CHADEMA INAMSALITI BEN SAA NANE: TAHADHALI KWA VIJANA WENGINE
Toka kutoweka kwa Ben Saanane kuripotiwe sikuwahi kuandika chochote zaidi ya maoni machache kwenye maandiko ya watu wengine katika mtandao wa “facebook”, na zaidi kusoma kupitia JF, na mitandao kadha wa kadha. Sikufanya hivyo kwa sababu, mosi suala la uhai wa mtu ni suala nyeti sana, na kulifanyia siasa ni ishara ya ukosefu wa ustaarabu, maana ni jambo linaloiumiza familia sana na wote walio na mahusiano ya karibu na Ben.
KUTOWEKA KUTUMIWA KISIASA
Kwa mara ya kwanza nimesikia kikundi kinachoitwa UTG, ambacho kimemtambulisha Malisa kama Mwenyekiti wake na Ben Saanane kama Katibu wa hicho kikundi, na viongozi wengine wa hicho kikundi ni wanachadema kindakindaki. Lakini wakasema hawafungamani na chama chochote (naona wana mioyo miwili, wa kufungamana na chama na ule usiofungamana na chama).
Katika kurasa za vijana hao za facebook walikuwa wakihusisha kupotea kwa Ben na ukosoaji wake wa PHD ya Mh. Rais, Dr. John Pombe Magufuli. Wakisema mtu mwenye IQ kubwa hadi ya kuhoji PHD ya Rais awezaje kupotea? Katika maoni yangu niliwaambiwa wafikiri kabla ya kuandika, kwanza kukosoa jambo lolote hakuhitaji IQ, hivyo nikawashauri ni kheri kuwa na akiba ya maneno na subira kuliko kukurupuka, lakini yote waliyoendelea nayo hadi mradi wa kuuza tsheti kupitia kutoweka kwa Ben twakujua. Na katika tamko lao wakatoa siku tatu ili serikali na Chadema watoe taarifa ya alipo Ben.
Siku ya tatu ya tamko la UTG, Mh. Tundu akaongea na waandishi wa habari, naye akalifanya suala hilo kisiasa na kuonyesha serikali inajua au imehusika kumteka na maneno yake hayakutofautiana sana nay a vijana wa UTG, kuwa kumkosoa Rais na serikali yake ndio kumesababisha Ndugu Saanane kupotea. Akazungumza mengi na yote twayafahamu.
NAFASI YA MWAJIRI WA BEN SAANANE NA KUTOWEKA KWAKE
Nimekuwa mtumishi wa Makao Makuu ya CHADEMA, kama Msaidizi wa Mwenyekiti wa Tiafa. Watumishi wote wako chini ya ofisi ya Katibu Mkuu, chini ya Kurugenzi ya Fedha na Utawala, ambaye Mkurugenzi wake, ni Mh. Anthony Komu (MB). Kila asubuhi lazima mtumishi afike ofisni kabla au saa mbili kamili asubuhi na anasaini kitabu cha wafanyakazi getini kwa mlinzi kabla ya kuingia ndani. Hivyo ikitokea mtumishi hajaonekana kazini, siku hiyo hiyo ofisi ya Katibu Mkuu inachukua hatua ya kujua kwa nini hujaonekana.
Na pia kwa nafasi yake kama Katibu Myeka wa Mwenyekiti, maana yake ni kwamba kila siku lazima uwasiliane na mkuu wako wa kazi, akupangie majukumu au umpe taarifa ya majukumu uliyotekeleza na kadhalika, kutoweka kwa mtu wa namna hiyo hadi wiki tatu hujatoa taarifa, si polisi tu bali hata kwa wazazi kunazua shaka ya uhusika wako katika sakata hilo.
Kwa mujibu wa gazeti moja la siku, siku ya tatu ya Ben kutoonekana nyumbani, mmiliki wa nyumba anayoishi alienda makao makuu ya CHADEMA na kuulizia kama wanajua alipo maana hajamuona siku tatu na simu zake hazipatikani, wao wakamjibu hawajui na inavyodhihirika hawakuchukua hatua yoyote.
