Mwanahalisi: Nchimbi agoma kujiuzulu

Mwanahalisi: Nchimbi agoma kujiuzulu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Emmanuel Nchimbi, "amegoma kujiuzulu," kwa mujibu wa gazeti la Mwanahalisi.

Taarifa mikononi mwa gazeti hilo zinasema, Dk. Nchimbi amekuwa akikabiliwa na shinikizo la kumtaka kujiuzulu wadhifa wake, kufuatia kuibuka kwa madai ya kutoelewana na bosi wake, kuchonganisha chama chake na wananchi, kutoa kauli zinazozusha taharuki kwa jamii na kuondosha umoja serikalini.

Chanzo: Mwanahalisi.
Mkuu Para,@parabolic, asante kwa taarifa hii, ila Masikini rafiki yangu Kubenea na gazeti lake la Mwanahalisi, anakwenda kufungiwa tena kwa kuripoti habari za kweli za siri za vikao vya chama, iwapo chama kitakanusha hivyo Kubenea na gazeti lake la Mwanahalisi, kufungiwa kwa kuchapisha habari za ‘uongo’ na ‘uzushi’ wa ‘kulisha watu maneno’!.

Kwa kawaida ya vikao vya CCM,baada ya kikao,Mwenezi hutoa taarifa rasmi ya kikao, na uamuzi wa mwanachama wake yeyote kuitwa kamati ya maadili, hutolewa taarifa. Kwa vile mpaka sasa hakuna taarifa yoyote rasmi kutoka CCM, ya mwanachama yeyote wa CCM kuitwa kamati ya maadili, hii maana yake, CCM wameamua kufanya siri, hivyo taarifa hii ya gazeti la Mwanahalisi, itachukuliwa kuwa ni taarifa ya uongo, umbea na uzushi” , hakuna namna Kubenea na gazeti lake la Mwanahalisi, atakiepuka kikombe hiki!.

Hili tutakumbashana mbele ya safari.

P
 
1786320138002.jpeg
1786320138002.jpeg



View: https://web.facebook.com/KipanyaMasoud/posts/pfbid029tdcZFz1aD1h9MP9V4pwefo2umt3jzJCQnwiS8NMo94VxE2Bqecm4YzbnBosxUewl

Comments zinajisema
 
Mkuu Para,@parabolic, asante kwa taarifa hii6, masikini rafiki yangu Kubenea na gazeti lake la Mwanahalisi, anakwenda kufungiwa tena kwa kuripoti habari za uongo na uzushi wa kulisha watu maneno!.

Kwa kawaida ya vikao vya CCM,baada ya kikao,Mwenezi hutoa taarifa ya kikao, na uamuzi wa mtu kuitwa kamati ya maadili, hutolewa taarifa. Kwa vile mpaka sasa hakuna taarifa yoyote rasmi kutoka CCM, mtu kufikishwa maadili, hii maana yake taarifa hii ni taarifa ya umbea na uzishi.

P
Hii ndio story iliyomponza Mwanahalisi.
P
 
Hii ndio story iliyomponza Mwanahalisi.
P

Kaka yangu P ulikuwa mbele ya Muda

jukwaani kuna vichwa maji wengi wakiona taarifa yoyote wanaimeza kama ilivyo👈

lkn wenye uweledi wataichunguza kwanza iyo taarifa
Mana sio Jambo dogo kuombwa Kiongozi mwenye hadhi kubwa kama yule Immanuel Nchimbi kujiuzulu

Ndio tuseme wapo mitandaoni
kupika MAJUNGU tu☠️✍️
 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Emmanuel Nchimbi, "amegoma kujiuzulu," kwa mujibu wa gazeti la Mwanahalisi.

Taarifa mikononi mwa gazeti hilo zinasema, Dk. Nchimbi amekuwa akikabiliwa na shinikizo la kumtaka kujiuzulu wadhifa wake, kufuatia kuibuka kwa madai ya kutoelewana na bosi wake, kuchonganisha chama chake na wananchi, kutoa kauli zinazozusha taharuki kwa jamii na kuondosha umoja serikalini.

