Mwanafunzi wa Upadri (Frateri) wa Kanisa Katoliki Shirika la Roho Mtakatifu Tanga anadaiwa kujinyonga hadi kufa

Mwanafunzi wa Upadri (Frateri) wa Kanisa Katoliki Shirika la Roho Mtakatifu Jimbo la Tanga Rogassion Hugho anadaiwa kujinyonga hadi kufa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amezungumza na JamiiForums na kusema “Ni kweli huyo Mwanafunzi wa Upadri amekutwa amejinyonga kwenye mazingira ya eneo wanalosoma (Magamba alipokuwa akiishi).

“Uchunguzi wa awali unaonesha chanzo ni kwamba alifeli masomo yake, akiwa ndiye Mwanafunzi pekee kati ya wote waliofanya mitihani.

“Alikuwa na umri wa Miaka 25 na kinachofanyika kwa sasa ni uchunguzi wa Jeshi la Polisi kuendelea ili kubaini kama kulikuwa kitu kingine kilichosababisha afanye maamuzi hayo.”

Amesema chanzo cha kujinyonga kwake kinadaiwa ni kufeli mtihani wake uliokuwa unampeleka kwenye Daraja la Upadri ambapo wenzake wote wamefaulu kasoro yeye.

Hivyo, kutokana na msongo wa mawazo ndiyo akafikia uamuzi huo wa kujinyonga,” amedai Kamanda Mchunguzi.

Amesema Polisi wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho na ukikamilika, taarifa kwa umma itatolewa.
Hii habari ndio inanifanya niamini mapadri huwa wanafanya umalaya kuliko watu wenngine wote, yaani mtu ujinyonge kisa umekwepeshwa na jela ya maisha?
 
Mwanafunzi wa Upadri (Frateri) wa Kanisa Katoliki Shirika la Roho Mtakatifu Jimbo la Tanga Rogassion Hugho anadaiwa kujinyonga hadi kufa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amezungumza na JamiiForums na kusema “Ni kweli huyo Mwanafunzi wa Upadri amekutwa amejinyonga kwenye mazingira ya eneo wanalosoma (Magamba alipokuwa akiishi).

“Uchunguzi wa awali unaonesha chanzo ni kwamba alifeli masomo yake, akiwa ndiye Mwanafunzi pekee kati ya wote waliofanya mitihani.

“Alikuwa na umri wa Miaka 25 na kinachofanyika kwa sasa ni uchunguzi wa Jeshi la Polisi kuendelea ili kubaini kama kulikuwa kitu kingine kilichosababisha afanye maamuzi hayo.”

Amesema chanzo cha kujinyonga kwake kinadaiwa ni kufeli mtihani wake uliokuwa unampeleka kwenye Daraja la Upadri ambapo wenzake wote wamefaulu kasoro yeye.

Hivyo, kutokana na msongo wa mawazo ndiyo akafikia uamuzi huo wa kujinyonga,” amedai Kamanda Mchunguzi.

Amesema Polisi wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho na ukikamilika, taarifa kwa umma itatolewa.
ALIANZA ASKOFU
KAJA MWANAFUNZI
NXTY...MASISTER WA PAROKIA .JIANDAÈE HILI N ROHOOO
 
Kumbuka ufute nyuzi zako za zamani ili wasikufate Wayahudi

1. Si tulishakubaliana kujibu hoja kwa hoja?

IMG_20240521_151515.jpg

2. Kulikoni kurukaruka kama bisi kwenye kikaangio?

3. Bila kusahau ICC huhitaji wachumba tu, majibu yako tafadhali!
 
Frateri wa Kanisa Katoliki Shirika la Roho Mtakatifu Jimboni Tanga, Rogassion Massawe, anadaiwa kujinyonga hadi kufa.

Hili ni tukio la pili kwa viongozi wa dini kudaiwa kujinyonga. Mei 16, 2024 mkoani Dodoma, Askofu Mkuu wa Makanisa ya Methodist, Joseph Bundala naye alidaiwa kujinyonga ndani ya ofisi yake iliyopo katika kanisa hilo eneo la Meriwa jijini Dodoma.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu jana Jumatatu Mei 20, 2024 usiku, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi kuhusiana na kujinyonga kwa Frateri Massawe, amesema amekutwa amejinyonga kwenye nyumba yao ya Malezi ya Magamba aliyokuwa akiishi.

Hata hivyo, kamanda huyo amesema chanzo cha kujinyonga kwake kinadaiwa ni kufeli mtihani wake uliokuwa unampeleka kwenye daraja la daraja la ushamasi kuelekea upadri.

“Taarifa za awali tulizozipata zinadai sababu ya kujinyonga kwa mwanafunzi (Frateri) huyo, walikuwa na mitihani ya kuvuka kutoka ngazi moja, kwenda mwaka mwingine, sasa katika wenzake wote yeye peke yake ndio amefeli.

