TANZIA Mwanafunzi wa mwaka wa Pili wa Chuo cha Misitu auawa kikatili

TANZIA Mwanafunzi wa mwaka wa Pili wa Chuo cha Misitu auawa kikatili

Kama ni hivyo na waliofanya Wana roho ngumu asee Kama vile wao ni waaminifu sana
Kitu nilichojifunza wanawake wengi wanachukulia poa sana hisia za watu bila kutambua ukomo wa uvumilivu unatofautiana baina ya mtu na mtu,pia kuna binadamu wengine ni wanyama sana.

Wanawake wengi wanapoumizwa hisia zao hukimbilia kwa waganga,kwa wanaume vitu ni tofauti.
 
Haya yatakuwa mapenzi tu pengine kawachanganya wavuta bange wa Kaskazini
R.I.P felista
 
Mwili wake ulikutwa mtupu jirani na korongo ukiwa umechomwa na vitu vyenye ncha kali pamoja na kufanyiwa ukatili

Tukio hilo la kusikitisha limetokea siku ya xmas

======

Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo cha Misitu Tanzania (FITI), Felista Daudi (21) ameuawa na mwili wake kutupwa kwenye korongo katika eneo la Laliga mjini Moshi.

Mwili huo uliokotwa ukiwa bila nguo huku ukiwa umetobolewa sehemu mbalimbali kwa kitu chenye ncha kali, na ukiwa na viashiria pia vya kufanyiwa vitendo vya ukatili.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Ronald Makona alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mwili wa mwanafunzi huyo uliokotwa kwenye korongo.

“Ni kweli tukio limetokea la mwanafunzi huyu kuuawa na mwili wake ulikutwa umetupwa kwenye korongo.

“Lakini dalili za kwenye eneo la tukio hazionyeshi aliuawa pale, inaonekana aliuawa katika sehemu nyingine na kisha kutupwa kwenye hilo eneo,” alisema Kamanda Makona. Makona alisema Jeshi la Poli-si linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wote walio-husika na tukio hilo.

“Juhudi za uchunguzi zinaendelea ili kubaini chanzo cha mauaji haya na tayari simu za marehemu tunazo, tuna-chokifanya sasa tunafuatilia kujua mtu wa mwisho aliyewasiliana naye ni nani, ili hatua nyingine zichukuliwe,” alisema Kamanda Makona.

Akizungumzia tukio hilo, Ofisa utumishi wa chuo hicho, Havyalimana Nyamaliza alise-ma Desemba 25, mwanafunzi huyo alitoka na wenzake kwa ajili ya kusheherekea Krismasi na hakurudi nyumbani aliko-panga.

“Desemba 26 asubuhi nilipigiwa simu kuwa kuna mwili wa mwanafunzi wetu umetupwa na uko pembeni ya maji kwenye korongo, tulifika eneo la tukio kuutambua mwili ndio tukabaini kuwa ni mwanafunzi wetu wa mwaka wa pili.

“Tulipofika kwenye eneo la tukio mwili wa mwanafunzi wetu ulikuwa mtupu, akiwa amechomwa na vitu vyenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake, ambapo kwenye ziwa upande wa kushoto na kwenye mbavu alikuwa amechomwa na kitu chenye ncha kali.

“Ni tukio lenye kusikitisha na lenye kuumiza, pia mwili ulionekana kama umefanyiwa ukatili (kubakwa), tunaomba Jeshi la Polisi kuhakikisha waliohusika na tukio hili wanakamatwa ili haki itendeke,” alisema ofisa huyo.
Katika kipindi kama hiki mwaka jana pia kulikuwa na matukio kadhaa ya mauaji, kujeruhiana na kujinyonga.

Mwaka huu 2020 ulianza kwa Polisi Kilimanjaro wanamsaka mama na mtoto wa miaka 12, ambaye alikuwa anadaiwa kumuua kwa jiwe mpenzi wa mama yake mzazi aliyetajwa kuwa ni Serafin Mrema (29).

Pia, walikuwa wanasakwa wamuua kwa kumchoma visu polisi anayejulikana kwa jina la Living, ambaye alikuwa ametoroka lindo na kwenda kunywa pombe na askari mwenzake.
Some a happy some are not.
Wengine wanakufa
Wengina wanatafutwa kwa kuua.

Dunia bado ipo na mambo mengi sana.
Tuzidi kujichunga.
 
Xmas ndio nini?
Kama uliweza kuweka paragraph kubwa hivi ulishindwa nini kuandika kwa ufasaha?
X haipo kwenye neno Christmas.
Nyie ndio mnaovaa suruali zimechanwa miguuni utadhani ni mafukara wa akili.
Ok, turudi kwenye mada.
Ulevi na uesharati ndio hupelekea vijana kufa vifo vya hali hii
 
Duh! aisee nimepita eneo fulani huku Goba usiku wa leo mida ya saa nane nikiwa kwa miguu...nimekuta gari Premio nyeupe imechomekwa vichakani kama inataka kuelekea mabondeni huko...nilienda kuchungulia kama kuna mtu yamemsibu nikaikuta tupu na wala haijaharika..nahisi imefanya tukio nikirudi mtaani ntaulizia kilichojiri.

Tuweni makini hizi sikukuu...RIP
@Kelevra
Salamu.. Naomba kama utaweza kupata detail za hiyo Premio nikimaanisha namba za gari tuwasiliane PM pls. Kuna Premio nyeupe ya Rafiki yangu imeibiwa wiki ya pili sasa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usikute kala vya watu hataki kutoa mzigo, na nyodo juu, au kagonganisha mabwana wakaona wamfanyizie, ila yote kwa yote tuliachie jeshi la polisi lifanye uchunguzi na wahusika wachukuliwe hatua kali kwa unyama huu. Pumzika kwa amani binti.
 
@Kelevra
Salamu.. Naomba kama utaweza kupata detail za hiyo Premio nikimaanisha namba za gari tuwasiliane PM pls. Kuna Premio nyeupe ya Rafiki yangu imeibiwa wiki ya pili sasa..

Sent using Jamii Forums mobile app
Nikirudi jioni nitaulizia...maana ilikua ni usiku wa saa nane na asubuhi nimepita njia nyingine.
 
Duh! aisee nimepita eneo fulani huku Goba usiku wa leo mida ya saa nane nikiwa kwa miguu...nimekuta gari Premio nyeupe imechomekwa vichakani kama inataka kuelekea mabondeni huko...nilienda kuchungulia kama kuna mtu yamemsibu nikaikuta tupu na wala haijaharika..nahisi imefanya tukio nikirudi mtaani ntaulizia kilichojiri.

Tuweni makini hizi sikukuu...RIP
Unaroho ngumu, nawewe ungenasa hapo !
 
Back
Top Bottom