"Huyu bwana amekuwa katika shinikizo kubwa la kumtaka ajiuzulu, lakini amekataa kuachia ngazi. Amesema, hana kosa na hajatenda kosa lolote linalomfanya afikie uamuzi huo," kimeeleza chanzo cha taarifa kinachofahamu kwa undani suala hilo.

Alipoulizwa iwapo kuna uwezekano wa Dk. Nchimbi kuridhia kujiuzulu, mtoa taarifa huyo amesema,

"...kwa jinsi ninavyomfahamu, sioni kama hilo litawezekana. Ninamfahamu vizuri Nchimbi. Simwoni akichukua uamuzi huo.

Bali aliyekuwa kiongozi mwandamizi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sasa ni mjumbe wa Halmashauri ya Taifa (NEC) ya chama hicho, amemweleza mwandishi wa gazeti hilo kuwa hakuna namna ambayo Makamu wa Rais Dk. Emmanuel Nchimbi anaweza kusalimika kuondolewa kwenye wadhifa wake.

"Amesha elekezwa kibla. Ni lazima atachinjwa. Ninavyoifahamu CCM, uwezekano wa Nchimbi, kujinasua na kitanzi hiki ni mdogo sana," ameeleza mwanasiasa huyo.

Anayetajwa kumfikishia Makamu wa Rais ujumbe wa kujiuzulu ni kigogo mmoja mwandamizi serikalini. anayedaiwa kuwa yuko karibu na kiongozi huyo.

Taarifa hizi zimepatikana, wiki moja, baada ya wajumbe wa NEC, waliokutana mjini Unguja, kuridhia pendekezo la kumfikisha Makamu wa Rais huyo, kwenye Kamati ya Maadili.

Hoja ya kutaka Dk. Nchimbi kufikishwa Kamati ya Maadili, illtolewa na Paul Makonda, mjumbe wa NEC, kupitia kapu la wabunge wa CCM.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Makonda alisema, “Mheshimiwa mwenyekiti, huyu Emmanuel Nchimbi, anatuvuruga sana. Amekuwa akitoa kauli zinazokwenda kinyume na mwelekeo wa serikali na chama chetu.”

Akaongeza, "Ninayo mifano zaidi ya sabini, lakini kwa leo, nitataja mitatu. Moja, ni kauli yake ya juzi ya kutaka wananchi wapambane kupata Katiba mpya."

Akahoji, "Unawataka wananchi wapambane kupata Katiba mpya, ili iweje na wapambane na nani?”

Alisema, akiwa ziarani nchini Ufaransa alikutana na kiongozi mmoja wa viongozi wanaongoza mashirika ya kimataifa na kumweleza kuwa Maria Sarungi, mwanaharakati wa Tanzania aishiye uhamishoni nchini Kenya, alimhakishia kuwa amepata ushahidi wa mauaji yaliyotokea nchini.

Alisema, "Mwenyekiti, mimi nilikuwa kule Ufaransa. Nilikutana na kiongozi mmoja wa kimataifa, akanithibitishia kwamba huyu Maria Sarungi, ambaye Emmanuel Nchimbi, anasema anatamani kufanya naye kazi, amemhakikishia kuwa anao ushahidi wa matukio ya 29 Oktoba.

Akaongeza, "Kauli za Emmanuel Nchimbi, zinanipa wakati mgumu sana wa kutekeleza majukumu yangu ya uwaziri. Unawezaje kusema unatamani kufanya kazi na watu wanaovuruga serikali kila siku? Haiwezekani. Hayo mapenzi yanatoka wapi kama siyo kutaka kutuvuruga? Naomba huyu Emmanuel Nchimbi, afikishwe Kamati ya Maadili.”

Makonda alienda mbali zaidi akasema, kitendo cha Nchimbi, wakati akiwa katibu mkuu wa chama hicho, kumtetea John Mnyika, katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakati wa mauaji wa Ally Mohamed Kibao, kilichangia kuzorotesha uchunguzi.

