Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) atuhumiwa kumuua Mwanafunzi mwenzake

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) atuhumiwa kumuua Mwanafunzi mwenzake

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (Must), mwaka wa kwanza, Emilia Joseph (21) kwa tuhuma za mauaji ya mwenzake wakiwa kwenye 'Club' ya Mbeya Pazuri jijini humo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amedai kuwa mtuhumiwa alifanya mauaji ya mwenzake wa mwaka wa tatu Gerald Philber Said (22), baada ya kumchoma na kitu chenye ncha kali tumboni

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumanne Juni 16,2025, Kamanda Kuzaga amesema tukio hilo lilitokea Juni 14,2025 saa 11.00 alfajiri wakiwa wamelewa pombe kupita kiasi

Amedai kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo ni baada ya kuibuka ugomvi baina ya marehemu na mtuhumiwa uliotokana na matumizi ya ulevi wa pombe kupindukia

" Baada ya kuibuka ugomvi mabaunsa walimtoa mtuhumiwa nje ambaye alienda kwenye eneo alikoegesha gari , ambapo marehemu alimfuata kwa lengo la kuendeleza ugomvi ndipo alipomchoma na kitu chenye ncha kali tumboni ,"amesema

Amesema baada ya marehemu kubainika kudhurika ndipo wasamaria wema walimbeba na kumuwahisha katika Hospitali ya Rufaa Kanda kwa matibabu zaidi

"Wakati madaktari wakiendelea kumpatia matibabu ilipofika saa 7.00 mchana alifariki dunia,"amesema.

Kufuatia tukio hilo Kamanda Kuzaga ameonya wanafunzi wa vyuo vikuu kuachana na matumizi ya pombe kupitia kiasi na badala yake kuzingatia masomo na kutimiza ndoto zao

must.png
 
Maisha ya bar,sjui club sehemu za ovyo kabisa
Haya mmoja hapo anaenda kuzikwa na nwingine kwenye majengo ya serikali
Hapo labda acheze na kesi na inaweza mchukua miaka kama 10 na zaidi ashapoteza kila kitu

Ova
 
Kilicho nishangaza ni kwamba wiki hii hapo must wameanza Ue. Inakuaje ijumaa baada ya kujiandaa na mitihani unnaenda pub? Mimi pia nimesoma must hapo kwa nature ya mitihani ya chuo hicho inaonekana hao vijana walikua wamejikatia tamaa.
 
Yaani kaamuliwa akaona haitoshi akaamua kumfuata jamaa huko huko nje Ili aendelee kugombana hatimaye kafuata kifo...Hizi mambo za ugomvi zinahitaji busara za kuzaliwa sana, ukishaona uko kwenye ugomvi halafu ukaamuliwa basi kimbia mbali na sehemu ya tukio. Aibu kweli.
 
Hakuna kesi hapo, marehemu alinifuata nikiwa naondoka kuepusha ugomvi akiwa na silaha ikabidi nijihami ili kujiokoa.

Kijana atasumbuliwa hapa hapa na pale lakini anatoboa kwenye hiyo kesi.

Ulevi sio kitu kizuri, madhara yake ni makubwa sana.
Ni kweli!

Kwa nchi zenye mifumo makini ya sheria dogo angepata very light sentence ya kuua bila kukusudia.

Huku kwetu sheria ni pesa yako tu.
 
Back
Top Bottom