Mwanaharakati Albanie Marcossy atoweka kunusuru maisha yake

Mwanaharakati Albanie Marcossy atoweka kunusuru maisha yake

hapa JF watu wanajihami sana lakini ukweli utajulikana tu,hakuna kukumbatia madudu hapa,tanzania kwanza mambo mengine baadaye,aman na uhuru mbele chama baadaye.watanzania tubadilike ukimuona mtu anhujumu nchi mripoti hatutakii mema huyo.
 
Tunasubiria video ya wanaomfuatilia itoke.
 
Nchi ya hovyo sana hii_mtu msema kweli ndio anageuka adui wa kuwindwa,....i wish kama ningekuwa mchawi ningemroga mkw..ere na familia yake yote.
mkuu naona hujawahi ingia magogoni wewe, kuna kuna timu ya vigagula pale tena iko full kama barcelona. yaani ninauhakika ungefrot mwenyewe tu.... fastjet hawezi fanya safari bila ramli kupigwa kudadek.......chezea mukulu wewe?
 
Time will tel lazima watakuja kusema hivyo! Jamaa wana uoga sana na nguvu ya chadema!

Sasa kama Chadema wana uwezo mkubwa namna hiyo kuna hatari tukasikia Kikwete katekwa na Chadema
 
Jamani kama mwanaharakati katoweka hajulikani aliko msisema katoroka kwani hii ni hatari kabisa huenda kesha uawa!
 
Mapambano haya hayataisha hata wakiwaua baadhi ya wanaharakati wengine watayaendeleza? Mimi nimeshakutana na vitisho mara nyingi tu kupitia simu (bahati mbaya huwezi kujua vitisho uchwara na vya ukweli). Hata hivyo, mimi nimeamua kusema ukweli kwa gharama yo yote. Mtu atakayenitanguliza mbinguni ajue na yeye si mtu wa kudumu humu duniani - sote tunapita. Hatuwezi kuogopa kusema ukweli kwa sababu tunaogopa koleo ya kutolea meno au kuna kifo.
Akina Nyerere, Mandela na Nkurumah na wengineo wangekuwa waoga, Afrika isingekuwa hapa ilipo leo.

hahaha umenifurahisha eti wewe umekutana na vitisho kwa lipi ambalo umelifanya yani wewe ni harmless kabisa sasa huyo anayekutisha au anajua unavyoishi kwa kudhania wewe ni bonge la Mwanaharakati au Mwanasiasa.
Kweli siasa imevamiawa duh hadi wewe unapata vitisho
 
Kwa hiyo ukiwa na bango hilo ndiyo utafutwe kuuawa au?
Mkuu hukufuatilia kipindi cha kipima joto kinachotajwa kwenye mada hii bila shaka. Alimpa tabu sana Naibu speaker na aliushutumu wazi wazi uongozi wa bunge na hata jinsi viongozi wa serikali wanavyobehave na kuingilia bunge.......sio hicho tu ila ni mtu anayesema uovu wa serikali na taasisi zake wazi wazi. Sishangai kama amefuatiliwa kwasababu nchi hii fisadi ndo anapongezwa na mtu anayeonekana anatetea maslahi ya taifa ni adui. One day the truth shall stand......
 
Kuna ushindi katika historia ya mapambano haya baada ya umwagaji damu huu.Msiwaogope wao wauao mwili halafu hawana lingine wanaloweza kufanya.HUYU NDIYE MTAKAYEMWOGOPA,YEYE AWEZAYE KUUA MWILI NA KUITUPA ROHO YA MTU MILELE KATIKA JEHANUM!
 
Laiti tungefanya mapinduzi katika nchi hii kuliko haya yanoendelea sasa,kwasababu mtanzania yeyote yupo subject kupatwa madhara na mauti,kwasababu tu ya kusimamia anachokiamini kwa vile tu hakiwapendezi viongozi.

Mambo mabaya na ya kutisha tunafanyiwa hakuna anayejali,tumefungwa kwenye gereza la njaa kutokana na wasimamiaji wetu wakuu wa uchumi wamegeuka kuwa vibaraka wa wageni.

Na mahali walipotuweka kiuchumi hawataki tutoke maana kama njaa itakuwa si tatizo tena kwetu basi tutahangaikia usalama wetu,ambao kimsingi wao(viongozi) ndo wenye dhamana kubwa kwenye hilo.

Kwa matukio yote haya ya kina Mwakyembe,Kubenea,Ndimara,Ulimboka,Mwangosi na kadhalika vidole vyote vinaelekezwa Ikulu halafu wabongo wametulia tuli,utasikia vijikelele vya hapa na pale baada ya muda kimya,na viongozi huko wanasema watz ni wasahaulifu yatapita tu.

Sasa sijui tunangoja adhurike nani au auwawe nani ndipo tuamke. Mpaka hapa tulipofikia hii serikali tuliyonayo imepoteza uhalali wakutuongza watanzania,MAPINDUZI nikitu cha lazima sana sasa, SAA ILIYOKUBALIKA NI SASA,WAKATI WA UKOMBOZI NI SASA.

Hawa jamaa tunatakiwa kuwaondoa kisha wanatiwa hatiani kwa yote yanayofanyika sasa hakuna cha The Hague wala nini tunawafanyia hapahapa,ili iwe mfano kwa wengine watakaokuja ili angalau tupumue,kwa kweli hali ilivyo sasa ni maisha ya mashaka,wasiwasi,haipaswi kuwa hivi kwenye taifa ambalo lipo huru.

Na ni wakati huo ukifika utaona na hapa jf patabadilika sana, kwasababu wengi tutaingia hapa kwa majina yetu halisi.
 
Watatisha watu wote, hata wakiwauwa watetezi lakini ukweli utabaki. Hizo ndizo dalili za kuanguka kwa dola ni muda tu mambo yote yatakuwa wazi.
 
Something must be done. Vitisho vimezidi ila Mungu akiwa upande wetu hata wanyeje hawataweza.
 
usalama wa wanaharakati na waandishi wa habari uko mashakani
huku tukijisifu ni nchi ya amani.
nadhani jeshi la polisi wajisafishe na waache kutumiwa.
naona wamejisahau kuwa tunaishi nao mitaani.
 
Back
Top Bottom