Mwanafunzi wa field azungumza mbele ya RC Chalamila changamoto ya Rushwa ya ngono wanayokumbana nayo kwenye ofisi mbalimbali wakati wa kutafuta field

Mwanafunzi wa field azungumza mbele ya RC Chalamila changamoto ya Rushwa ya ngono wanayokumbana nayo kwenye ofisi mbalimbali wakati wa kutafuta field

Rushwa ya ngono imetajwa kama kikwazo kikubwa kwa Wanafunzi wa kike wanaokwenda kuomba kufanya field katika Ofisi mbalimbali nchini Tanzania ambapo kero hiyo imeibuliwa na Mwanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila.

Baada ya ziara ya Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila Chuoni hapo kukagua miradi ya ujenzi, alifanya mkutano na Uongozi wa Chuo pamoja na Wanafunzi wa Chuo hicho ambapo katika waliohusika kutoa maoni ni huyu aliyepaza sauti kuhusu rushwa ya ngono.
#milardayoupdates.

Shida hii ipo toka Enzi za Ukoloni. Vitu kama hv zamani ilikua n siri sio kutangaza kwenye vyombo vya Habari. Yaan ukiombwa mzigo na Boss wko unakubal au kukataa kimya kimya.
Vijana,Wadada na Wamama wa siku hizi hawana kabisa SIRI. Kila kitu kwao n kuongelea tu kwa watu. Maadili ya kizaz hiki yameshuka sana.
 
Ila hiyo ya malecture wanakuza sana tofauti na uharisia ulivo.

Mwanafunzi ndo atamtafuta lecture kwa ajili ya course work.
Hapo utasema lecture ndo mwenye shida au mwanafunzi..?
Hii nimeishuhudia mkuu, lecturer akishamuelewa student flani anaanza kumfuatilia kikawaida Ila akikataliwa ndio anaanza kutumia "ulekcha" wake kufanya hivyo. Na usichokitambua, kuna baadhi ya "lecturers" hiyo kwao ni part of fun na huwa wanahadithiana na kusaidiana.
Kuna chuo kimoja, kuna lecturer alikuwa ana tabia ya kutembea na wanafunzi group zima, yani kama kuna watoto wa kike wanaopenda kutembea pamoja, yeye atataka kuwapitia wote ili tu atimize fantasy zake


Nakuhakikishia, ikitengenezwa system ya kukamata lecturers, wengi watafukuzwa kazi
 
Vyuoni wengi wanafosiwa japo wanaojilengesha nao wapo pia.
Kabisa Ila watu wanachukulia wachache wanaotoa rushwa za ngono kusawazisha mambo yao. Na usishangae, student kamiss mtihani au kakamatwa somo flani, lecturer ndio anatumia huo mwanya kufanya yake..

Vyuoni kuna mengi yanaendelea. Lecturers baadhi wanatumia wanafunzi kama part of fun
 
Back
Top Bottom