Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Huyu jamaa alifika kazini akawa anajiona yeye ndo yeye. Kazi anaipenda sana kuliko sisi wengine. Basi ikawa kila mfano mzuri boss anamsema yeye. Kila jambo jema mfano yeye.
Jamaa akaanza kupewa pewa safaris nyingi sana. Akawa anapewa bonus kila mara, yaani kiufupi jamaa alianza kupendeza. Akawa anapiga tie, mara suits, anachomekea na siku hizi mnaita Unyakyusa mwingi sana. Nikaliona hili nalo likafikiriwe. Nikawaita wadau kamati ya roho mbaya.
Tukakaa wenyeji, tukajadiliana kuwa huyu dogo mbona kama sisi wenyeji anakosa heshima kwetu. Kaja tunamwona hivi hivi, jamaa mmoja akasema anabonga naye. Akaenda mshtua dogo akajibu yeye si mtu wa majungu kaja kufanya kazi.
Tukarudishiwa taarifa. Basi jamaa mmoja akasema tumpatie pesa fulani atashughulika naye. Akaenda Bagamoyo tu hapo. Wala si mbali.
Yule dogo akaanza kuwa kazini mara haji, akawa anagida sana pombe, anaweza akapotea siku mbili analewa analala bar. Akawa mkorofi kinyama kazini. Mpaka boss anamsemea mbovu. Anasema kwani hii nayo kazi? Basi tu ila yeye si wa kufanya kazi sehemu kama ile.
Tukamwekezea na majungu kinyama, akaharibu ile mbaya pale job. Wakamtimua. Aiseee tulifurahi sana. Tukampongeza fundi wetu kiungo mchezeshaji. Tukabaki wenyewe tu job kwa starehe zetu.
Hizi kazi umekuja umeikuta utaiacha. Usilete kujua saaaaana.watu tumekaa Zanzibar, tumekaa Tanga... tunajua kuishi na watu. Usitake jifanya wewe ndio unafaaanya sana kazi. Mwishowe kazi nayo itakufanya. Muwe mnaheshimu wakubwa. Tunaweza kukufanya kama tulivyomfanya Mashaka Gobwe. Huyu hawezi kutusahau milele... Ishini na watu vizuri.....shauri zenu.