Hivyo kutokana na msongo wa mawazo ndiyo akafikia uamuzi huo wa kujinyonga,” amedai Kamanda Mchunguzi.

Amesema Polisi wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho na ukikamilika, taarifa kwa umma itatolewa.

Mwananchi leo Jumanne Mei 21, 2024, limezungumza pia na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Magamba wilayani Lushoto, Julias Nyangusi amesema tukio hilo lilitokea jana na taarifa za kujinyonga kwa Frateri huyo walizipata mchana.

Amekiri kuwa Massawe alikuwa akiishi kwenye nyumba ya malezi (wamezoea kuita chuo cha mapadri) iliyoko katika mtaa huo.

“Na taarifa za awali tulizozipata zinadai ni barua aliyopewa na uongozi wao ikimtaka aondoke kwenye nyumba hiyo kwa sababu hataweza kuweka nadhiri ya kiapo cha upadri (ushemasi) mwezi ujao,” amedai mwenyekiti huyo.

Mwenyekiti huyo amedai taarifa zaidi zinadai marehemu ameacha ujumbe wa maandishi kwenda kwa mama yake unaosomeka; "Mama usilie, nimeshindwa kufikia malengo, ninajua nimewakwaza wengi,” amedai Nyangusi.

Mwananchi limewatafuta viongozi wa nyumba hiyo ya malezi na wengine wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga bila mafanikio.

Hata hivyo, mmoja wa viongozi wa nyumba hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa si msemaji, amesema ni kweli Frateri Massawe amejinyonga lakini ni mapema mno kuzungumzia hilo bali taarifa kamili zitatolewa na viongozi wa kanisa baadaye.

CHANZO: MWANANCHI
 
Duu, Huyu itakua vigezo vya Wito tuu ndio amekosa, Advance pale USA river alikua vizuri sana, ni # 2/3, leo hii uniambie Amekua wa Mwisho out of 14?
Sijui hili darasa lina nini, namba 1 naye hivyo hivyo alijimaliza kwa kuambiwa hawezi kuendelea..
 
Naoma Fr. Deusi kamla kichwa mchaga mwenzake wa kibosho, Holly ghost Hawana utani, Brother alitorokaga pale Oaklands Magamba enzi hizo za Shayo,

Mimi niliwaambiga live pale USA RIVER kua sina wito, jamaa yangu akafosi, akaishia kudakwa akiwa anasafirisha vingurue.

Wengine wanahama shirika, Zamani ya Babu ilikua kuanza 20 na kumaliza 10 ilikua jambo la kawaida, Usiombee usiwe Mchaga sasa, hapo ndio balaa na nusu.
 
View attachment 2996105

Mwanafunzi wa Upadri (Frateri) wa Kanisa Katoliki Shirika la Roho Mtakatifu Jimbo la Tanga Rogassion Hugho anadaiwa kujinyonga hadi kufa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amezungumza na JamiiForums na kusema “Ni kweli huyo Mwanafunzi wa Upadri amekutwa amejinyonga kwenye mazingira ya eneo wanalosoma (Magamba alipokuwa akiishi).

“Uchunguzi wa awali unaonesha chanzo ni kwamba alifeli masomo yake, akiwa ndiye Mwanafunzi pekee kati ya wote waliofanya mitihani.

“Alikuwa na umri wa Miaka 25 na kinachofanyika kwa sasa ni uchunguzi wa Jeshi la Polisi kuendelea ili kubaini kama kulikuwa kitu kingine kilichosababisha afanye maamuzi hayo.”

Amesema chanzo cha kujinyonga kwake kinadaiwa ni kufeli mtihani wake uliokuwa unampeleka kwenye Daraja la Upadri ambapo wenzake wote wamefaulu kasoro yeye.

Hivyo, kutokana na msongo wa mawazo ndiyo akafikia uamuzi huo wa kujinyonga,” amedai Kamanda Mchunguzi.

Amesema Polisi wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho na ukikamilika, taarifa kwa umma itatolewa.
Poor young soul.....😌😌
 
Rip. Ila mapadre wa katoliki wanaongoza kuwa na long life expectancy. Na pia mbali na madhaifu machche ya kidini , catholic ni moja ya taasis ambayo iko well stuctured organized iliyodumu kwa zaidi ya miaka 2000
 
Duu, Huyu itakua vigezo vya Wito tuu ndio amekosa, Advance pale USA river alikua vizuri sana, ni # 2/3, leo hii uniambie Amekua wa Mwisho out of 14?
Sijui hili darasa lina nini, namba 1 naye hivyo hivyo alijimaliza kwa kuambiwa hawezi kuendelea..
Poleni sana, kuna roho chafu ilipandikizwa hapo
 
Back
Top Bottom