Mwanafunzi aumizwa vibaya baada ya kuchapwa fimbo 20 na walimu 6 Jangwani Sekondari

Mwanafunzi aumizwa vibaya baada ya kuchapwa fimbo 20 na walimu 6 Jangwani Sekondari

Wewe Ni mwafunzi tena mtukutu unajua viboko 20 wewe? Acha ujinga soma na uache kutumia simu shuleni
 
Kwenye sheria mwalimu anatakiwa kumchapa viboko vitatu tu na kwa ruhusa ya Mwalimu mkuu. Sasa ukiua mwanafunzi utaulizwa ulichapa fimbo ngapi na sheria inasemaje.
Ndo ivo fimbo tatu hazitoshi.

Hiyo sheria wala haifuatwi na sio rafiki hata kidogo na huna pa kumpeleka mwalimu akilamba mboko nyingi labda itokee bahati mbaya akamuumiza bibaya mwanafunzi.
 
Kwahiyo mkuu unashauri viboko vitumike mtu achapwe viboko 50 maana adhabu ya viboko pia kuwa watu wanakua sugu huwezi mchapa mwanafunzi viboko vitano ili akome utaenda mpaka 50 sasa mkui viboko 50 au hata viboko 20 huoni unaelekea pabaya, nikuilize tu mara pah umemchapa ukampoteza mtoto wa watu utawajibu nini wazazi wake muangalia na side effect ya adhabu,

Mkuu ukiniambia kulima unazoea ni kama shuguli za nyumbani unakosea mashamba ya shule ni makubwa acha adhabu ya kulima zipo nyingi ambazo mtoto sio rahisi akawa mkaidi kwa kuzoea adhabu na mtoto akishakua kwenye hiyo stage ya ukomavu wa adhabu hata ukitumia fimbo hatasikia zaidi atakuongezea hasira utampiga vibaya
NDIO,,,, Viboko visiachwe Mashuleni

Na kwanini Mkuu unasisitiza sana Viboko vitaua mtoto,,,una research ya waliokufa kwa sababu ya kuchapwa Bakora,,, kuna Watu Afya zao ni mbaya always,,,,hata ukimrusha kichura tu anaweza kufa,,,,(Hili tusiliweke kama Hoja,,,ni assumption inayoweza kutokea pande zote)....kwasababu inahusisha Afya ya anayeadhibiwa....tujadili hoja tukiwa na assumption kuwa Mwanafunzi ana Afya Njema,,hana tatizo lolote

Vilevile kila jambo lina kiasi mkuu,,,, hata hizo adhabu zingine pia zina kiasi,,, so kiasi kizingatiwe.....Nikisema Bakora zitumike sina maana mtu achapwe bakora mia tisa.,,,so tuzungumze tukizingatia haya.
 
Kwani unavyoanza kuchapa unajua kama utaua, unajua ukichapa huwa kuna hasira nyuma ya lile tendo unalolifanya sasa ukianza kuchapa unakua huna dhamira ya kuua ila unaposhika bakora na kuanza kuchapa kila neno lake moja mwanafunzi wewe mwalimu unakazia mtoto anasema nimekosa sitarudia tena wewe ndiyo unazidisha kumla fimbo moyo wako unasema ngoja huyu leo mpaka akome unajua madhara ya hiyo dhana
Inatokeaga bahati mbaya tu kuchapa mpaka mtoto akapata madhara.

Na mwalimu anaejielewa hawezi kumchapa mwanafunzi maeneo hatarishi ni mikononi ama makalioni basi.
Kumchapa maeneo tofauti na hapo ni kutafuta kesi sasa.
 
zianzishwe speacial programs za kutrain walimu namna ya kuadhibu wanafunzi, viboko viwe na idadi yake na nanma ya kuchapa, kuwe na adhabu nyingine kama kuchimba mashimo ya takataka, kufanya kazi za jamii shuleni kama kufagia darasa unalosomea na wenzio, kupiga deki ofisi za walimu, kupanga vitabu library nk.....

Ifike mahala pia wazazi wawe wanaitwa mashuleni na kushauliana na walimu namna bora ya kuboresha tabia ya mtoto anayeonyesha tabia mbaya...shida nyingine huanzia majumbani....

Mwisho kabisa, Serikali iboreshe maisha ya walimi, walimu wengi wanahali duni zinazopelekea stress...
 
Ndo ivo fimbo tatu hazitoshi.

Hiyo sheria wala haifuatwi na sio rafiki hata kidogo na huna pa kumpeleka mwalimu akilamba mboko nyingi labda itokee bahati mbaya akamuumiza bibaya mwanafunzi.
Sema tu wanafunzi wengi ni wajinga wa sheria. Ila ningekuwa ni mimi nipo shule nisingechapwa fimbo zaidi ya 3. Wanafunzi wanaonewa kwa sababu ya kutojua sheria na haki zao. Cha kushangaza hata walimu wenyewe hawajui kuwa sheria inataka mwanafunzi mwisho kuchapwa fimbo 3, laiti wangekuwa wanajua wasingekuwa wanachaoa fimbo nyingi.
 
Mwalimu kama wewe watoto si ndo wangekupiga hadi dole la kati wewe!
Kuna adhabu za kuwapa watoto na sio mabakora. Ndio maana tunaonekana manyani meusi yasiyo na akili.
Mpe jembe akalime/afyeke/asafishe vyoo vya shule/apige magoti aite mvua mpaka wenzake wakitoka darasani/apewe suspension/alazimishwe asome vitabu kadhaa na aviandikie muhtasar la sivyo anafukuzwa shule n.k nk. mpe adhabu za kumjenga na sio kudhalilisha utu wake.
 
Walimu huwa ni wapumbavu sana. Huwa wana mob psychology
Uwe na adabu na heshima kwa walimu. Kilikupeleka Nini kwao Kama siyo kuongeza upumbavu uliokuwa nao Hadi ukahitimu kuwa mpumbavu mkubwa Kama ulivyo?
Fanya hivi, Anza kuwaita wazazi wako wapumbavu na wako na mob psychology kwani waliiga kwa majirani waliowapeleka watoto wao shule ili wakafundishwe upumbavu nawe ukaunganishwa huko ili ukawe mpumbavu mahiri Kama ulivyo Sasa!
Mpumbavu pro max katika ubora wako!
 
Adhabu gani Duniani ambayo haitii UOGA,,,.???? zitaje hizo adhabu ambazo hazitii UOGA.....
adhabu yeyote unayoijua ambayo itamfanya mhusika akuigope na sio kumjenga kupitia hio adhabu,adhabu yeyote inayotokela kama kukomoa/kulipiza kisasa pasipo kuwa na kiasi
 
Back
Top Bottom