“Mheshimiwa mwenyekiti, Nchimbi akiwa katibu mkuu wa CCM, aliwahi kutoa kauli tata iliyomtetea Mnyika, kwamba hahusiki na mauail ya Kibao. Eti anavyomfahamu Mnyika, hata panya anamwogopa. Kauli yake hii, imesababisha hata vyombo vya dola, kushindwa kufanya uchunguzi,” alieleza.

Ni baada ya kauli ya Makonda, ndipo mwenyekiti wa kikao, Rais Samia akahoji wajumbe na kuridhia hoja ya kumfikisha Makamu wa Rais, Kamati ya Maadili, inayoongozwa na Stephen Wassira, makamu mwenyekiti wa chama hicho, Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa katiba ya CCM, mara baada ya Kamati ya Maadili kumaliza kumhoji Dk. Nchimbi, Sektarieti ya chama hicho, Itawasilisha taarifa na mapendekezo, mbele ya Kamati Kuu (CC).

Nayo Kamati Kuu, baada ya kupokea na kujadili mapendekezo kupokea ya Kamati ya Maadili, yaweza kufikisha suala hilo NEC na kwamba, iwapo bado Dk. Nchimbi ataendelea kung'ang'ania kiti chake, huku wanaotaka ang'olewe wakiendelea na msimamo huo, suala hilo linaweza kufikia uamuzi wa kupigiwa kura.

Miongoni mwa adhabu anazoweza kupewa, ikiwa atapatikana na hatia, ni pamoja na onyo, karipio au kufukuzwa uanachama.

Hata hivyo, Ibara ya 103 ya Katiba ya chama hicho, pamoja na kuwa na uwezo wa kumwachisha au kumfukuza uongozi, kiongozi yeyote wa chama hicho, lakini uteuzi wa mwisho wa kiongozi huyo, uwe umefanywa na NEC.

Uteuzi wa Makamu wa Rais ambaye alikuwa mgombea mwenza wa Rais aliyepo madarakani, hufanywa na mkutano mkuu, jambo linaloweza kusababisha sakata la Nchimbi kufikishwa kwenye mkutano mkuu

Ibara ya 128 ya katiba ya chama hicho, imeweka utaratibu wa kufikia uamuzi. Kwamba utafikiwa kwa kufuata makubaliano ya jumla au wingi wa kura za wajumbe waliohudhuria na kupiga kura za siri.

Aidha, kabla ya suala hili kufikishwa kamati kuu, linaweza kufikishwa kwenye Baraza la Ushauri la Viongozi Wakuu Wastaafu.

Baraza hilo linaloundwa na marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano na Zanzibar, pamoja na makamu wa wenyeviti wastaafu wa chama hicho, limepewa mamlaka ya kutoa ushauri kwa CCM na serikali zake.

Vile vile, Ibara ya 123 (3) ya Katiba ya CCM inasema, "Kwa madhumuni ya kutoa ushauri katika jambo mahususi, wajumbe wa baraza hilo, wanaweza kualikwa, ama wote kwa pamoja au kwa mwakilishi wao, kuhudhuria vikao vya ngazi za taifa pale ambapo busara zao zitahitajika. hususan katika masuala muhimu na nyeti

Akifungua mkutano mkuu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRDC), jijini Dar es Salaam, Dk. Nchimbi aliwataka wananchi, kupigania upatikanaji wa Katiba mpya

Alisema, kama angepewa nafasi ya kuwaambia Watanzania jambo moja tu, angewaambia, "Pambaneni mpate Katiba mpya,” na akaongeza, haki za binadamu si suala la sheria pekee, bali linagusa maisha ya kila siku ya kila Mtanzania.

Kauli ya Makamu wa Rais, imekuja katikati ya shinikizo la wananchi kutaka kuwepo kwa Katiba mpya na mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi, mambo yanayotajwa kuchangia kuwapo kwa maandamano ya 29 Oktoba mwaka jana.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema, hoja ya kutaka kumchomoa Nchimbi kabla ya kumaliza muda wake, inasukumwa na mbio za urais kuelekea 2030 kwa kila kundi kutaka kulidhoofisha jingine.

