Mwanaharakati Albanie Marcossy atoweka kunusuru maisha yake

Mwanaharakati Albanie Marcossy atoweka kunusuru maisha yake

Mohamed Mtoi,inaonekana una ratiba ya kila siku ya Marcosy Albanie.Kutokukuaga siku moja tu tayari roho juu?

Mkuu Mingoi.
Uko mjini lakini inawezekana huna taarifa za kutosha! Hii habari nimeiweka jana na leo iko kwenye gazeti la Mwananchi sijui unacho kibisha ni kipi?! Kwa kukusaidia soma habari yenyewe hapa chini na jifunze kuutafuta ukweli.

Mwanaharakati
Albanie Marcossy, Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Civil and Political Right Watch (CPW) ameondoka nyumbani kwake Kimara Dar es Slaam akidai kilichomwondoa ni kupokea vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana.

Marcossy, awali aliwahi kufanya kazi kwenye Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC) ambako alikuwa mmoja wa waliopeleka mashtaka- kwenye Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa (ICC), Septemba 28, 2012 dhidi ya serikali kutokana na mauaji yenye utata ya watu 23 akiwamo Mwandishi wa habari- Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi.

Akizungumza- jana kutoka alikokimbilia,- Marcossy alisema ameamua kuikimbia nyumba yake kwa ajili ya usalama na kubainisha kuwa taarifa ya vitisho vyake aliwasilisha kwa Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRD-Coalition,) Onesmo Olengurumwa.

Olengurumwa alithibitisha kupokea taarifa hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela alipoulizwa jana alisema polisi hawana taarifa kuhusiana na kutoweka kwa mwanaharakati huyo wala kutishiwa kutokana na kutopokea taarifa yoyote kuhusiana na suala hilo .

Chanzo: mwananchi 15 Machi, 2015. Uk 8.
 
Last edited by a moderator:
hii nchi watakimbia wengi,Mungu atusaidie tu.
Halafu utamsikia mkuu wa Kaya, akiwa ziarani nje ya nchi anasema..."watanzania mlio nje ya nchi rudini nyumbani mjenge nchi yenu"....

Kauli kama hizi zinatolewa na watesaji walewale, ambao ni wepesi kusahau na wagumu kuelewa. Kubwa kwao ni kukariri tu!!!!
 
Na Frederick Katulanda | Mwananchi | Ijumaa, Marchi 15 2013

Mwanaharakati Albanie Marcossy, Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Civil and Political Right Watch (CPW) ameondoka nyumbani kwake Kimara Dar es Slaam akidai kilichomwondoa ni kupokea vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana.

Marcossy, awali aliwahi kufanya kazi kwenye Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC) ambako alikuwa mmoja wa waliopeleka mashtaka kwenye Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa (ICC), Septemba 28, 2012 dhidi ya serikali kutokana na mauaji yenye utata ya watu 23 akiwamo Mwandishi wa habari Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi.

Akizungumza jana kutoka alikokimbilia, Marcossy alisema ameamua kuikimbia nyumba yake kwa ajili ya usalama na kubainisha kuwa taarifa ya vitisho vyake aliwasilisha kwa Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRD-Coalition,) Onesmo Olengurumwa.

Olengurumwa alithibitisha kupokea taarifa hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela alipoulizwa jana alisema polisi hawana taarifa kuhusiana na kutoweka kwa mwanaharakati huyo wala kutishiwa kutokana na kutopokea taarifa yoyote kuhusiana na suala hilo


 
Mwanaharakati halafu unakua muoga?maajabu Helen Bi Kijo hakimbiagi mtu wala polisi.
 
Kamanda kala kona? Si abaki tu ili wakimtesa atoe tamko kama walivyomtumia yule daktari aliyeng'olewa meno bila ganzi?
 
Hivi Vitisho na Vilivyotokea ni kama vile ENZI za IDD AMIN DADA huko UGANDA... Unarudi nyumbani Unapigwa kama Chura; Unahudhuria Mikutano wanafuta wanayetaka kumdhuru na kummaliza hapo hapo;pia hakupenda viongozi wa dini fulani... walikuwa wanawateteresha kama MIHOGO... Hii style tunayotumia ni ya kizamani kweli inaonyesha anayeidhinisha sio MTAALAMU... Poleni Watanganyika... Nje ya NCHI hakuna WAKIMBIZI wengi wa KISIASA toka TANGANYIKA kuna WENGI TOKA ZANZIBAR... nadhani sasa ni wakati wa kufikiria hayo kama ni MOJA ya kuidhoofisha CCM NJE YA NCHI
 
Magamba at work na vikumbo vya 2015...... Na bado maana kutolewa kucha na meno looooooo bora kimbia mapema ila tunashukuru kwa kutusaidia kutufikishia taarifa za mauwaji yanayoendelea kwa dunia nzima
 
Halafu utamsikia mkuu wa Kaya, akiwa ziarani nje ya nchi anasema..."watanzania mlio nje ya nchi rudini nyumbani mjenge nchi yenu"....

Kauli kama hizi zinatolewa na watesaji walewale, ambao ni wepesi kusahau na wagumu kuelewa. Kubwa kwao ni kukariri tu!!!!
hii nchi inatia hasira sana inahitaji nguvu ya ziada kuiokoa. ila tusikate tamaa.
 
Mkuu. Naamini hawa manguli wanachukua hatua thabiti kuepusha macho na meno yao dhidi ya makoleo ya kina Joseph Mulundi.

Atakaye pona JF ni Invisible peke yake maana hawata muona au huenda wako naye lakini hawamuoni.

Naomba ujumbe huu umfikie na ndugu Yericko Nyerere wasije wakamzamisha kwenye kivuko cha kigamboni maana huwa anawasema CCM kwa sauti kali sana
 
mkuu naona hujawahi ingia magogoni wewe, kuna kuna timu ya vigagula pale tena iko full kama barcelona. yaani ninauhakika ungefrot mwenyewe tu.... fastjet hawezi fanya safari bila ramli kupigwa kudadek.......chezea mukulu wewe?
je bado analindwa na majini ya sheikh yahaya?
 
Yakitoka kwa waandishi na wanaharakati yatakuja kwa wabunge wa upinzani kama kina tundu lissu, mnyika , lema, zitto na wengineo. Mungu aepushie mbali. Tanzania saa hizi ni kama burundi ama rwanda.
 
Kweli wanahaki ya kuitwa pro Chadomo mambo yamejaa uzushi mtupu
 
hakika haki haiwezi kuszuiliwa na kikundi cha wahuni wachache. iwe isiwe kuna siku ukweli utajulikana tu
 
Mwanaharakati halafu unakua muoga?maajabu Helen Bi Kijo hakimbiagi mtu wala polisi.


Ulitaka afanyiwe kama Ulimboka na Kibanda ndo akimbie akiwa tayari kahasiwa. Huyu ndiye mjanja na inaonyesha yuko highly informed na halali usingizi
 
Sasa ndiyo tunashuhudia utawala dhalimu na wa mabavu wa JK.Kila auaye kwa upanga atakufa kwa upanga.
 
Back
Top Bottom