TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

Inna Li Llahi wa Inna Ilayhi Rajiun.

Inasikitisha sana, jana tu nimetoka kumuulizia humu JF. Nilikuwa sijamsikia siku nyingi.

Allah amsameh, amghufirie na amlaze pema peponi.

Wafiwa wote poleni sana tena sana na wana JF wenzetu poleni sana.

Inasikitisha sana.

Du, inauma Sana ila Mwenyezi Mungu amrehemu.
 
Ikiwa kifo cha huyu bwana kuna mtu awaye yeyote anahusika nacho maana sarakasi za siasa tunazijua basi Mungu na asimame.
 
Pumzika kwa Amani kamanda Mohamedi Mtoi, na Mungu aipe faraja familia yako!
Mwana CCM ambaye uko humu, ambaye unashabikia jinsi wanaccm wenzio wanavyomdhihaki mh. Lowassa kwa sababu ya ugonjwa wake, ujifunze kwamba maswala ya afya na uzima ni Mungu tu ndio anajua, binadamu mwenye akili timamu hawezi kujivunia afya, maana afya na uzima ni neema tu kutoka kwa Mungu!, leo unashabikia dhihaka anayofanyiwa lowassa kesho baba yako au mama yako au Dada yako au kaka yako au wewe mwenyewe unakufa au unapata ajali na kua kilema!, tufanye siasa, maswala ya afya tumuachie Mungu!
 
Alikua mwenyewe kwenye gari??poleni sana familia ya marehemu na makamanda wote
 
dah!!!jf hii,huyu bwana namfahamu humu tu lakini msiba umenigusa sana!

Tangulia kamanda mtoi, upumzike kwa amani, tunaendeleza mapambano, we shall dedicate the victory to you

Nipigo kubwa sana kwa wana mabadiliko
 
Nimeumizwa sana na kifo hiki!.

Ama kweli nimeamini yanayosemwa na watu, "wanaopendwa na wengi, hufa wangali vijana!".

Ila Tanga nako....!, na hizi ajali za kuelekea chaguzi!....

Nimeikumbuka ajali ya Marehemu Juma Jamaldin Akukweti, ambayo ilitokea kuelekea uchaguzi!, ilikuja kusemekana kuna mkono wa mtu katika kugombea jimbo!, na huyo mtumiwa, japo alilitwaa hilo jimbo, lakini hakuchukua round, tena yeye aliondoka kwa mateso makubwa!.

Kama ni ajali ya kawaida, Mungu amrehemu marehemu!, lakini kama ni mkono wa mtu, subirieni 'karma' reaction soon, karma haikopeshi wala haiongopi!.

Poleni sana wafiwa, poleni Chadema!, poleni wana jf, tumempoteza sio tuu mwana jf mwenzetu, bali mpashanaji habari mahiri!.

RIP Kamanda Mtoi!.

Pasco
 
Too soon bro I know this guy a very young and determined politician ,nilikua nampenda sana anapo defend hoja za udini kwa UKAWA!!!daaah amefariki kipindi anahitajika sana R.I.P

Your very right, nakumbuka sana hoja zake na hivi karibuni nilikuwa simuoni jukwaani labda kama alikuwa haingii na ile verified id, apumzike kwa amani.
 
Sio siri roho imeniuma sana, kupoteza mtu huyu hata kama nilikuwa simfahamu ila tumepoteza
 
Mungu ampumzishe kwa aman
 

Attachments

  • 1442119116284.jpg
    1442119116284.jpg
    47.2 KB · Views: 221
Back
Top Bottom