TANZIA Mwanachama wa JamiiForums (kutoka JF Arusha Wing), Easymutant afariki dunia

RIP
 
Pole kwa wanafamilia ndugu,jamaa na marafiki. We loved you ila Yeye aliye na mamlaka kakupenda zaidi.Pumzika kwa amani mwanafamilia wa JF.
 
Nimelazimika kurudi hapa kwa haraka sana ili kuungana na wenzangu nyote kumlilia mwanaJF mwenzetu Easymutant.

Kifo chake kimekuwa si cha kawaida, maana kimetustua sana. Kwa ufupi hakuna aliyetarajia kuwa jamaa angeondoka katika siku za karibuni.

Arusha Wing tumepata pigo kuu maana huyu jamaa alikuwa ni mchezaji makini sana na alisaidia kutufanya Arusha Wing tuwe vile tunavyojulikana.

Kwasasa tunachofanya ni kumuombea kwa Mungu ili apokelewe salama.
Buriani Easymutant.
 
Mungu awape faraja wote walioguswa Kwa ukaribu kabisa na msiba wa member mwenzetu.
 
Pole sana rafiki,Umenitupa sana.
 
Namllilia ndugu yetu huyu, sikujua id yake humu before,nakiri kuwa alikuwa mwema kwa binadam wenzake, apumzike kwa amani rafiki mwema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…