Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera anadaiwa kuvamiwa na 'watu wasiojulikana' nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es salaam baada ya watu kadhaa wakiwa na magari kuvamia na kuzingira nyumba na kuzuia watu kuingia.
Namba ya gari lililomchukua imetajwa ni T746DFS.
Erick Kabendera, a Tanzanian journalist, has been abducted from his home in Mbweni, Dar es Salaam. He told one of his colleagues of a high presence of security vehicle and unknown people around his house shortly before he disappeared to never be reached by phone this evening.
UPDATES:
Baada ya watu hao kuzingira nyumba huku wakionekana kuwa na nia ovu, yeye na familia walifunga milango. Wananchi akiwemo M/kiti wa mtaa walipofika na kuhoji wao ni nani walisema wao ni Polisi (hawakuwa na sare wala gari la polisi). Sasa inadaiwa wamekwenda naye kituo cha Polisi Oysterbay.
UPDATES: 2100HRS
Jeshi la Polisi inadaiwa linaendelea kumhoji Kabendera kuhusu mambo ambayo hayajawekwa wazi na wala hawajasema anahojiwa kituo gani. Taarifa hii ni kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kinondoni.
Kabendera alichukuliwa na watu 6 waliokuwa na silaha na inadaiwa simu yake ilikuwa blocked tangu. Jumamosi huku Mtandao wa Vodacom wakimwambia wamefanya hivyo kwa maagizo ya TCRA. Wakimtaka ajisalimishe Voda Shop
Wananchi waliokusanyika nyumbani kwa Erick walijitahidi kuwazuia watu hao na kuwataka wajitambulishe. Pamoja na jitihada za wananchi kutaka kupiga picha, simu zao zimechukuliwa kwa kudaiwa kuwa hawaruhusiwi kupiga picha.
05:20am - July 30, 2019
Chanzo kinabainisha Erick alikamatwa na Maafisa wa Polisi waliotokea Kituo cha Polisi Mbweni lakini njiani inadaiwa magari yalibadilishwa na bado hakuna taarifa rasmi za kituo gani anahojiwa.
10:20am - July 30, 2019
IGP Simon Sirro amethibitisha Kabendera anashikiliwa na Jeshi la Polisi na kuwa Polisi kupitia Kamanda Mambosasa wataongea na Vyombo vya Habari ifikapo saa 7 mchana
10:25am - July 30, 2019
TCRA wamekanusha kuhusika kwa namna yoyote na uzimwaji/ukatwaji wa mawasiliano ya simu ya Kabendera na kusisitiza kuwa wao wanahusika na kudhibiti simu zisizotakiwa (fake)
10:28am - July 30, 2019
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema suala la Erick Kabendera kuhojiwa ni la Polisi na si la Serikali
UPDATES1400HRS
- Erick Kabendera anashikiliwa na Polisi, anahojiwa kuhusu Uraia wake.
ZAIDI, SOMA:

- Kamanda Mambosasa: Mwandishi Erick Kabendera anahojiwa uraia wake
- Polisi wakagua nyumbani kwa Erick Kabendera, waondoka na hati yake ya kusafiria na nyingine za ndugu zake
- Mmoja wa Mawakili wa Erick Kabendera aeleza kinachoendelea
- Free Erick Kabendera
- Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu
- Mama Mzazi wa Erick Kabendera amuomba Rais Magufuli kumsamehe mwanae
- Mama mzazi wa Mwandishi Erick Kabendera, Verdiana Mjwahuzi amefariki dunia leo Jumanne Desemba 31, 2019
- Kisutu: Kesi ya Erick Kabendera yaendelea. Jamhuri yaweka kisiki Erick kushiriki msiba wa mama yake mzazi
- Danadana: Kesi ya Kabendera yaahirishwa kwa madai kwamba Hakimu kapata udhuru
- Mwandishi wa habari za Kiuchunguzi, Erick Kabendera ataka kuongea na DPP ili kumaliza kesi yake
- Erick Kabendera aachiwa huru baada ya kukiri makosa na kufutiwa shtaka
- Amnesty International: Kabendera ameonewa, hakustahili kununua uhuru wake
- Erick Kabendera atoa maoni yake kwa Tume ya Haki Jinai, Adai Mahakimu wa Mahakama wanaiogopa ofisi ya DPP
- Erick Kabendera aitaka Vodacom imlipe Dola Milioni 1 kwa kufanikisha kutekwa kwake 2019
- Mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), Azory Gwanda apotea siku 10 na hajulikani alipo
- Mhariri Mtendaji wa Gazeti la MwanaHALISI, Saed Kubenea avamiwa na kumwagiwa tindikali akiwa ofisini kwake
- Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA
- Absalom Kibanda (Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri) avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa
- Mwandishi wa Watetezi TV mbaroni kwa madai ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni juu ya watuhumiwa kulazimishwa kulawitiana Kituo cha Polisi
- Mwandishi wa Mwananchi Jesse Mikofu ashambuliwa na askari akitekeleza majukumu yake
- Mwandishi wa Habari, Kazimbaya Makwega ashikiliwa na Polisi, asafirishwa kutoka Mwanza hadi Dodoma
- Mchora katuni Opptertus John Fwema ashikiliwa na Polisi kwa Makosa ya Mtandao