Vyama vyote Tanzania hili hawalitaki ila ngoja niongelee vyama hivi viwili kwanza. CCM, hawa katiba haikatazi ila wamejiwekea tamaduni tu ndani ya chama na ukithubutu ku challenge hilo basi jiandae kweli maana unaweza ukawa ndio mwisho wako kisiasa mnakumbuka yule aliyechukuwa form wakati wa Kikwete? japo CCM tamaduni hizi ni awamu 2 tu miaka kumi mwenyekiti mpya anakuja.
Chadema, hawa ukitia nia yakutaka kum challenge mwenyekiti chamoto utakiona utahama mwenyewe na utaanzisha chama chako yalimkuta Zitto. Hawa hatujui ni tamaduni au katiba ila ukijitosa tu ujue ndio mwisho wako umefika.
TFF, huko ukitaka tu basi utaletewe zengwe la kesi na utafungiwa maisha kushiriki kwenye soka...