Mwanaharakati Boniface Mwangi aondolewa mashitaka ya ugaidi, sasa akabiliwa na kosa la kumiliki risasi kinyume cha sheria

1Africa54

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2025
Posts
464
Reaction score
549
Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) nchini Kenya imeondoa mashitaka ya ugaidi dhidi ya Mwanaharakati Boniface Mwangi, ambaye sasa anakabiliwa na mashitaka ya kumiliki risasi kinyume cha sheria.

Mwangi, ambaye ameachiwa kwa dhamana, awali alishtakiwa kwa kusaidia shughuli za kigaidi kufuatia maandamano ya kupinga serikali yaliyofanyika tarehe 25 Juni, 2025. Mashitaka hayo ya awali yalizua mjadala mpana kuhusu haki za kiraia na uhuru wa kujieleza nchini Kenya.

Uamuzi wa DCI kuondoa mashitaka hayo ya ugaidi umepokelewa kwa hisia mseto, huku baadhi ya wanaharakati wakisema ulikuwa ni ushindi kwa demokrasia, na wengine wakihimiza uchunguzi wa kina kuhusu namna mashitaka ya ugaidi yalivyotolewa awali.

Suala hili linazidi kuvuta hisia na mijadala mitandaoni kuhusu nafasi ya wanaharakati katika jamii, uhuru wa kuandamana, na matumizi ya sheria za kupambana na ugaidi kwa malengo ya kisiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…