Huyo Makonda, ambaye pia ni Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni, inadaiwa yuko kambi ya urais ya Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba.

Tayari hoja ya sasa, imeanza kuchukua sura ya U-Zanzibar na U-Tanganyika, kufuatia madai ya usaliti dhidi ya Dk. Nchimbi, kuibuliwa kwa mara ya kwanza na Simai Mohamed Said, mbunge wa Bunge la Muungano, kutokea Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Akichangia bajeti ya wizara ya fedha, bungeni mjini Dodoma, tarehe 5 Juni 2026b, mwakilishi huyo wa Tunguu, Unguja, alidai kuwa ndani ya serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, "kuna Yuda anayesaliti dhamira yake.

Simai hakutaja jina la aliyemuita Yuda, lakini wote waliomkabili mbunge huyo, akiwamo mbunge wa Tarime Vijijini (CCM), Mwita Waitara na Jacqueline Msongozi, mbunge wa Viti Maalum, kutokea mkoani Ruvuma, walimtaja Dk. Nchimbi.

Alisema, kiongozi huyo aliyeaminiwa na rais na kisha kugeuka Yuda, amekuwa akitumia nyumba za ibada na jina la John Magufuli, kutafuta uungwaji mkono kwenye safari yake ya kisiasa, hali Inayotajwa kuwa chama hicho, kina wakati mgumu…

Chanzo: Mwanahalisi.

Pia soma: Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya
Kwa hio hii ina maana mwanahalisi ilifungiwa sababu tu,ulisema ukweli?
 
Mkuu Para,@parabolic, asante kwa taarifa hii, ila Masikini rafiki yangu Kubenea na gazeti lake la Mwanahalisi, anakwenda kufungiwa tena kwa kuripoti habari za kweli za siri za vikao vya chama, iwapo chama kitakanusha hivyo Kubenea na gazeti lake la Mwanahalisi, kufungiwa kwa kuchapisha habari za ‘uongo’ na ‘uzushi’ wa ‘kulisha watu maneno’!.

Kwa kawaida ya vikao vya CCM,baada ya kikao,Mwenezi hutoa taarifa rasmi ya kikao, na uamuzi wa mwanachama wake yeyote kuitwa kamati ya maadili, hutolewa taarifa. Kwa vile mpaka sasa hakuna taarifa yoyote rasmi kutoka CCM, ya mwanachama yeyote wa CCM kuitwa kamati ya maadili, hii maana yake, taarifa hii ya gazeti la Mwanahalisi, itachukuliwa kuwa ni taarifa ya umbea na uzushi” Hakuna namna Kubenea na gazeti lake la Mwanahalisi, atakiepuka kikombe hiki!.

Hili tutakumbashana mbele ya safari.

P
Bado ni uzushi?
 
Hapana.

Mimi ningempa sanasana 70%.

kaziacha sehemu kadhaa zikining'inia bila ya maelezo ya kutosha..

Kwa mfano:

Huo mtiririko wa vikao, kuanzia Kamati ya Maadili, hadi jambo linavyoweza kufikishwa kwenye Halmashauri Kuu ya Chama haikunyooka sawasawa ikaeleweka. Ni vigezo vipi vitalifikisha jambo huko juu hadi kupigiwa kura na wajumbe.

Hata maelezo ya yaliyosemwa na Makonda, yanaonyesha kasoro kubwa ya uwasilishaji wa habari.

Huyo anayemfahamu Nchimbi, na yeye kaokotwa mahala tu na kutoa taarifa?

Kuna upungufu mkubwa ndani ya taarifa hiyo, hata hiyo sabini ninayotoa mimi naona nimefuata tu mkumbo wako.

Hii siyo taarifa ya kuitegemea sana.
Kuna mdau ka-like hadi kanirudisha huku.
Ulikua sahihi kwa namna fulani,mchakato umeenda tofauti kweli
 
Mtasubiri sana kujiuzulu Kwa hiari

Nani Yuko tayari kubebeshwa lawama zote za mauaji ?

