Mwanadada bondia Claressa Maria Shields atangaza pambano lake dhidi ya bondia wa kiume Ryan Garcia amuoneshe kazi.

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Mashabiki wengi wa ngumi pamoja na mabondia mbalimbali wa ngumi duniani wameshtushwa baada ya kuona maandalizi ya pambano kati ya mwanadada Claressa Shields pamoja na bondia wa kiume Ryan Garcia .

Ryan Garcia tangu amtandike kiroho mbaya bondia Devin Haney amekuwa na mapepe sana mpaka imekuwa kero kwa mabondia wenzake.

Mashabiki walimjia juu Ryan Garcia baada ya kusema anataka kumtandika Errol Spence na akampa masaa 72 tu ya kukubali pambano hilo ili amchakaze kuliko alivyochakazwa na Terence Crawford.

Sasa kabla ya hili sekeseke halijapoa kamfata tena Claressa na kumuongelea kauli chafu .

Sasa Claressa sio demu wa maneno mengi kamwambia mambo yasiwe mengi nataka official fight na wewe na katoa kauli za kishujaa sana jambo lililowashtua wadau mbalimbali wa boxing duniani.

 
Sina wasiwasi na uwezo wa Claressa Maria Shields , atashangaza wadau mbalimbali wa boxing ulimwenguni.
 
Haney katutafutia kero sana mjini,looks hata lile pambano lake na lomachenko alibebwa,huyo garcia kiboko ni tanker
 
Ngoja tuonee
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ huyo demu nimemfuatilia hawez kupigana na huyo masta wakikubali kuingia ulingoni basi nyumbani kwake watandike turubai
Jibu jepesi ambalo naweza kusema humfahamu vizuri Claressa Shields.

Sio kwenye boxing kaenda kuwachallange hata wale wa MMA na bado kawatandika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…