ili mtoto huyo aweze kunufaika na matunda au pato la mali hiyo wakati wa uhai wake
1. Mtoto wa Zinaa, mlipeana mimba hata kama ina wiki mbili ndio mkaoana, huyo mtoto ni wa zinaa, je anapata urithi?