Kwa msingi wa mazingira haya kuna ishara kubwa sana kuwa kutoweka kwa Ben Saanane ni kazi ya ndani ya chama na haswa hao viongozi wakuu na walitaka kulitumia hilo tukio kwa manufaa yao ya kisiasa.
KWA NINI NAWAZA CHADEMA SASA INAMSALITI BEN?
Jana, Mwanahalisionline.com wamesema Ben yupo, anaonekana kwenye vijiwe vya kahawa na kwa marafiki zake na haendi ofisini wala nyumbani. Huku likisema limemnukuu mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CHADEMA, ambaye hawakumtaja akisema huo ni mkakati binafsi wa Ben wa kujitafutia umaarufu ili kupata nafasi za uongozi.
Sikumbuki kuwahi kuona gazeti lolote likitoa dokezo la habari watakayoitoa wiki inayofuata. Pia gazeti hili tunafahamu linamilikiwa na Mkurugenzi wa fedha na Utawala wa Chadema, na pia Mbunge wa Ubungo, Mh. Said Kubenea. Na ma ra zote limetumika kama propaganda mashine ya CHADEMA, na limetumika kuwachafua na kuwasafisha watu kadhaa kisiasa kwa manufaa ya wamiliki na chama chao.
Ukisoma katikati ya mistari utagundua kwamba, viongozi hao wakuu wa CHADEMA walikubaliana na Ben kuwa ajifiche na wafanyie tukio hilo siasa, kumbuka walienda ziara Ulaya na malalamiko yao yalikuwa ya kukandamizwa na kutekwa. Kuna kila dalili sasa jambo hilo limewageuka, maana watu wengine pia wanaweza tumia akili zao na kufikiri nje ya sanduku.
Sasa kwa kuogopa tukio hilo kugeuka, sasa wameanza kuwaandaa watu kuwa Ben kajificha mwenyewe kwa manufaa ya kisiasa, kwa wiki nzima watu wakisubiri gazeti la Mwanahalisi hiyo jumatatu litoe taarifa kamili. Tayari wameshaanza kuonyesha kaijificha kwa sababu ana tamaa ya vyeo na yuko tayari kufanya lolote kupanda cheo. Pamoja na kusingle out ili msalaba uwe juu yake, huo pia utaendana na mkakati wa kusitisha ajira na career yake ndani ya CHADEMA ili hata akiamua kusema ukweli basi wajue ni kwa sababu kaondolewa nafasi yake na sasa anaongea kama mkosaji.
Kwa hiyo habari hiyo ya Mwanahalisi ni mkakati wa wao kujisafisha na kumuangushia Ben jumba bovu, ili kama ni kushitakiwa na ashitakiwe yeye kwa ulaghai alioufanya.
Na sipati picha habari hiyo ingeandikwa na gazeti la uhuru, hadi leo mitandao ya kijamii ingejaza server kwa makombora kutoka kwa mashabiki wasiofikiria ambao wamebatizwa jina la nyumbu kwa uwezo wa kuona, kutafakari na kutenda mambo.
ONYO KWA VIJANA
Vijana wengi sana wanatumika vibaya kisiasa na mwisho wanakuwa desperate na kutelekezwa, lazima kuwa makini na viongozi wengi wa vyama hasa vya upinzani. Tumewaona wengi wakibeba mikoba na hadi wengine wakisahau kuandaa maisha yao ya kesho, wakitumika kama ngazi za wao kupanda huku wakipanda wanawaacha chini. Matukio haya yatupe fikra na namna za kuwafanya hawa viongozi pia wawajibike, tofauti na hapo utatumika na mwisho wa siku analoenda kufanyiwa Ben nawe utafanyiwa. Mwenye sikio na asikie, mwenye jicho na atazame.
NAWATAKIA KHERI YA MWAKA MPYA NA UKOMAVU WA FIKRA 2017
Deo Meck.