TANZIA Mwanachama na mfanyakazi wa JamiiForums, Dotto Mnzava afariki dunia kwa ajali ya pikipiki

TANZIA Mwanachama na mfanyakazi wa JamiiForums, Dotto Mnzava afariki dunia kwa ajali ya pikipiki

Status
Not open for further replies.
Aisee polen amemaliza safari je wewe umejiandaaje kwenda sehwmu salama nawapapole wafiwa faraja ya Mungu ikatawale.mioyoni mwenu...
 
Poleni familia ya doto Mungu ampumzishe kwa amani.
 
Last edited by a moderator:
Poleni wafiwa. Mungu awatie nguvu...Neno la Mungu linasema tushukuru kwa kila jambo. Mhubiri anasema kila jambo na wakati wake...wakati ulikuwa umefika....Tusijiulize maswali mengi maana majibu yake sisi kama wanadamu HATUNA...

ILA kifo cha Dotto kitukumbushe tu wapitaji katika dunia hii...mwenzetu amemaliza safari yake...kesho hatujui ni nani...tutengeneze njia zetu sasa..maana huko mbele......."ni kheri uishi kama Mungu yupo halafu umkute hayupo kuliko uishi kama Mungu hayupo halafu umkute"

Nawapenda na poleni sana kwa msiba huu. Tujitie nguvu...jipe moyo.
 
Heri Maji Jikoni; yachomwapo huchemka
Heri Chakula tumboni; kifikapo huyeyuka!
Heri chozi jichoni, lidondokapo hukauka

Lakini Chozi lishikalo moyo, uchungu wake ni vigumu kuundoa!

Pumzika kwa Amani Dotto Mnzava
 
Last edited by a moderator:
Heri Maji Jikoni; yachomwapo huchemka
Heri Chakula tumboni; kifikapo huyeyuka!
Heri chozi jichoni, lidondokapo hukauka

Lakini Chozi lishikalo moyo, uchungu wake ni vigumu kuundoa!

Pumzika kwa Amani Dotto Mnzava

Maisha ya mwanadamu ni fumbo tata kwakweli... Fikiria ameamka kama kawaida asubuhi akaendelea na shuhuli zake vizuri mpaka mauti yalipomkuta gafla mchana waleo.
 
Last edited by a moderator:
Mwanadamu aliyezaliiwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi nazo zimejaa taabu na shida. Ee bwana utufundishe kuzihesabu siku zetu tujipatie moyo wa hekima. Poleni sana ndugu na jamaa, mke&watoto kama anao. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana libarikiwe.
Inalillah wahina rajuhun!
 
R.I.P-Mpendwa wangu,wetu DOTTO MNZAVA.
KIROHO UPO NASI ILA KIMWILI UMEPOTEA..
AMEN
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom