Angel Nylon
JF-Expert Member
- Jul 26, 2011
- 9,164
- 18,402
🤪Ushawai kuona hizo rangi kama za huyo dada zinasota kupata ajira ?
Ushawai kuziona kwenye interviews za utumishi ?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🤪Ushawai kuona hizo rangi kama za huyo dada zinasota kupata ajira ?
Ushawai kuziona kwenye interviews za utumishi ?
Hakuna aliyesema miaka 21 ni umri mdogo uwe mwelewa.Miaka 21 ni umri mdogo? Chini ya 18 yrs old tumuitaje!
Inawezekana hawafuati mtaala wa NECTAHesabu hii umeipigaje..
21-6 =15
15-2=13
13-4=9
9-7=2
Then how is it Possible unasema inawezekana mwanafunzi ana Miaka 2 kuanza darasa la kwanza eniwei tuseme alianza akiwa na miaka 3 na bado hajamaliza internship mwaka 6...
Hata kama Mzee miaka 3..Inawezekana hawafuati mtaala wa NECTA
Twende pamoja.
Umri 5-12 msingi(7 yrs)
13-16 sekondari(4 yrs)
17-19 A level (2 yrs)
19- 23 Udaktari.(5yrs)
Hiyo 21 kuna madarasa alivushwa,au kuna udanganyifu mahali!
Palestine na Israel kawaida sana
Inawezekana na hakuna.cha kushangaza na hiyo ni kwa wachahce tu.Maana yake alimaliza kidato cha 6 na kuanza mwaka wa kwanza akiwa na miaka 16.
Alimaliza kidato cha nne na miaka 14.
Alimaliza la saba na miaka 10.
Alianza la kwanza na miaka 3.
Inawezekana kabisa.
Ma shaa Allah
Mwanafunzi huyo atakuwa miongoni mwa wahitimu 138 wa fani ya udaktai katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU) kwenye mahafali ya 21 yatakayofanyika siku ya Jumamosi.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam Makamu Mkuu wa chuo cha (HKMU), Profesa Yohana Mashalla wakati akizungumzia mahafali ya 21 ya chuo hicho.
Amesema kuwa wameangalia rekodi kwenye vyuo mbalimbali nchini na hawajaona mtu aliyewahi kuhitimu fani ya udaktari binadamu kwa umri huo.
“Tumeuliza kwenye vyuo mbalimbali vya tiba kuona kama kuna mtu aliyewahi kuhitimu shahada ya udaktari katika umri wa miaka 21 tumekosa. Tumeuliza Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili (MUHAS) lakini wamesema hawajawahi kutokea kwa hiyo tunampongeza Ahlam kwa kuweka rekodi,” amesema
Amesema mwanafunzi aliyewahi kupata Shahada ya Udaktari kwa umri mdogo alikuwa na umri wa miaka 23 hivyi kuwa na miaka 21 Ahlam ameweka rekodi ya aina yake.
Vile vile, HKMU) kimesema kimejipanga kuongeza matumizi ya teknolojia katika utoaji wa elimu, kuongeza tafiti, machapisho na ubunifu ili kwenda na kasi ya dunia kidijitali.
Amesema maboresho hayo yamo kwenye mpango mkakati wa miaka mitano ijayo kuanzia mwaka 2023-2028 ambao umejiita kwenye maeneo sita ya kimkakati.
Profesa Mashalla amesema HKMU imemaliza tathmini ya utekelezaji wa mpango mkakati wa chuo wa miaka mitano wa 2018-2023 mwezi huu kilizindua mpango mkakati wa miaka mitano.
Amesema mpango huo umejikita katika uimarishaji wa utoaji wa elimu na utawala ikiwa ni pamoja na mazingira ya kufundishia na kuongeza udahili, kuboresha mtandao na kuongeza matumizi ya teknolojia katika utoaji wa elimu kwa wanafunzi, wanataaluma na wafanyakazi.
Aidha, Profesa Mashalla amesema kwenye mpango mkakati huo chuo kimepanga kuongeza tafiti, machapisho, ubunifu na kuimarisha mifumo ya mipango na fedha.
Amesema katia kutekeleza mpango huo mwaka huu wa masomo chuo kimedahili wanafunzi wapya 465 katika fani mbalimbali.
“Ongezeko hili la wanafunzi katika mwaka wa kwanza litafanya chuo kuwa na jumla ya wanafunzi 1,628 kulinganisha na wanafunzi 1,452 katika mwaka wa masomo uliopita.
Amesema katika mahafali hayo jumla ya wahitimu watakuwa 296 na kati yao wanawake ni 166 na wanaume ni 130 wakati kwenye Shahada ya Udaktari wa Binadamu wanawake ni 65 na wanaume ni 73.
Profesa amesema kabla ya mahafali hayo kutakuwa na kusanyiko la kitaaluma ambao pia utajadili fursa za kibiashara na mgeni rasmi atakuwa aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene.
“Tumeona badala ya kujadili masuala ya afya peke yake tuita wataalamu wabobezi kwenye masuala ya biashara na uchumi ili nao watoe mchango wao katika utoaji wa watalamu kwenye sekta ya afya,” amesema
Chanzo: Nipashe
1atu wanaongelea kwa Tanzania.Kuna mwingine ghana kamaliza na miaka 20.
Una uhakika kasoma mtaala wako wa NECTA?Maana yake alimaliza kidato cha 6 na kuanza mwaka wa kwanza akiwa na miaka 16.
Alimaliza kidato cha nne na miaka 14.
Alimaliza la saba na miaka 10.
Alianza la kwanza na miaka 3.
Inawezekana kabisa.