TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

Hivi jina mgombea wa ubunge wa Lushoto kupitia ccm ni nani?
 
Picha ya gari ndio imeniacha hoi kabisa, hapo ni ilikuwa imeishainuliwa (yaani ili pinduka??) au hivyo hivyo ilivyosimama ndio mtu afe hapo??/ kuna kitu hakiko sawa hapo ...nooooo..
 
Tanzia

Mgombea ubunge wa CHADEMA jimbo la Lushoto Mohamed Mtoi amefariki dunia leo akiwa katika harakati za kampeni jimboni humo mara baada ya gari aliyokuwamo kupata ajari.

Mtoi pia alikuwa mratibu wa kanda maalumu CHADEMA taifa,

Mungu alitoa na sasa ametwaa,jina lake lihidimiwe,Rabuka akulaze pema peponi kamanda Mohamed Mtoi.

Nawapa pole wanaCHADEMA wowote popote pale walipo na watanzania kwa ujumla wake kwa msiba huu mkubwa kabisa.
Taarifa hii imethibitishwa na msemaji wa chama taifa Tumaini Makene😭😭😪😪😪
 
So sad, so sad......Mungu pokea rohyro ya mja wako.......Apumzike kwa amani.
 
JAMANI NAONBA MUELEWE KUWA WAMETOKA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI TARAFA YA MLOLA.

KAMANDA MTOI AKAWAPELEKA WENZAKE MPAKA LUSHOTO MJINI KISHA AKAONDOKA KUELEKEA NYUMBANI KWAKE NDIO NJIANI GARI IKAPATA AJALI NA NDIPO KAMANDA MTOI AKAFARIKI DUNIA.

Maelezo haya nimeyapata kwa katibu wa chama wilaya Kamanda Dulla.
 
Dah it's a very shocking news, too sad, too young, gone soon.... RIP Mtoi, nimemkumbuka Regia Mtema... RIP all Mlale pema peponi
 
R.I.P...Kamanda mudi....aluta continues..... Lowasa mpaka aapishwe..
 
Inna Li Llahi wa Inna Ilayhi Rajiun.

Inasikitisha sana, jana tu nimetoka kumuulizia humu JF. Nilikuwa sijamsikia siku nyingi na siku zote nikimwambia aachane na hao akina Mbowe.

Allah amsameh, amghufirie na amlaze pema peponi.

Wafiwa wote poleni sana tena sana na wana JF wenzetu poleni sana.

Inasikitisha sana.

Mbowe anahusikaje hapo?? We mama ni mchawi kabisa, hii ni Mara ya pili unaandika upuuzi. Mara ya kwanza ni pale mwanafunzi wa chuo cha Makumira alipogongwa na gari ukasema atakuwa amelewa viroba ukapigwa ban kisha leo unarudia uharo wako. Ngoja na wewe afe mwanao au mumeo kisha tuseme tulikwambia achana na CCM ndiyo utafurahi. Pumbavu sana wewe mama.
 
Oh maskini mtoi mama f umemwacha bado watoto wall wadogo walikuwa bado wanakuihitaji kamanda
 
dah! aise hapana sijaamini kiukweli hadi sasa hii si habari nzuri kabisa kuisikia my God Mtoi dah!nimeumia sana kusikia hii habari jamani dah! Eee we Mwenyezi Mungu mpokee mja wako na umpuzishe kwa Amani.Pumzika kwa amani kamanda Mtoi
 
Inna Li Llahi wa Inna Ilayhi Rajiun.

Inasikitisha sana, jana tu nimetoka kumuulizia humu JF. Nilikuwa sijamsikia siku nyingi na siku zote nikimwambia aachane na hao akina Mbowe.

Allah amsameh, amghufirie na amlaze pema peponi.

Wafiwa wote poleni sana tena sana na wana JF wenzetu poleni sana.

Inasikitisha sana.
Inasikitisha sana lakini ndio mapenzi ya Muumba. RIP Mtoi. Tutaendeleza mapambano kwa kukuenzi wewe na makamanda wengine waliotangulia mbele ya haki. Umetangulia nasi tuko nyuma yako.

Jamani hili lisanamu FF huwa ni binadamu au ni li-robot? Maake binadamu hawezi kuwa na roho ya jiwe kama linavyoonesha!
 
Back
Top Bottom