Chakorii
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 18,773
- 51,429
Na wewe utapata faida gani ukishaiona picha ya mtu ambae hana uhai tena?Kwanini haipendezi ? Tayari ameshatangulia mbele za Haki kuna faida gani kuendelea kumbakiza Anonymous ?
Sijawahi kuzoeana na marehemu na wala simjui na si lazima kumjua lakini kitendo cha kuwa mmoja wa wanajf na amekata pumzi tukapata taarifa kwa wakati sahihi basi ni jambo Jema sana na lakumshukuru Mungu.ninajaribu kuwaza kwa mapana sna kesho na keshokutwa sina uhai je atakuwepo mtu wa kuja kuleta taarifa JF kuwa Chakorii hatunae tena na baadhi ya wanajf wakapata muda wa kuja kunizika?au Ndio ID yangu itanyamaza ama kupotea mazima wanajf wakidhani nimebanwa na majukumu ya maisha kumbe nilishakufa kitambo mno..🥺🥺
Inatia simanzi mno..na kama mtu hakumuona akiwa hai itabadilisha nini kumuona akiwa mfu?inafikirisha mno.
Ukijifunza kuvaa viatu vya mtu,hakika kuna baadhi ya mambo lazima uyaache yapite kimya kimya na kuzidi kuomba Rehema ya Mungu.
Maisha haya🥺🥺ona sasa jina limebadilika anaitwa marehemu🥺🥺
Tuzidi kuomba mwisho mwema jamani.
Mwanga wa milele umuangazie warumi apumzike kwa Amani.