Mwanafunzi wa Kidato cha 3 ahukumiwa kuchapwa viboko 12 kwa kumlawiti mwenzake

Mwanafunzi wa Kidato cha 3 ahukumiwa kuchapwa viboko 12 kwa kumlawiti mwenzake

Hali ya mmomonyoko wa maadili imekuwa kubwa sana kwenye jamii zetu

Wazazi tuzidishe maombi Kwa watoto wetu, bila kusahau kusimamia suala la malezi yao kiukamilifu
Tujitazame nyenendo zetu pia,kama dhambi kwetu kufanya ni suala la kawaida....basi wanetu maji yatafuata mkondo.Tumrudie Bwana
 
Hii kitu haizingatii majina asili wala dini bro!

Kuna baba hapo Mara akiitwa Nyantira sijui nani siukumbuki ubini wake lakini ni hawa hawa majina ya asili alimpasua speaker mwanae wa kiume wa kumzaa.
Asante kwa ufafanuzi, nilikuwa nimejipotosha, maana kuna watu wa hayo majina ya zile nchi zinazalisha mafuta kwa wingi.
 
Mtu yeyote aliye chini ya miaka 18 anahesabika kama mtoto na kesi zao zinaendeshwa kulingana na sheria ya mtoto namba 21 ya 2009. Kifungu 119 (1) kinaeleza kuwa mtoto hafungwi bali anapewa adhabu mbadala. Na hata adhabu ya viboko imefutwa kwa watoto. Kwa hiyo hapo hukumu ni kifungo cha nje kikiambatana na fidia. Kiukweli sheria ya mtoto inahitaji kufanyiwa mabadiliko. Angalau kuwe na kipengele cha adhabu ya kufungwa katika gereza la vijana.
 
Nakumbuka movie flani ya Hollywood jamaa alienda mahakamani alipoona hukumu ya judge imezingua akasema ameamua kusamehe kesi mahakama kama ikataharuki
Jamaa akaamua kuja ku deal na wale wahuni kwa sheria za mtaa ilikuwa ni mwendo wa guns kwa kwenda mbele
 
Tujitazame nyenendo zetu pia,kama dhambi kwetu kufanya ni suala la kawaida....basi wanetu maji yatafuata mkondo.Tumrudie Bwana
Ni kweli

Huenda matokeo ya dhambi za kizazi cha akina Ruthu enzi za Sodoma na Gomora ndiyo tunayaona sasa

Ngoja Wazee tuendelee kuliombea Taifa 🙏
 
Hija Hamis Msumi (16) Mwanafunzi ya Kidato cha Tatu, ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nyanjati wilaya ya Kibiti, mkoa wa kipolisi Rufiji, amehukumiwa adhabu ya kuchapwa viboko 12, kwenye makalio mbele ya mahakama kwa kosa la kumbaka na kumlawiti mwanafunzi wa darasa la Nne mwenye umri wa miaka 12.

Mahakama imemuamuru mshitakiwa huyo kumlipa muhanga fidia ya Shilingi laki 5, kwa madhara ambayo amemsababishia mwanafunzi huyo ambaye jina lake limehifadhiwa.

Mahakama imesema mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo kati ya mwezi Agosti na Novemba, 2023, huko Kijiji cha Nyanjati wilaya ya Kibiti.
Chanzo: ITV
Safi sana na aweke chini ya uangalizi wa dawati la jinsia akariporti huko hata miezi 3.
Hadi ajua tabia ya kipidid sio nzuri.
 
Hali ya mmomonyoko wa maadili imekuwa kubwa sana kwenye jamii zetu

Wazazi tuzidishe maombi Kwa watoto wetu, bila kusahau kusimamia suala la malezi yao kiukamilifu
Shida tunatoka SAA 12 tunarudi SAA 3 usiku watoto wanalelewa na dada wakazi plus English medium
 
Back
Top Bottom