Mwanafunzi wa UDSM akamatwa kwa kusambaza taarifa na Takwimu za uongo za Covid-19 WhatsApp

Mwanafunzi wa UDSM akamatwa kwa kusambaza taarifa na Takwimu za uongo za Covid-19 WhatsApp

Maskini,, pengine alikusudia kuandika wagonjwa 23 ila akakosea 0 ikajiongeza bila yeye kukusudia.

Ndio imeshakua hivyo watamkazia ili wapatiepo sifa,, kwahiyo fine itamuhusu tu,,
 
Maskini,, pengine alikusudia kuandika wagonjwa 23 ila akakosea 0 ikajiongeza bila yeye kukusudia.

Ndio imeshakua hivyo watamkazia ili wapatiepo sifa,, kwahiyo fine itamuhusu tu,,
Na ndio kilichotokea na hakuna sifa watakayopata, wabunge wa shy nao hovyo tu yamenyamaza kimya, hivi Salome yule mbunge wa vitimaalumu yupo kweli? Hapa ndio namkumbuka Rachel mashishanga
 
Maoni SI lazima mtu akitaka kutoa yapelekwe kwanza shirika la viwango,yakathibitishwe,maoni mtu hutoa tu,tofautisha kutoa maoni na kutoa taarifa rasmi
Mkuu, tofautisha maoni na takwimu. Huyo binti hakutoa maoni ilà alitoa takwimu za walioathirika na waliokufa. Kazipata wapi? That's another question!!
 
Hajalazimisha kwamba takwimu alozotoa kipindi anachati wasapu nduo za kweli.
Takwimu rasmi SI zinafahamika,,kwanini upoteze human resource kusneak kwenye magroup watu wanapiga soga kutafuta mtu wa kukamata?

bado upoteze resource kumsaka na kumkamata na bado resource za kumweka ndani na kumpeleka mahakamani kwa kupiga soga?
Ni issue ndogo mno hata kutumia kuipa muda wa kuifuatilia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefuatilia Michango yote kwa umakini ya WADAU waliochangia hapa, nikitegemea kukutana na Mchango wa Mlimbwende Victoire.

Shawty yuko wapi?
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mwaka wa Tatu Kitivo cha Kiswahili Mariam Jumanne Sanane (23) kwa kosa la Kuchapisha na kusambaza taarifa na takwimu za uongo kuhusu Corona kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Whatsapp.

Akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari leo Jumamosi Aprili 11,2020,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba mtuhumiwa alikamatwa Aprili 9,2020 majira ya saa mbili na dakika saba(2:07) usiku eneo la Mwadui, mtaa wa Tabora, kwenye machimbo ya almasi wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kwa kosa la kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii.

“Tarehe 26/03/2020 Askari wa kikosi kazi cha mtandao kilifanikiwa kuona ujumbe kwenye whatsapp uliotumwa na mtuhumiwa unaosema ‘mpk ss Tanzania ina wagonjwa wapatao takribani 230 wa Covid 19 na waliofariki ni 04”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

Amesema mtuhumiwa amepekuliwa na kukutwa na simu iliyotumika kutuma ujumbe huo na ameshahojiwa na atafikishwa mahakamani kwa makosa ya kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo mtandaoni pamoja na kutoa takwimu za uongo.

Kamanda Magiligimba ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii na kuacha kupotosha watu kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Huyo rpc nae bumuda tu kama sura lake,ukimuona utafikiria fundi majeneza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Police wa Tanzania kwa mikwara!!!eti wanaweza kudukua WhatsApp serikali kama china wameshindwa kudukua WhatsApp sembuse ccm [emoji23]


Sent using IPhone X
 
Wamsamehe tu, hii sheria huko mbeleni inabidi wake waifute, Uhuru wa kutoa maoni Hapa unakiukwa, kila mtu anajua takwimu rasmi ni zipi na kila mtu anafuatilia taarifa rasmi kwa umakini Sana,
Acha ujinga weewe. Wizara ya Afya pekee ndiyo inayo mamlaka ya kutoa taarifa zozote za magonjwa. Acheni utoto nyie bavicha
 
Mathalani wewe Yonga imetokea umekufa nami nikaandika mtandaoni kuwa "Yonga amekufa" hii itakuwa ni taarifa isiyo sahihi na ni kosa? wakati serikali ikisema hiyo itakuwa sio kosa? ukweli sheria ile very soon itahitaji marekebisho kwani inaleta mgongano kwenye uhuru wa kuongea
Kamanda kuwa mpole. Binti amepewa nafasi ya kuthibitisha taarifa zake akiwa mahakamani
 
Ulimbukeni wa mitandao, ngoja sheria ishughulike nae
 
Back
Top Bottom