Nani Yuko tayari kujikabidhi Icc PEKEE yake ?

Utakuwa usaliti Kwa kundi lote na mtandao na washauri wake

Nani Yuko tayari kuachilia mpini ashile MAKALI ya Upanga

Hata maboresho ya katiba yatafanyika kulinda au kuangeza muda wa kujilinda Hadi kuhakisha hakuna nguchiro yoyote inayofuatilia kundi husika na mtandao wake

Hizo ndoto za kujiuzulu Kwa hiari ni ndoto za mazuzu ya nchi ya kusadikika

Anyway Kwa mfano aamue kujiuzulu Leo Hilo kundi lake wataacha salama sembuse vyombo

Hukuna mtu wa kujitoa kafara Kwa ajili ya wajinga wanaweza KUBADILISHIWA mwelekeo TU na ujauzito wa Zichu au mimba ya Wima.

Lisu PEKEE yake ndo ameamua kuwatetea wajinga wa nchi ya kusadikika.

Wakati lisu angeweza kwenda TU pale jikoni akaingia makubaliano Akala bii zake za kutosha akaenda kula Maisha ughaibuni huko na familia yake

Mbowe alishtuka dk za mwisho kundi la kubwa la raia ni wajinga kuhusu haki zao na hawana utayari wa kutosha kuzitetea
Nimependa sana andiko lako lote isipokuwa mstari huo wa mwisho..

Naamini tukiujadili kati yetu tutakubaliana kwamba hayo uliyoandika hapo siyo kweli.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Emmanuel Nchimbi, "amegoma kujiuzulu," kwa mujibu wa gazeti la Mwanahalisi.
Mkuu Parabolic , asante tena kwa taarifa hii. Gazeti hili lisingefungiwa, saa hizi taifa lingeishapatiwa taarifa, VP Nchimbi amefukuzwa chama kwa kufanya kosa gani, we are on the dark, na ni kama hatuna any credible media, kufanya IJ, ya what happened!.
P
 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Emmanuel Nchimbi, "amegoma kujiuzulu," kwa mujibu wa gazeti la Mwanahalisi.

Taarifa mikononi mwa gazeti hilo zinasema, Dk. Nchimbi amekuwa akikabiliwa na shinikizo la kumtaka kujiuzulu wadhifa wake, kufuatia kuibuka kwa madai ya kutoelewana na bosi wake, kuchonganisha chama chake na wananchi, kutoa kauli zinazozusha taharuki kwa jamii na kuondosha umoja serikalini.

"Huyu bwana amekuwa katika shinikizo kubwa la kumtaka ajiuzulu, lakini amekataa kuachia ngazi. Amesema, hana kosa na hajatenda kosa lolote linalomfanya afikie uamuzi huo," kimeeleza chanzo cha taarifa kinachofahamu kwa undani suala hilo.

Alipoulizwa iwapo kuna uwezekano wa Dk. Nchimbi kuridhia kujiuzulu, mtoa taarifa huyo amesema,

"...kwa jinsi ninavyomfahamu, sioni kama hilo litawezekana. Ninamfahamu vizuri Nchimbi. Simwoni akichukua uamuzi huo.

Bali aliyekuwa kiongozi mwandamizi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sasa ni mjumbe wa Halmashauri ya Taifa (NEC) ya chama hicho, amemweleza mwandishi wa gazeti hilo kuwa hakuna namna ambayo Makamu wa Rais Dk. Emmanuel Nchimbi anaweza kusalimika kuondolewa kwenye wadhifa wake.

"Amesha elekezwa kibla. Ni lazima atachinjwa. Ninavyoifahamu CCM, uwezekano wa Nchimbi, kujinasua na kitanzi hiki ni mdogo sana," ameeleza mwanasiasa huyo.

Anayetajwa kumfikishia Makamu wa Rais ujumbe wa kujiuzulu ni kigogo mmoja mwandamizi serikalini. anayedaiwa kuwa yuko karibu na kiongozi huyo.

