Mzee
Pascal Mayalla, kila "taboo" huwa inafikia ukomo wake nyakati na majira yake yanapowadia...
Kwa kipindi cha miezi 12 ijayo, utashuhudia "taboos" nyingi zikifikia ukomo wake na kubatilishwa. Mojawapo ni hii ya "U - Rais wa mserereko."
Zipo factors na indicators za kutosha na zinazojitosheleza kwa zaidi ya 100% kuwa huyu mama alikuwa ni RAIS WA MPITO tu na mwisho wake ni miezi michache ijayo;
MOSI; Mzanzibari hawezi kuwa Rais wa Tanganyika tena. Hali ilivyo sasa kwa Tanganyika kuongozwa na raia wa kigeni toka nchi ya Zanzibar inaudhi na kumkera kila Mtanganyika bila kujali itikadi ya kisiasa tulizonazo. Tusiambiane habari za muungano huu wa kinadharia kati ya Tanganyika na Zanzibar. Hii ni nadharia ya hovyo iliyokwisha kupitwa na wakati na inayopaswa kuondoka na kupotelea mbali huko pamoja na waasisi wake wazee wa kizazi cha Hayati Julius K. Nyerere...!
Ni afadhali mara milioni moja tuwe na Rais Mtanganyika wa sampuli ya John Pombe Magufuli (lakini Mtanganyika) kuliko ujinga na uhayawani wa kukubali kutawaliwa na Rais wa nchi ya kigeni...!!
PILI; Ukiachilia mbali u - Zanzibari wake, huyu binadamu ni mwanamke. Itoshe tu kusema kwa ufupi sana kuwa, nchi hii ya Tanganyika si kama Marekani (USA) yenye mifumo thabiti ya udhibiti (i.e CHECKS & BALANCE) yenye full mandatory authority ya kufuatilia na kudhibiti tabia na mienendo ya ma - Rais wanapokuwa ktk ofisi kuu ya nchi....
Chini ya mfumo huu thabiti wa CHECKS & BALANCE wa USA, ipo possibility ya karibu 50% ya mwanamke kuwa Rais na akaongoza kwa mafanikio. Na bila shaka Kamala Harris wa chama cha Democrats anaweza kumshinda Donald Trump wa Republican mapema wiki ijayo na kuwa Rais mwanamke wa kwanza USA...
Hapa Bongo - Tanganyika, bado wakati huo haujafika kuruhusu hili. Lilifanyika kosa huyu akapenya na kujikuta tu hapo. Haipaswi kuliendeleza kosa hili wakati fursa ya kurekebisha imepatikana...
Na for sure kabisa, kwa miaka hii minne tumethibisha pasipo shaka kuwa, nchi hii haiwezi kuwa chini ya uongozi wa mwanamke kwa sababu za kiasili (natural reasons) na zile za udhaifu wa mifumo yetu ya kisheria na kikatiba inayoruhusu hooligans kutumia udhaifu wa asili (natural weakness) wa mwanamke kuingilia maamuzi ya nchi kwa maslahi binafsi ya majambazi haya. Na ndiyo maana kama nchi tuko hivi tulivyo leo..!
TATU; Huyu Rais mwanamke ni mwana - CCM. Na ishara ziko wazi sana kuwa, mwisho wa CCM umekwishakufika na mwisho huu utahitimishwa kwa mikono ya wana CCM wenyewe kama ambavyo KANU ya Kenya ilivyojimaliza yenyewe. Ishara ziko wazi mno kwa waonaji na watambuzi wa mambo...
KWA HIYO; hawa wanaoijiandaa kuvunja "taboo" ya hiki ulichokiita "u - Rais wa mserereko", eleweni kuwa ni sehemu ya utimilifu wa mwisho na amini usiamini ITAKUWA HIVYO....!!!