Mwanadada bondia Claressa Maria Shields atangaza pambano lake dhidi ya bondia wa kiume Ryan Garcia amuoneshe kazi.

Mwanadada bondia Claressa Maria Shields atangaza pambano lake dhidi ya bondia wa kiume Ryan Garcia amuoneshe kazi.

Mashabiki wengi wa ngumi pamoja na mabondia mbalimbali wa ngumi duniani wameshtushwa baada ya kuona maandalizi ya pambano kati ya mwanadada Claressa Shields pamoja na bondia wa kiume Ryan Garcia .

Ryan Garcia tangu amtandike kiroho mbaya bondia Devin Haney amekuwa na mapepe sana mpaka imekuwa kero kwa mabondia wenzake.

Mashabiki walimjia juu Ryan Garcia baada ya kusema anataka kumtandika Errol Spence na akampa masaa 72 tu ya kukubali pambano hilo ili amchakaze kuliko alivyochakazwa na Terence Crawford.

Sasa kabla ya hili sekeseke halijapoa kamfata tena Claressa na kumuongelea kauli chafu .

Sasa Claressa sio demu wa maneno mengi kamwambia mambo yasiwe mengi nataka official fight na wewe na katoa kauli za kishujaa sana jambo lililowashtua wadau mbalimbali wa boxing duniani.

View attachment 2986786
K
 
Back
Top Bottom