Taarifa hizi zimepatikana, wiki moja, baada ya wajumbe wa NEC, waliokutana mjini Unguja, kuridhia pendekezo la kumfikisha Makamu wa Rais huyo, kwenye Kamati ya Maadili.

Hoja ya kutaka Dk. Nchimbi kufikishwa Kamati ya Maadili, illtolewa na Paul Makonda, mjumbe wa NEC, kupitia kapu la wabunge wa CCM.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Makonda alisema, “Mheshimiwa mwenyekiti, huyu Emmanuel Nchimbi, anatuvuruga sana. Amekuwa akitoa kauli zinazokwenda kinyume na mwelekeo wa serikali na chama chetu.”

Akaongeza, "Ninayo mifano zaidi ya sabini, lakini kwa leo, nitataja mitatu. Moja, ni kauli yake ya juzi ya kutaka wananchi wapambane kupata Katiba mpya."

Akahoji, "Unawataka wananchi wapambane kupata Katiba mpya, ili iweje na wapambane na nani?”

Alisema, akiwa ziarani nchini Ufaransa alikutana na kiongozi mmoja wa viongozi wanaongoza mashirika ya kimataifa na kumweleza kuwa Maria Sarungi, mwanaharakati wa Tanzania aishiye uhamishoni nchini Kenya, alimhakishia kuwa amepata ushahidi wa mauaji yaliyotokea nchini.

Alisema, "Mwenyekiti, mimi nilikuwa kule Ufaransa. Nilikutana na kiongozi mmoja wa kimataifa, akanithibitishia kwamba huyu Maria Sarungi, ambaye Emmanuel Nchimbi, anasema anatamani kufanya naye kazi, amemhakikishia kuwa anao ushahidi wa matukio ya 29 Oktoba.

Akaongeza, "Kauli za Emmanuel Nchimbi, zinanipa wakati mgumu sana wa kutekeleza majukumu yangu ya uwaziri. Unawezaje kusema unatamani kufanya kazi na watu wanaovuruga serikali kila siku? Haiwezekani. Hayo mapenzi yanatoka wapi kama siyo kutaka kutuvuruga? Naomba huyu Emmanuel Nchimbi, afikishwe Kamati ya Maadili.”

Makonda alienda mbali zaidi akasema, kitendo cha Nchimbi, wakati akiwa katibu mkuu wa chama hicho, kumtetea John Mnyika, katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakati wa mauaji wa Ally Mohamed Kibao, kilichangia kuzorotesha uchunguzi.

“Mheshimiwa mwenyekiti, Nchimbi akiwa katibu mkuu wa CCM, aliwahi kutoa kauli tata iliyomtetea Mnyika, kwamba hahusiki na mauail ya Kibao. Eti anavyomfahamu Mnyika, hata panya anamwogopa. Kauli yake hii, imesababisha hata vyombo vya dola, kushindwa kufanya uchunguzi,” alieleza.

Ni baada ya kauli ya Makonda, ndipo mwenyekiti wa kikao, Rais Samia akahoji wajumbe na kuridhia hoja ya kumfikisha Makamu wa Rais, Kamati ya Maadili, inayoongozwa na Stephen Wassira, makamu mwenyekiti wa chama hicho, Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa katiba ya CCM, mara baada ya Kamati ya Maadili kumaliza kumhoji Dk. Nchimbi, Sektarieti ya chama hicho, Itawasilisha taarifa na mapendekezo, mbele ya Kamati Kuu (CC).

Nayo Kamati Kuu, baada ya kupokea na kujadili mapendekezo kupokea ya Kamati ya Maadili, yaweza kufikisha suala hilo NEC na kwamba, iwapo bado Dk. Nchimbi ataendelea kung'ang'ania kiti chake, huku wanaotaka ang'olewe wakiendelea na msimamo huo, suala hilo linaweza kufikia uamuzi wa kupigiwa kura.

Miongoni mwa adhabu anazoweza kupewa, ikiwa atapatikana na hatia, ni pamoja na onyo, karipio au kufukuzwa uanachama.

