Mwanafunzi wa UDSM akamatwa kwa kusambaza taarifa na Takwimu za uongo za Covid-19 WhatsApp

Ndo maana wamemkamata ili athibitishe hao wagonjwa 200 wapo wapi?.
huyo ni mtuhumiwa tu akiwaonesha hao wagonjwa walipo ataachwa HURU.
Taarifa sahihi ni ipi? Askari wamejuaje kuwa hio taarifa sio sahihi? Je, ilileta madhara gani kwa jamii?

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
Taarifa sahihi ni zile zinazotolewa na serikali kupitia kwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na si vinginevyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna nchi inayoitwa "mpk ss Tanzania" tuna jamhuri ya muungano wa Tanzania au kwa kifupi JMT, inawezekana huyo binti alikuwa anaongelea mtaa mmoja huko china
 
Taarifa sahihi ni zile zinazotolewa na serikali kupitia kwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na si vinginevyo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mathalani wewe Yonga imetokea umekufa nami nikaandika mtandaoni kuwa "Yonga amekufa" hii itakuwa ni taarifa isiyo sahihi na ni kosa? wakati serikali ikisema hiyo itakuwa sio kosa? ukweli sheria ile very soon itahitaji marekebisho kwani inaleta mgongano kwenye uhuru wa kuongea
 
Tbc nao walitoa taarifa zisizo sahihi
Vp wao hawakamatwi?
 
Inaweza kua inahitaji marekebisho sawa sikatai lakini kwa sasa tuifuate sheria iliyopo kabla ya hayo marekebisho unayo yataka.

Halafu kumbuka kauli ya waziri mkuu alisema kwamba anayepaswa kutoa taarifa za ugonjwa huu ni waziri wa afya tu na ikishindikana atatoa yeye au makamu au rais mwenyewe

Kuna aina za taarifa mkuu sio kila taarifa hairuhusiwi kutolewa kuna taarifa zingine lazima zitolewa na mamlaka husika kwa maslahi mapana ya taifa na wamefanya maksudi ili kuondoa taharuki hivi kila mtu akianza kutoa taarifa zake kuhusu corona we unaona itakua sahihi kwa jamii yetu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli siku zote una tabia ya kuuumbua
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Usikute nasikia Mtaani, yeye sio chombo cha Habari wala msemaji was chochote
 
Taarifa sahihi ni ipi? Askari wamejuaje kuwa hio taarifa sio sahihi? Je, ilileta madhara gani kwa jamii?
angetoa ushahidi wa hao watu 230 waliogua na 4 waliokufa kama alivyosema angekuwa sahihi Kama hauna ushahidi huo huyo dada ajiandae na kuingia kwenye mikono ya sheria.
 
Kwani taarifa zinawezaje kuenea si zinaenea kwa style hizi hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…