TANZIA Mwanachama wa JamiiForums (kutoka JF Arusha Wing), Easymutant afariki dunia

TANZIA Mwanachama wa JamiiForums (kutoka JF Arusha Wing), Easymutant afariki dunia

Mkuu tupo kwenye maombolezo haturuhusiwi kucheka, ni uchungu tu au prediction za simu zitakuwa zimefanya akosee
 
WanaJF,
View attachment 1235230
Taarifa nilizozipata ni kwamba, mwenzetu, Easymutant amefariki dunia usiku wa kuamkia Jana kwa ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Sabble Square karibu na uwanja wa ndege wa Kisongo. Msiba upo Olasiti Arusha na updates zaidi nitawaletea hapa.

Poleni sana JF Arusha Wing na Members wore wa JamiiForums kwa ujumla.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.

View attachment 1235020

Updates:

Maziko ni kesho, mwili utachukuliwa Mount Meru Hosp asubuhi saa 4 na kupelekwa nyumbani kwake saa saba mchana na kupelekwa kanisani Kanisa la Mt. Joseph Mfanyakazi, Olasiti.

Maziko yatafanyika kwenye nyumba yake Mateves chini ya kituo cha mafuta cha OilCom Kisongo baada ya ibada.

Michango ya rambirambi inapokelewa na Hortensia Tarimo kwa namba 0759422471. Yeyote atakayeguswa anaweza kutuma rambirambi yake kwa namba hiyo!
Rest Easy [emoji120]
 
Pumzika kwa Amani rafiki yetu kipenzi 😭😭😭😭😭
 
Back
Top Bottom