Hata hivyo, Ibara ya 103 ya Katiba ya chama hicho, pamoja na kuwa na uwezo wa kumwachisha au kumfukuza uongozi, kiongozi yeyote wa chama hicho, lakini uteuzi wa mwisho wa kiongozi huyo, uwe umefanywa na NEC.

Uteuzi wa Makamu wa Rais ambaye alikuwa mgombea mwenza wa Rais aliyepo madarakani, hufanywa na mkutano mkuu, jambo linaloweza kusababisha sakata la Nchimbi kufikishwa kwenye mkutano mkuu

Ibara ya 128 ya katiba ya chama hicho, imeweka utaratibu wa kufikia uamuzi. Kwamba utafikiwa kwa kufuata makubaliano ya jumla au wingi wa kura za wajumbe waliohudhuria na kupiga kura za siri.

Aidha, kabla ya suala hili kufikishwa kamati kuu, linaweza kufikishwa kwenye Baraza la Ushauri la Viongozi Wakuu Wastaafu.

Baraza hilo linaloundwa na marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano na Zanzibar, pamoja na makamu wa wenyeviti wastaafu wa chama hicho, limepewa mamlaka ya kutoa ushauri kwa CCM na serikali zake.

Vile vile, Ibara ya 123 (3) ya Katiba ya CCM inasema, "Kwa madhumuni ya kutoa ushauri katika jambo mahususi, wajumbe wa baraza hilo, wanaweza kualikwa, ama wote kwa pamoja au kwa mwakilishi wao, kuhudhuria vikao vya ngazi za taifa pale ambapo busara zao zitahitajika. hususan katika masuala muhimu na nyeti

Akifungua mkutano mkuu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRDC), jijini Dar es Salaam, Dk. Nchimbi aliwataka wananchi, kupigania upatikanaji wa Katiba mpya

Alisema, kama angepewa nafasi ya kuwaambia Watanzania jambo moja tu, angewaambia, "Pambaneni mpate Katiba mpya,” na akaongeza, haki za binadamu si suala la sheria pekee, bali linagusa maisha ya kila siku ya kila Mtanzania.

Kauli ya Makamu wa Rais, imekuja katikati ya shinikizo la wananchi kutaka kuwepo kwa Katiba mpya na mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi, mambo yanayotajwa kuchangia kuwapo kwa maandamano ya 29 Oktoba mwaka jana.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema, hoja ya kutaka kumchomoa Nchimbi kabla ya kumaliza muda wake, inasukumwa na mbio za urais kuelekea 2030 kwa kila kundi kutaka kulidhoofisha jingine.

Huyo Makonda, ambaye pia ni Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni, inadaiwa yuko kambi ya urais ya Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba.

Tayari hoja ya sasa, imeanza kuchukua sura ya U-Zanzibar na U-Tanganyika, kufuatia madai ya usaliti dhidi ya Dk. Nchimbi, kuibuliwa kwa mara ya kwanza na Simai Mohamed Said, mbunge wa Bunge la Muungano, kutokea Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Akichangia bajeti ya wizara ya fedha, bungeni mjini Dodoma, tarehe 5 Juni 2026b, mwakilishi huyo wa Tunguu, Unguja, alidai kuwa ndani ya serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, "kuna Yuda anayesaliti dhamira yake.

Simai hakutaja jina la aliyemuita Yuda, lakini wote waliomkabili mbunge huyo, akiwamo mbunge wa Tarime Vijijini (CCM), Mwita Waitara na Jacqueline Msongozi, mbunge wa Viti Maalum, kutokea mkoani Ruvuma, walimtaja Dk. Nchimbi.

Alisema, kiongozi huyo aliyeaminiwa na rais na kisha kugeuka Yuda, amekuwa akitumia nyumba za ibada na jina la John Magufuli, kutafuta uungwaji mkono kwenye safari yake ya kisiasa, hali Inayotajwa kuwa chama hicho, kina wakati mgumu…

Chanzo: Mwanahalisi.

Pia soma: Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya
Para Nchimbi yupo wapi mpaka mda huu?
 
Back
Top Bottom